ZINAA; SEHEMU YA KWANZA

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Katika madhambi makubwa ambayo kwamba umebainishwa bayana ukubwa wake ni Zinaa, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Maimamu watakatifu, mfano wa Imam Sadiq (a.s) na Imam Kadhim na Imam Ridhaa na Imam Jawaad (a.s) wameshuhudia ukubwa wa dhambi hiyo kwa mujibu wa Aya tukufu ya Qur’ani:

"وَالَّذِينَ لَا يدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلَا يقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يزْنُونَ وَمَنْ يفْعَلْ ذَلِكَ يلْقَ أَثَامًا. يضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يوْمَ الْقِيامَةِ وَيخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا".

"Na wale wasio mwomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara. Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka”.[1]

MAANA YA MADHARA YA MALIPO YA UBAYA:

Imepokelewa katika kitabu al- manhaj kwamba () katika aya hii ni jina la kiwanja katika jahanamu atakacho adhibiwa ndani yake wazinifu na imesimuliwa ya kwamba katika neno () kuwa ni kitu kipitacho ndani ya miili ya watu wa motoni kifananacho na damu pamoja na usaha.

Imepokelewa katika baadhi ya riwaya ya kwamba maneno mawili hayo yaliyokuja ndani ya Aya hii na kuongezea neno () lililokuja katika Aya tukufu (فَسَوْفَ يلْقَوْنَ غَيا) kuwa ni majina ya mashimo mawili ndani ya moyo wa jahanamu ambapo litupwapo jiwe ndani yake, huhitaji miaka sabini ili kufikia kwenye kina chake.

Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat baniy israa:

"وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا".

"Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbayaWala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya”.[2]

Ni kwa sababu zinaa ni sababu ya kukata kwa nasaba na kupotea kizazi na kubatilika urithi na kuvunjika silsila ya undugu na haki za wana juu ya wazazi wao na haki ya wazazi juu ya wana wao.

ATHARI ZA KIDNIA NA AKHERA KWA MZINIFU:

Amesema Mjumbe wa Allah (s.a.w.w): "Mzinifu hupata mambo sita, matatu duniani na matatu mengine akhera, ama matatu ya duniani ni kwamba hupoteza nuru yake na kusababisha ufukara na kuharakisha kifo cha ghafla, na ama ambayo ni kwa ajili ya akhera ni kupata ghadhabu za Mwenyezi Mungu na malipo mabaya na kudumu katika moto”.[3]

ADHABU YA MZINIFU KATIKA KABURI:

Na imepokelewa kutoka kwake (s.a.w.w): "Yeyote atakayezini na mwanamke wa Kiislamu au Kiyahudi au wa Kikristo au majusi, sawa huru au mtumwa, kisha hakutubia dhambi yake na akafa akiwa ni mwenye kung’ang’ania katika dhambi hiyo, Mwenyezi Mungu atamfungulia kaburini kwake milango mia tatu itokayo chatu na nge na nyoka wa motoni, ataungua hadi siku ya kiama, na atakapofufuliwa kaburini ataudhi watu kwa ubaya wa harufu yake na hapo atafahamika na watu kwa kile alichokitenda alipokuwa duniani hadi atakapoamrisha malaika kumpeleka motoni, tambua ya kwamba, Mwenyezi Mungu ameharamisha ya haramu na akaweka mipaka ya hududi hivyo hapana yeyote awezaye kubadilisha mabadiliko ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na atakayekiuka aliyoharamisha Mwenyezi Mungu ataharamisha maovu”.

WATU WOTE WATALAANI WAZINIFU SIKU YA HESABU:

Na imepokelewa kutoka kwa Amirul Muuminin (a.s): "Itakapofika siku ya kiama Mwenyezi Mungu atavumisha upepo mkali wenye harufu kali itakayowaudhi watu wote, hadi itakapowakirisha watu harufu hiyo, ndipo atanadi Mwenye kunadi na kusema, je! Mwajua ni harufu gani hii iwakerayo? Watasema: Hapana hakika imetukirihisha mno kero isiyo na kikomo, akasema (a.s): Kisha wataambiwa: Hakika hii na harufu ya tupu ambazo zimekutana na Mola wao zikiwa katika zinaa na ilihali hazijatubia makosa yao, hivyo muwalaani kwani amekwisha walaani Mwenyezi Mungu, na wakati huo hatobakia yeyote katika kisimamo cha kiama ila amesema: Mola wangu walaani wazinifu”.

ZINAA HULETA UFUKARA NA KIFO CHA GHAFLA:

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Itakapo kithiri zinaa baada yangu basi yatakithiri mauti ya ghafla”.

Na kutoka kwake tena (s.a.w.w): "Zinaa huleta ufukara na kuyafanya majumba kuwa magofu”.

Itaendelea.....[1] Al- Furqaan/ 68 – 69.

[2] Al- Israa/ 32.

[3] Furuu’ al Kaafiy, juz 5, uk 541, mlango; al- Zaaniy, Hadithi 1.