Mwanzo
Tafuta
Ni jambo ambalo lipo wazi kwamba katika dini ya Uislamu kulikuwa na vita nyingi mno ambazo Waislamu wakishinda, lakini ushindi ambao Mwenyezi Mungu anamuahidi mtume wake hapa ni ushindi juu ya kuufungua mji wa Maka kutoka katika mikono ya waabudu masanamu, hasa ukiangalia kwamba Waarabu walikuwa hawaamini kwamba itatokea siku moja Maka ikawa katika mikono ya Waislamu, na kama itatokea ikawa hivyo basi bila shaka Mtume atakuwa ni wa kweli na haki, maana haiwezekani ambaye ni mwongo kuja kuikomboa....
Imepokelewa katika riwaya kwamba uadui wa Abuu lahab kwa mtume na kwa Uislamu kwa ujumla haukuwa uadui mdogo, bali ulikuwa umefikia kiasi ambacho hata kama Abuu lahab alikuwa anaumwa hoi hakuweza kuvumilia kukaa kitandani huku Mtume akiendelea kulingania watu, bali alikuwa akimfuata kila kona ambayo alikuwa akienda huku akimwandama kwa maneno mabaya na matusi.........
Kwa hivyo basi ni kwamba kila jambo ambalo lipo katika dini na hata maisha yetu kwa ujumla linakuwa na falsafa na hekima yake, ama swala la kuijua au kutoijua hekima hiyo ni swala lingine kabisa, na ndio maana dini ya Kiislamu inapoona kwamba kuna ulazima wakubainisha hekima ile basi inafanya hivyo..........
“kama ni hivyo basi sitauabudu moto ambao umeabudiwa na ndugu yangu, na mimi nitaanzisha moto wangu na kuupa nadhiri zangu na nina imani kwamba zitakubaliwa tu.....”.