bayyinaat

Published time: 08 ,October ,2017      10:33:21
Sifa ni zake Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, na sala la amani zimuendee mbora wa walimwengu bwana wa manabii na mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye mbinguni ameitwa kwa jina la; Ahmad, na ardhini akaitwa kwa jina la; Abal Qaasim Muhammad, yeye pamoja.....
News ID: 111

Sifa ni zake Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, na sala la amani zimuendee mbora wa walimwengu bwana wa manabii na mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye mbinguni ameitwa kwa jina la; Ahmad, na ardhini akaitwa kwa jina la; Abal Qaasim Muhammad, yeye pamoja na Aali zake watakatifu na masahaba wake wema,

Ndugu msomaji wangu, hizi ni sifa hasa na masharti pamoja na mazingira ya kiroho na kimwili kutoka katika maneno ya maimamu watakatifu (a.s).

MAMBO YANAYOLETA SIHA YA MWILI

1) Safari.

2) Funga (Swaumu)

3) Kujiepusha kutema mate msikitini.

4) Kula kidogo.

5) Kunywa maji katika hali ya kusimama wakati wa mchana.

6) Kula wakati wa kuhisi njaa.

7) Kumeza chakula laini wakati wa kutafuna.

8) Kutobana mkojo wakati wa kulala.

9) Kunywa maji kidogo.

10) Kunywa maji ya Mvua.

11) Kuosha mikono kabla ya kula.

12) Kusali Sala za usiku.

MAMBO YANAYOSABABISHA UGONJWA

1) Kutokula chakula cha Usiku.

2) Kuvimbiwa.

3) Kula baina ya baada ya chakula cha mchana na kabla ya cha Usiku.

4) Kunywa katika hali ya kusimama wakati wa Usiku.

5) Kunywa maji katikati ya Chakula.

6) Kukaa Juani kwa muda mrefu.

7) Kula Nyama iliyokaushwa kwa wingi.

8) Kupanda ngazi mara kwa mara.

9) Kufanya tendo la ndoa na Mwanamke mtu mzima.

10) Kula sana samaki.

11) Ghamu kwa wingi na huzuni nyingi.

MAMBO YANAYOPENDEZESHA USO NA KULETA RANGI YA KUVUTIA

1) Kula vitunguu maji kwa wingi.

2) Kula mafuta ya Zaituni.

3) Kula kwa wingi Bilingani.

4) Kula komamanga.

5) Kuondosha Nywele za Puani.

6) Kunyoa Nywele za kichwani.

7) Kula kidogo na kutoshiba zaidi.

MAMBO YANAYOLIPA NGUVU TUMBO NA UTUMBE WAKE

1) Kunywa maji ya Waridi tisa.

2) Kula komamanga na mbegu zake.

3) Kula Baqal haad na maganda yake.

4) Kula Spinachi (Mbogamboga).

5) Kupiga mswaki.

6) Kula Tufaha.

7) Kula Vitumbua kwa wingi.

8) Kunywa maji ya Baridi.

MAMBO YANAYOZIDISHA NGUVU ZA KIUME

1) Kula Karoti kwa wingi.

2) Kula Vitunguu maji kwa wingi.

3) Kula Nyama pamoja na Mayai.

4) Kula komamanga Tamu.

5) Kula kwa wingi Kuzbara.

6) Kunywa maziwa.

MAMBO YANAYODHOOFISHA NGUVU ZA KIUME

1) Kukuza Nywele za siri.

2) Kuvaa viatu vyeusi.

3) Funga (Swaumu).

4) Kula Sidhabi/ fayjal.

MAMBO YANAYOSABABISHA UGONJWA WA UKOMA

1) Kula wakati umeshiba.

2) Kula na kunywa wakati ni mwenye janaba.

3) Kuoga na Kutia Udhu kwa maji yaliyopigwa na Jua.

4) Kufanya tendo la ndoa na Mwanamke mwenye hedhi.

MAMBO YANAYOSABABISHA UJUNUNI

1) Kunya katikati ya makaburi.

2) Kutembelea kiatu kimoja.

3) Kulala pekee ndani nyumba.

4) Kukosa utulivu.

5) Kulala kabla ya kuosha mikono.

MAMBO YANAYOZUIA UJUNUNI

1) Kukata kucha siku ya Ijumaa.

2) Kutoa Sadaka.

3) Kula chumvi.

4) Kula Mdalasini wakati wa chakula.

5) Kusoma sana Surat Yaasin mara kwa mara.

MAMBO YNAYOUPA MWILI NGUVU

1) Kula Nyama.

2) Kula Vitunguu maji mara kwa mara.

3) Kula Baqala Haad.

4) Kula Zaituni kwa wingi.

5) Kula komamanga.

6) Kula zabibu kavu.

7) Kunywa sana maziwa.

8) Kutoingia msalani wakati ni mwenye Njaa.

9) Kunyoa nywele za mwilini.

MAMBO YANAYODHOOFISHA MWILI

1) Kutokula Chakula cha Usiku.

2) Kula udongo.

3) Kuoga maji ya baridi bafuni.

MAMBO YANAYOSABABISHA MAAMBUZI YA KIBOFU CHA MKOJO

1) Kubana mkojo kwa muda mrefu .

2) Kubana Manii wakati wa matamanio.

3) Kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu sana.

4) Kutokojoa baada ya kutoka Manii.

MAMBO YANAYOKONDESHA

1) Kula nyama iliyokaushwa kwa wingi.

2) Kuoga kila siku.

3) Kufanya tendo la ndoa na Wanawake (Wakongwe).

4) Kula sana Mayai.

5) Kula sana Samaki.

6) Kuhuzunika sana (Mawazo).

MAMBO YANAYOZIDISHA UPEO WA AKILI

1) Kula sidhabi/ fayjal kwa wingi.

2) Kula siki.

3) Kupiga mswaki.

4) Kufanya Hijamu.

5) Kujipulizia kwa wingi manukato.

6) Kutaka ushauri.

7) Kusafiri.

8) Kufanya Biashara.

Sheikh : Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: