bayyinaat

Published time: 06 ,October ,2017      12:13:45
Binti ambaye aliyemsaidia Baba yake katika mapambano dhidi ya makafiri wa mji wa Makka, katika Bonde la Abutalib. Na kustahamili mazito yaliyomsibu Baba yake, akiwa ni mwenye umri wa miaka saba, au nane kwa mujibu wa hitilafu za riwaya, hadi alipofariki Abutalib...........
News ID: 105

Binti ambaye aliyemsaidia Baba yake katika mapambano dhidi ya makafiri wa mji wa Makka, katika Bonde la Abutalib. Na kustahamili mazito yaliyomsibu Baba yake, akiwa ni mwenye umri wa miaka saba, au nane kwa mujibu wa hitilafu za riwaya, hadi alipofariki Abutalib.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akiwa pekee yake pasi na wa kumliwaza, wanyonge wote wamemfanya yeye kuwa ndio kimbilio, lakini ni nani wa kumfuta yeye vumbi la wake uso? Kwa kipindi fulani alikuwa bi Khadija, ambapo kwa sasa hayupo tena. Alikuwa Abutalib kwa kipindi fulani ambapo na yeye kwa sasa hayupo. Katika mazingira mfano wa hayo alikuwa katika hali mbaya ya njaa na kiu, baridi kali na joto la jangwa kipindi cha miaka mitatu ya bonde la Abutalib ambapo kilikuwa kipindi kigumu mno cha maisha ya Mtume, na akiwa pamoja na Waislamu wachache, aliishi kwa maisha ya kutengwa; hakika binti huyu alikuwa ni mfano wa malaika mwokozi kwa ajili ya Mtume; mfano wa Mama kwa babaye, mfano wa mlezi mkubwa kwa mtu mwenye shakhsiya kubwa, aliyestahamili na kuvumilia matatizo makubwa. Alikuwa ni mwenye kumliwaza Mtume, alibeba majukumu ya babaye, alimuabudu Mola wake, aliikuza Imani yake, alijijenga mwenyewe na hatimaye kushikamana na njia ya nuru ya kuelekea kwa Mola wake kwa moyo wake wote. Ambapo hayo ni vigezo ambavyo humfikisha mwanadamu kwenye ukamilifu.

Aidha katika kipindi cha hijira, mwanzoni mwa kipindi cha ujana wake, kipindi ambacho alipoolewa pamoja na Imam Ali bin Abitalib (a.s), kwa mahari yake na maandalizi ya harusi yake; ambapo watu wote hufahamu ni jinsi gani yalikuwa ni maandalizi ya kawaida na ya mazingira ya kimaskini, binti ya mtu wa kwanza ambaye ni mbora kuliko viumbe wote anaolewa na kijana aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu mtukufu baada ya Mtume kushikilia majukumu ya kuongoza umma.

Mumewe aliyekuwa katika umri wa ujana ambaye daima alikuwa katika viwanja vya vita; ama katika mazingira ya matatizo na ugumu wa maisha, Bi Fatima (a.s), alikuwa ni kinara kwa ajili ya marejeo ya watu na Waislamu kwa ujumla.

Yeye alikuwa ni mwanamke mchapa kazi, na katika mazingira ya kimaisha ya namna hayo alisimama imara kuendesha maisha yake kikamilifu; alilea watoto wake mfano wa Hassan na Hussein na Zainab; alimuenzi mume mfano Ali na kumridhisha Baba ambaye ni Mtume! Alifungua njia ya ufunguzi na ngawira pia, ni mwanamke ambaye hakujiweka wazi na mapambo ya kidunia kama walivyokuwa wanawake wengine.

Imam Ali (a.s) anasema haya kuhusu Bi Fatima Zahra (a.s) kwamba:

«ما اغضبنى و لا خرج من امرى».

"Kamwe hata siku moja mwanamke huyu katika kipindi cha ndoa yetu hakuwahi kunighadhibisha, na hata siku moja hakupinga amri yangu”.

Hivyo bibi Fatima (a.s) kwa utukufu wake na utakatifu wake, katika mazingira ya nyumbani, kwa anuani ya mke na mwanamke wa nyumbani; ni mfumo ambao Uislamu unayouzungumzia.

MUJAHIDI WA KUIGWA:

Jihadi za Bibi huyo katika Nyanja tofauti; hakika ni jihadi za kuigwa.

1. Katika kutetea Uislamu.

2. Katika kutetea Wilaya na Uimamu.

3. Katika kumhami Mtume (s.a.w.w).

4. Katika kumlinda Kiongozi wa Uislamu, yaani Imam Amirul muumin ambae ni Mumewe, ambapo tunakuta Imamu huyo katika kumsifu Bibi Zahra anasema: "ما اغضبنى و لا خرج من امرى. "Katu hakuniudhi wala kunighadhibisha, na kamwe hakutoka nje ya Utii wangu”. Rejea: Bihar al Anwar: juz 43, uk 134.

Bibi Fatima Zahra pamoja na utukufu na daraja yake, katika mazingira ya nyumbani, alikuwa ni Mke na Mwanamke bora, kama Uislamu usemavyo na umtakavyo Mwanamke kuwa.

BIBI FATIMA NI MAMA WA PEKEE:

Bibi Fatima Zahra (a.s) jinsi alivyokuwa akiwapenda wanae, hata katika siku za maisha yake ya mwisho alikuwa wa mbele zaidi kwao, na alimuusia Mumewe Amirul muunin na Babae kuhusu wanae.

Bibi Fatima akiwa katika kitanda cha umauti na kukaribia kuitikia wito wa Mola wake, aliusia nasaha aina mbili:

1. Amchague mke, atakayekuwa mpole kwa wanae.

2. Apende wanae na wajihisi uwepo wa Baba yao katika maisha yao.

Hapana shaka ya kwamba Imam Ali (a.s) ni maasum, na katu maasum hatendi dhambi, hivyo ataweza kuishi na wanae kwa upendo na ukarimu, ila wasia wa Bibi Fatima katika hali ile, ulikuwa ni ujumbe wa mapenzi ya Mama kwa wanae, na hiyo ilikuwa kwamba wanae wasinyongeke kwa kuondokewa na Mama.

Licha ya ujumbe wa nasaha ya Bibi huyo Mtukufu kuhusu wanae, bali uendelee kubaki kuwa ni hisia za umama kwa wanae, nao pia wahisi mapenzi ya Mama yao hata baada ya kufariki kwake.


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: