bayyinaat

Published time: 28 ,May ,2017      13:31:02
Unaweza kuona ni dua fupi kwa maneno na ambazo hazichukui hata dakika nyingi katika kuzisoma, lakini endapo tukiangalia lengo lake kubwa la kumkumbusha mwanadamu na kumuweka katika hali ya mawasiliano ya daima na mola wake, ndipo tutajua thamani ya dua hizo. Zifuatazo ni......
News ID: 92

Kwa hakika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi ambao unakuja kwa lengo la kumjenga mwanadamu na kumjulisha ya kwamba swala la kuambatana na muumba wake si swala la wakati maalumu pasi na wakati mwingine, na jambo hili tunaweza kuligundua endapo tutakuwa ni wenye kuusoma na kuuangalia mwezi huu kwa macho matatu, hebu angalia jinsi gani Mtume saww amekuwa ni mwenye kutufunza dua mbalimbali kuhusiana na mwezi huu, ili mradi tu mwanadamu asiwe ni mwenye kujisahau ya kwamba anatakiwa daima awe ni mwenye kushikamana na mola wake, na mfano wa dua hizo ni dua ambazo kila siku Mwislamu anatakiwa asome katika mwezi huu mtukufu. Unaweza kuona ni dua fupi kwa maneno na ambazo hazichukui hata dakika nyingi katika kuzisoma, lakini endapo tukiangalia lengo lake kubwa la kumkumbusha mwanadamu na kumuweka katika hali ya mawasiliano ya daima na mola wake, ndipo tutajua thamani ya dua hizo. Zifuatazo ni dua ambazo kwa kila siku ya mwezi huu kutakuwa na dua yake maalumu, Mwenyezi Mungu atujaalie kuufunga mwezi huu kwa imani na nia safi na hatimae kufikia lengo lililokusudiwa na Mwenyezi Mungu (swt).

دعاء اليوم الأول

Dua ya siku ya kwanza


اَللّهُمَّ اجْعَلْ صِيامي فيهِ صِيامَ الصّائِمينَ وَ قِيامي فيِهِ قِيامَ القائِمينَ ، وَ نَبِّهْني فيهِ عَن نَوْمَةِ الغافِلينَ ، وَهَبْ لي جُرمي فيهِ يا اِلهَ العالمينَ ، وَاعْفُ عَنّي يا عافِياً عَنِ المُجرِمينَ

"Ewe mola wangu, jaalia saumu yangu katika siku hii iwe ni saumu ya kweli, na visimamo vyangu viwe bi visimamo vya kweli, na unizindue kutoka katika kujisahau, na unisamehe makosa yangu ewe mwenye kusamehe wenye makosa”.



دعاء اليوم الثاني

Dua ya siku ya pili


اَللّهُمَّ قَرِّبْني فيهِ اِلى مَرضاتِكَ ، وَجَنِّبْني فيهِ مِن سَخَطِكَ وَنَقِماتِكَ ، وَ وَفِّقني فيهِ لِقِرائَةِ اياتِِكَ ، بِرَحمَتِكَ يا أرحَمَ الرّاحمينَ


"Ewe Mwenyezi Mungu, niweke karibu na unayoyaridhia, na niweke mbali na chuki na hasira zako, na nipe uwezo wa kusoma aya zako (Quran), kwa rehema zako ewe mbora wa wenye kurehemu”.


دعاء اليوم الثالث

Dua ya siku ya tatu



اَللّهُمَّ ارْزُقني فيهِ الذِّهنَ وَالتَّنْبيهِ ، وَ باعِدْني فيهِ مِنَ السَّفاهَةِ وَالتَّمْويهِ ، وَ اجْعَل لي نَصيباً مِن كُلِّ خَيْرٍ تُنْزِلُ فيهِ ، بِجودِكَ يا اَجوَدَ الأجْوَدينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie ndani ya siku hii uelewa na kuzinduka, n auniweke mbali kutokana na upuuzi na kuharibikiwa, na unijaalie fungu kutoka katika kila la heri unayoishusha katika siku hii, ewe mkarimu wa wakarimu”.


دعاء اليوم الرابع


Dua ya siku ya nne


اَللّهُمَّ قَوِّني فيهِ عَلى اِقامَةِ اَمرِكَ ، وَ اَذِقني فيهِ حَلاوَةِ ذِكْرِكَ ، وَ اَوْزِعْني فيهِ لِأداءِ شُكْرِكَ بِكَرَمِكَ ، وَ احْفَظْني فيهِ بِحِفظِكَ و َسَتْرِكَ يا اَبصَرَ النّاظِرينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie nguvu ya kutekeleza amri zako, na nijaalie raha ya kukutaja wewe, na uniambatanishe na kutekeleza shukrani kutokana na kunikirimu kwako, na unihifadhi ndani ya siku hii kwa uhifadhi wako ewe mjuzi wa wajuzi”.



دعاء اليوم الخامس

Dua siku ya tano



اَللّهُمَّ اجعَلني فيهِ مِنَ المُستَغْفِرينَ ، وَ اجعَلني فيهِ مِن عِبادِكَ الصّالحينَ القانِتينَ ، وَ اجعَلني فيهِ مِن اَوْليائِكَ المُقَرَّبينَ ، بِرَأفَتِكَ يا اَرحَمَ الرّاحمينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie katika siku hii ni katika wenye kusamehewa, na unijaalie kuwa ni katika waja wako wema, na unijaalie kuwa ni katika vipenzi vyako vya karibu, kwa haki ya huruma yako ewe mbora wa wenye kurehemu”.



دعاء اليوم السادس

Dua siku ya tano



اَللّهُمَّ لا تَخْذُلني فيهِ لِتَعَرُّضِ مَعصِيَتِكَ ، وَ لاتَضرِبني بِسِياطِ نَقِمَتِكَ ، وَ زَحْزِحني فيهِ مِن موُجِبات سَخَطِكَ بِمَنِّكَ وَ اَياديكَ يا مُنتَهى رَغْبَةِ الرّاغِبينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, usinitie udhalili katika siku hii wa kuyaelekea maasi juu yako, na wala usiniadhibu kwa hasira zako, na naomba unitoe kutoka katika yanayopelekea hasira na chuki zako, kwa haki ya uwezo wako ewe kimbilio la wenye matakwa”.



دعاء اليوم السابع

Dua siku ya saba



اَللّهُمَّ اَعِنّي فيهِ عَلى صِيامِهِ وَ قِيامِهِ ، وَ جَنِّبني فيهِ مِن هَفَواتِهِ وَاثامِهِ ، وَ ارْزُقني فيهِ ذِكْرَكَ بِدَوامِهِ ، بِتَوْفيقِكَ يا هادِيَ المُضِّلينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nipe uwezo wa kufunga na kusimama, na uniepushe na majanga na mabalaa yake, na nijaalie niweze kukutaja utajo wenye kudumu, kwa haki ya tawfiq na uwezo wako ewe mwongozo wa waliopotea”.



دعاء اليوم الثامن

Dua siku ya nane


اَللّهُمَّ ارْزُقْني فيهِ رَحمَةَ الأَيْتامِ وَ اِطعامَ الطَّعامِ وَاِفْشاءَ وَصُحْبَةَ الكِرامِ بِطَوْلِكَ يا مَلْجَاَ الأمِلينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nijaalie moyo wa kuwahurumia na kuwalisha mayatima, na kuongea na kueneza yaliyo mema, kwa haki ya fadhila zako ewe kimbilio la wenye matarajio”.



دعاء اليوم التاسع

Dua siku ya tisa


اَللّهُمَّ اجْعَل لي فيهِ نَصيباً مِن رَحمَتِكَ الواسِعَةِ ، وَ اهْدِني فيهِ لِبَراهينِكَ السّاطِعَةِ ، وَ خُذْ بِناصِيَتي إلى مَرْضاتِكَ الجامِعَةِ بِمَحَبَّتِكَ يا اَمَلَ المُشتاقينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie na mimi fungu kutoka katika rehema zako zilizoenea, na uniongoze kwa dalili zako zenye kuwa wazi, na unibebe kuelekea katika ridhaa yako zenye kukusanya, kwa hai ya mapenzi yako ewe tarajio la wenye kukupenda”.



دعاء اليوم العاشر

Dua siku ya kumi


اَللّهُمَّ اجْعَلني فيهِ مِنَ المُتَوَكِلينَ عَلَيْكَ ، وَ اجْعَلني فيهِ مِنَ الفائِزينَ لَدَيْكَ ، وَ اجعَلني فيه مِنَ المُقَرَّبينَ اِليكَ بِاِحْسانِكَ يا غايَةَ الطّالبينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nijaalie ni katika wenye kukutegemea wewe tu, na unijaalie ni katika wenye kufaulu kwako, na unijaalie ni katika wenye kuwa karibu nawe, kwa haki ya wema wako ewe lengo la watafutaji”.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: