bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2017      11:28:16
Je, kuna ulazima wowote wa mwanadamu kumjua Mwenyezi Mungu?, kama ndio basi ni njia zipi sahihi za yeye kuweza kufikia katika kumjua Mwenyezi Mungu?..........
News ID: 13

KUMJUA MWENYEZI MUNGU (SWT)


nza kabisa tumshukuru mola ambaye ametupatia uwezo wa kukutana na kuweza kupeana mawili matatu katika mwanzo huu wa mlolongo wa makala zetu ambazo zinalenga maswala ya kiitikadi kwa ujumla. Bila shaka kila mwanadamu ndani ya nafsi yake anahisi kwamba kuna jambo ambalo anataka kulifikia, lakini bado kuna bakia na jambo moja ambalo ndio msingi wa mambo mengi ambayo tunayashuhudia katika ulimwengu huu, jambo lenyewe ni kwamba vipi mtu anaweza kufikia katika jambo tunalokusudia. Na hapa najaribu kuliweka jambo ambalo mwanadamu anatamani kulifikia kwamba ni lile lengo ambalo Mwenyezi Mungu aliweza kufanya ndio ufaulu wa kila mwanadamu katika maisha yake ya hapa duniani na hata kesho akhera kwa ujumla, maana hakuna kitu ambacho ni kizuri kwa mwanadamu kama kufikia lengo ambalo muumba wake anataka afikie.

 

Kwa msingi huu basi tunafikia katika hatua ya kutambua kwamba kumbe huyu mwanadamu kwanza ana muumba wake, pili ni kwamba muumba wa huyu mwanadamu anataka na anapenda kuona mwanadamu amefikia katika malengo matakatifu ambayo yatakuwa ni faida kwa huyuhuyu  mwanadamu.

Lakini je, ni jambo ambalo lipo wazi kwa kila mmoja wetu kwamba kuna muumba na anasifika na sifa gani?, au kwamba kuna malengo ambayo huyu muumba anataka sisi tuyafikie?, la hasha! Maana kama ingalikuwa hivyo basi kusingekuwa na tofauti mbalimbali katika kumuelekea huyo muumba. Hivyo kutokana na hayo yote kunakuwa na umuhimu wa kila mwanadamu kwanza kuweza kumtambua muumba wake pamoja na sifa zake anazostahiki kusifiwa nazo, pia kuweza kutambua sifa ambazo hapaswi kusifiwa nazo, na hatimaye ndio ataweza kutambua kwamba muumba mwenye sifa kama hizi atakuwa na malengo gani ambayo anataka mimi niyafikie.

 

Ni ipi njia sahihi ya kumjua Mwenyezi Mungu?, na je, kuna ulazima wa kumjua Mwenyezi Mungu?. Haya ni maswali mawili ambayo yatakuwa mwongozo mzima wa mada yetu kwa siku ya leo.

NJIA SAHIHI YA KUMJUA MWENYEZI MUNGU

Inawezekana kukawa na njia mbalimbali katika kujibu swali hili, lakini hatutakuwa na njia ambayo ni bora zaidi kwetu, kama kumtambua Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwake mwenyewe. Na hapa kwetu sisi kama Waislamu hatutakuwa na marejeo zaidi ya kurejea katika maneno yake matakatifu ambayo kama kutakuwa na njia nyingine basi yeye mwenyewe atatuelekeza.

Lakini katika jambo hili, kunaweza kukawa na mswali mawili matatu ambayo tunaweza kujiuliza, kama ambavyo ni lazima pia yaweze kupatiwa ufumbuzi sahihi. Moja ya maswali hayo  ni kwamba, je Quran imeelezea juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, mpaka sisi kupia Quran tuweze kusema kuwa tumegundua uwepo wake na hatimaye tuweze kutambua sifa zake?.

Katika kujibu swali hili, kuna rai mbili ambazo tunaweza kuzileta hapa, na kisha kuweza kubainisha rai sahihi kuhusiana na swali husika.

Itaendelea......

 
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: