bayyinaat

Published time: 06 ,October ,2017      12:10:53
Hii hutubainishia ya kwamba, nafasi ya kuamrisha mema na kukemea mabaya katika harakati ya Imam Hussein (a.s) ni kwa anuani ya lengo na kusudio la Imamu (a.s). Katika ziara ya Mtukufu huyo pia inatuthibitishia hilo pia pale inaposema:..............
News ID: 104

Katika tamaduni za siku ya Ashuraa, tupata kugundua ya kwamba utawala dhalimu wa Yazid bin Muawiya ulikuwa ni utawala mkubwa mno wenye kusimamia maovu yote ya kijamii, na suala la kubarizi kwa ajili ya kupingana na kiongozi dhalimu mfano wa Yazid na kusimamisha haki na kukata utawala dhalimu, ni jambo jema mno katika Uislamu. Aidha suala la kuamrisha mema na kukemea mabaya, ni moja ya falsafa zenye hamasa kubwa mno lililopelekea kumwagika damu ya mashahidi katika viwanja vy akarbalaa.

Bwana wa mashahidi katika wasia wake alioandika na kumkabidhi nduguye Muhammad hanafiyya, anasema:

«أَنِّی لَمْ أَخْرُجْ أَشِراً وَ لَا بَطِراً وَ لَا مُفْسِداً وَ لَا ظَالِماً وَ إِنَّمَا خَرَجْتُ لِطَلَبِ الْإِصْلَاحِ فِی أُمَّهِ جَدِّی ص أُرِیدُ أَنْ آمُرَ بِالْمَعْرُوفِ وَ أَنْهَی عَنِ الْمُنْکَرِ وَ أَسِیرَ بِسِیرَهِ جَدِّی وَ أَبِی».

"Hakika mimi sikutoka kwa ajili ya kutafuta shari wala ugomvi wala kufanya uharibifu wala kwa dhulma, bali nimetoka kwa ajili ya kutafuta kutengeneza katika umma wa babu yangu, ninataka kuamrisha mema na kukemea maovu na nifuate nyayo ya babu yangu na baba yangu Ali bin abitalib”.[1]

Hii hutubainishia ya kwamba, nafasi ya kuamrisha mema na kukemea mabaya katika harakati ya Imam Hussein (a.s) ni kwa anuani ya lengo na kusudio la Imamu (a.s). Katika ziara ya Mtukufu huyo pia inatuthibitishia hilo pia pale inaposema:

«اَشْهَدُ اَنَّكَ قَدْ اَقَمْتَ الصَّلوةَ وَآتَيْتَ الزَّكوةَ وَاَمَرْتَ بِالْمَعْروُفِ وَنَهَيْتَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَجاهَدْتَ فِى في سبیل اللَّهِ حتی اتک الیقین».

"Ninashahidilia ya kwamba Wewe umesimamisha Sala na umetoa Zaka na umeamrisha mema na ukamema maovu na ukapambana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu hadi ikakufikia yakini”.[2]

Hakika taabiri hii, hutudadafulia kina cha wajibu wa suala hili kidini ambalo hulitanguliza mbele katika matini za jihadi ya damu, pia na suala la kuamrisha mema na kukataza mabaya, ni katika mambo ya wajibu, hadi kusimama kwa ajili ya kusimamisha uadilifu na kupindua utawala batili na kubadilisha nidhamu mbovu za kijamii pia ni jambo limewajibishwa na dini.

Imam Hussein (a.s), baada ya kukataa kutoa bai’a kwa yazidi na mikutano ambayo imetokea baina yake pamoja na Walid na Marwan, alikwenda kando ya kaburi la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na usiku alifanya ibada hapo, vile vile katika dua yake kwa Mola wake, alidhihirisha mapenzi yake katika suala ya kupenda mema kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyzi Mungu na kuahidi kufuata nyenzo za Babu yake na Baba yake, alisema maneno haya matukufu:

«اللهم اني احب المعروف و انكر المنكر و أنا اسألك ياذالجلال و الاكرام بحق القبر و من فيه الا اخترت ما هو لك رضي و لرسولك رضي».

"Mola wangu hakika Mimi ninapenda mema na ninachukia mabaya, na mimi ninakuomba Ewe mwenye utukufu na mkarimu kwa haki ya kaburi na aliyekuwa ndani yake ila umeniteulia lile ambalo ni lenye kukuridhisha wewe na Mjumbe wako”.

Imeletwa kwenu na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.[1] Rejea: Hayaatul Imamul Hussein (a.s), juz 2, uk 246 na 288.

[2] Tazama: Mafatihul Jinaan, ziara tofauti za Imam Hussein (a.s).


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: