Usalama wa roho na mwili - 3

MAMBO YANAYOSABABISHA UFUKARA

1) Zinaa.

2) Nyimbo na Miziki.

3) Kumfanyia Mwislamu hiana/ usaliti.

4) Kudhihirisha ufukara wakati ni mwenye uwezo.

5) Kuita Jina baya.

6) Kuendelea kukiuka amri za Mwenyezi Mungu.

7) Kulala baina ya Magharibi na Isha, na kulala kabla halijachomoza Jua.

8) Kukithiri kula vya Haramu.

9) Kuomba omba watu wakati si mwenye shida.

10) Kupuliza chakula.

11) Kutoheshimu Wazazi wawili.

12) Kutana Nywele wakati wa kusimama.

13) Kuamka kitanda kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo ilihali uko Uchi.

14) Kupuuzia Sala.

15) Kutoondosha Tandabui ndani ya Nyumba.

16) Kuchoma maganda ya Vitunguu maji na Vitunguu saumu.

17) Kula wakati wa Janaba.

18) Kuhifadhi vyombo vichafu ndani ya Nyumba.

19) Kulaani watoto na kusema uongo.

MAMBO YANAYOSABABISHA GHADHABU YA MWENYEZI MUNGU

1) Kupeana mkono na Mwanamke Ajinabi.

2) Matusi na (kuitana kwa) majina mabaya.

3) Kulala sana.

4) Uvivu mwingi.

5) Ulafi.

6) Zinaa.

7) Hiana na chuki dhidi ya Mwislamu.

8) Kumdhalilisha fakiri wa Kiislamu kwa sababu ya ufukara wake.

9) Kumheshimu na kumkirimu Tajiri kwa sababu ya Mali zake.

10) Kuwaghadhibisha wazazi wawili.

11) Kumsifia Mwovu.

12) Kumkatisha Tamaa anayekutumainia.

MAMBO YANAYOMPA MJA HESHIMA

1) Kujiepusha kuwaudhi watu.

2) Kumsamehe aliyekukosea na aliyekudhulumu.

3) Kukatia Tamaa na kufumbia macho ya Walimwengu.

4) Tabia Njema.

MAMBO YANAYOMDHALILISHA MWANADAMU

1) Kudharau amri za Mwenyezi Mungu.

2) Kughafilika kumkumbuka Mola wake.

3) Kuridhisha Watu kwa kile kinachomuudhi Mwenyezi Mungu.

4) Kuacha kutetea haki.

5) Kudhihirisha Uadui kwa Baba.

6) Kudhihirisha Uhasama kwa Waombaji.

7) Kutoheshimu watu wazima wala wazee.

8) Kumfedhehesha Muumini.

9) Kudhihirisha Uadui kwa Viongozi.

10) Kudhihirisha shida zako kwa kila Mtu.

11) Kumdharau Muumini.

12) Kuacha Bishara (Baada ya kuanzisha).

MAMBO YANAYOZUIA DU’A KUJIBIWA

1) Kula vya Haramu.

2) Kuacha kuamrisha mema na kukemea mabaya.

3) Pombe na kila cha upuuzi kama; Miziki na kuhifadhi vitendea kazi vya kamari ndani ya Nyumba.

4) Dhulma ya haki za wengine.

5) Kupenda Dunia.

6) Kutotilia umuhimu Sala.

MAMBO YANAYOPELEKEA DU’A KUPOKELEWA

1) Kutamka (بسم الله) mwanzo wa Du’a.

2) Kumtakasa Mwenyezi Mungu.

3) Kumsalia Mtume (s.a.w.w) na Aali zake.

4) Kutowahitajia watu.

5) Kuelekeza Moyo na kutumainia majibu ya Du’a.

6) Kung’ang’ania sana katika kuomba Du’a.

7) Kuombea Waumini (Du’a) arobaini kabla ya kujiombea.

8) Kusoma Aya mia moja za Qur’ani na baada ya Du’a kutamka mara saba (يا الله).

9) Kutimiza Du’a kwa kutamka (ما شاء الله لا حول ولا قوّة الّا بالله).

MAMBO YANAYOPELEKEA MWANADAMU KUSAMEHEWA

1) Kupeana mikono na Muumini.

2) Kufagia Msikitini.

3) Kuwasha Taa za Msikitini.

4) Kusindikiza Jeneza.

5) Kuumwa/ maradhi.

6) Kutembelea Wagonjwa.

7) Kufunga Saumu za Sunna.

8) Kumshibisha Mwenye Njaa.

9) Kumsalia Mtume (s.a.w.w).

10) Kuheshimu na kukirimu wageni waumini.

11) Kurefusha Sijida (katika Sala).

MAMBO YANAYOLETA MWISHO MWEMA

1) Kujiepusha kutumia neema za Allah mahala pasipostahili.

2) Kutotakabari kwa hisani ya Mwenyezi Mungu.

3) Kumheshimu anayependa Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w).

4) Kwenda Hijja mara mbili.

MAMBO YANAYOPELEKEA UZITO WA KUTOLEWA ROHO/ SAKARATUL MAUT

1) Kuhukumu kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu.

2) Kutoa ushuhuda wa Uongo.

3) Kutoheshimu wazazi wawili.

4) Kukiuka amri za Mwenyezi Mungu.

Sheikh : Juma. R. Kazingati.