DHAMBI YA KULAWITI; SEHEMU YA KWANZA


Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Kulawiti ni katika madhambi makubwa ambayo umeelezwa ubaya wake, kama ilivyopokelewa kutoka katika riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa maimamu wema mfano wa Imam Sadiq (a.s) na Imam Ridhaa (a.s). bali uharamu wake ni mkubwa mno kuliko zinaa.

Imepokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s): "Uharamu wa makalio ni mkubwa mno kuliko uharamu wa tupu ya mbele ya mwanamke, kwani Mwenyezi Mungu ameangamiza kauli kwa kosa ya dhambi ya tendo la kulawiti na hakuangamiza kaumu yoyote kwa dhambi ya zinaa”.[1]

Na amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Yeyote atakayemjamii mvulana ataletwa siku ya kiama ilihali yu katika janaba ambayo hakutakaswa na maji ya duniani na Mwenyezi Mungu atamghadhibikia na atamlaani, na atamuandalia moto wa jahanamu na hayo ni mafikio mabaya, kisha akasema tena (s.a.w.w); Hakika dhakari ipandayo juu ya nyingine hutikisika enzi ya Mwenyezi Mungu kwa kitendo hicho na hakika Mtu huyo ataletwa katika kifungo kisha Mwenyezi Mungu atamfungia juu ya daraja la Jahanamu, hadi atakapomaliza hesabu ya viumbe wote, kisha atafikishwa Jahanamu na ataadhibiwa kwa kila tabaka za jahanamu hadi atakapofikia kina cha Jahanamu na hatotoka ndanimo milele”.[2]

TENDO LA KULAWITI NI UKAFIRI:

Amesema Amirul muuminiin (a.s): "Kulawiti kisicho kuwa makalio ya mwanaume na kutenda kwa tupu ya mwanaume ni ukafiri”.[3]

JIWE LA ADHABU WAKATI KIFO

Kutoka kwa Abuu Baswir, kutoka kwa Abuu Abdillah (a.s) katika kauli yake (s.w.t):

" فَجَعَلْنَا عَالِيهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيهِمْ حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ".

"Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni”. Akasema (a.s): Hapana mja atokae katika dunia akiwa amehalalisha matendo ya watu wa Lut –Na katika Riwaya ya al- wasaail imekuja kwamba: Yeyote atakayekufa ilihali ni mwenye kuendekeza matendo ya kulawiti – hatokufa hivi hivi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamteremshia udongo ambao utapelekea hatima yake na wakati huo viumbe wengine hawatomuona”.[4]

ADHABU YA WATU WA LUT MADHALIMU:

Hakika Qur’ani tukufu imebainisha aina tatu za adhabu kwa watu wa lut: Upepo mkali uvumao, kunyeshewa mvua ya mawe na kugeuza mji wao juu kuwa chini, kisha akasema” "وَمَا هِي مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ"Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo”.[5]

KIJANA ALIYEMUUA MKUU WAKE:

Baada ya kijana mmoja kukiri kosa la kumuua mkuu wake katika zama za ukhalifa wa Omar, aliamuru Omar kijana kuuliwa, Imam Ali (a.s) alimuuliza kijana; Kwanini umemuua mkuu wako? Akamjibu: Amenilawiti kwa nguvu na nikamuua, Imam aliomba wafia kuhudhuria, aliwauliza; Je! Mmeshamzika? Wakasema; Ndio tunatoka kumzika, Imam alimuomba Omar kumchelewesha kijana kwa siku tatu, baada ya siku tatu walikuja ndugu wa marehemu.

MLAWITI HUKUTANA NA WATU WA LUT

Baada ya kuisha siku tatu, Imam alikwenda pamoja na Omar na wafiwa hadi kwenye kaburi lake, Imam (a.s) aliwauliza: Je! Hili ndio kaburi na mtu wenu? Wakasema: Ndio, akasema (a.s): Fukueni kaburi hadi kufika kwa mwanandani, walipofika kwa mwanandani walivuta shuka/ sanda hawakukuta kiwiliwili, Imam (a.s) alipaaza sauti ya kumtukuza Mwenyezi Mungu na akasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba sijadanganya, kwani nilimsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w) akisema: Yeyote atayekufa katika umma wangu na ametenda matendo ya watu wa Lut pasina toba hakika hatobakia ndani ya kaburi lake kwa masiku matatu kaburini mwake isipokuwa ardhi itampeleka mahali walipoangamia watu wa Lut na atafufuliwa pamoja nao.[6]

Itaendelea.........[1] Wasaail al- shia, juz 14, uk 249, mlango; Tahriim al- liwaat, hadithi 2, Furuu al- Kafiy, juz 5, uk 544, mlango; Al- liwaat, hadithi 1.

[2] Wasaail al- shia, juz 14, uk 249, mlango; Tahriim al- liwaat, hadithi 1, Furuu al- Kafiy, juz 5, uk 544, mlango; Al- liwaat, hadithi 2.

[3] Furuu al- Kafiy, juz 5, uk 544, mlango; Al- liwaat, hadithi 3.

[4] Wasaail al- shia, juz 14, uk 250, mlango; Tahriim al- liwaat, hadithi 7.

[5] Surat Hud, Aya 83.

[6] Ma’lim al- zulfaa (Madhumuni ya Riwaya).