DHAMBI YA KULAWITI; SEHEMU YA NNE

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


NINI MAANA YA LIWAAT?

Bila shaka kitendo cha kulawiti ni kitendi kibaya mno chenye kuchukiwa na Dhati ya Mwanadamu, hivyo ni wazi kwamba yeyote anayetenda dhambi hiyo, basi ni dalili ya uchache wa akili zake, na hutubainishia ya kwamba dhamira ya mtu huyo imekwisha pigwa muhuri wa kila ovu. Ambapo dhati yake mwenye haipendezewi kwa kitendo hicho cha haramu. Na suala la kutuliza matamanio kupitia uchafu huu wa kulawiti ni dhambi nzito mno, kama vile dhambi iliyopelekea Kaumu ya Nabii Luut kuangamizwa. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani tukufu Surat Ashuaa’raa, Aya ya 165- 166, anahutubia kwa kuwaparipia kaumu ya watu mfano wa hao ya kwamba:

"أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ * وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُمْ مِنْ أَزْوَاجِكُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ".

"Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?, Na mnaacha alichokuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!”.

Madhumuni ya Aya hii ni kwamba: Kwanini jamii ya Wanaume ulimwenguni huhujumu zaidi Wanaume wenzao kwa kitendo cha kijinsia?, ambapo mwawacha wanawake ambao Mwenyezi Mungu amekuumbieni kwa ajili ya jambo hilo (Sharti liwe kwa njia ya halali), hakika nyinyi mme ruka mipaka.

Hakika kitendo cha Kulawiti ni tabia ambayo ilikuwa imeshamili zaidi katika Kaumu ya Nabii Luut (a.s), ambapo uhalisia wake ni kwamba yeyote atendae dhambi hii si mwingine ila ni yule asiyekuwa na aibu wala haya, asiyekuwa na chembe ya heshima wala utukufu wa nafsi. Na Mtu huyo katika jamii hutazamwa na watu kwa jicho la mtu duni dhalili. Vile vile kutokana na uchafu huo na kwa mujibu wa mantiki ya kitaalamu ni kwamba; Anayelawitiwa hufafanishwa na nyama iliyokwisha oza yenye mafuta yanayotoa harufu chafu yenye kukera mno pindi atakapoisogelea mtu, hivyo anayetenda uchafu huo (Anayelawiti) anakuwa ni yule anayekula nyama hiyo, ambapo haraka sana hukumbwa na kila aina ya maradhi mazito.

Ibn Qaym (r.a) amesema: Ni bora zaidi anayelawitiwa kuuliwa kuliko kubakia hai, ili asieneze uchafu huo kwa wengine. Kwa sababu Mwanaume kujiuza ni mfano wa kuaga kila kitu chema katika jamii endapo kitaharibikiwa, na wale watakaojihusisha na kitendo hicho watakosa haiba usoni mwao na kukosa aibu na haya, kiasi kwamba hawatamwogopa hata Muumba wao, wala kuwaonea aibu viumbe wa Mwenyezi Mungu. Hivyo Manii ya mwenye kulawiti pindi yanaposhuka basi hutia dosari kubwa moyoni mwake mithili ya sumu inayotembea katika mwili wa Mtu.

Wataalamu wamesema kwamba: Mtendewa uchafu huo ni mbaya zaidi, na khabithi zaidi kuliko Mtoto wa zinaa, hivyo watu wasitarajie heri kutoka kwake, bali ni lazima wamtupilie mbali. Kwa sababu mwenye kulawitiwa pindi ataomba heri kwa Mola wake basi Mwenyezi Mungu hatompa mema. Hivyo hakuna elimu itayomnufaisha pindi atasoma, wala amali njema wala toba halisi itakayomwokoa, isipokuwa pindi atakapo penda Mwenyezi Mungu kumsamehe.

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.