bayyinaat

Published time: 13 ,February ,2017      22:30:56
Imekuwa labda ni jambo ambalo hufasiriwa vibaya katika jamii zetu pindi linapokuja swala la kwamba ni nani anakuwa na jukumu la kupangilia mambo ya familia husika kati ya mwanaume na mwanamke, je, ni nani hasa ana jukumu hilo?.
News ID: 15


Swali:

Mwenyezi Mungu anasema:

 (مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ).

"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda”. Nahl; 97

Mungu, ameelekeza maamuzi yake kwa Waislamu, wanaume na wanawake kwa usawa lakini nani ambae hupangilia majukumu kati ya mwanamke na mwanamume? Dini au jamii? Ni mwanamume peke yake anapaswa kuhusika na siasa? Ni ipi nafasi ya Uislamu juu ya haki za wanawake katika siasa, kama vile haki ya kupiga kura na haki ya kugombea halmashauri za ubunge na ofisi za umma? Na ni lipi jukumu la mwanamke katika masuala ya umma na taifa? Je! Huingia uongozi wa mwanamke kuongoza wanaume katika nafasi hii?

Jawabu:

Aya tukufu inaonyesha kwamba wanaume na wanawake watakapo simamia utendaji wa amali kwa kumuelekea Muumba, na vilevile kazi inayotakiwa kwa mtu binafsi na maisha ya kijamii pia, na akasimamia majukumu yake kwa upande wa jamii, basi ataishi maisha mema katika dunia hii na atalipwa mema kwa yale aliyofanya.

Lakini ni upi wadhifa wa mwanamume? Na ni ipi kazi ya mwanamke? Aya si katika nafasi ya kulibainisha hilo, na haitumiki kwamba wadhifa binafsi wa Mwanaume au kijamii ni sawa na wadhifa wa Mwanamke, bali si mantiki kulinganisha hilo. Kwani sheria, akili na desturi hupambanua wadhifa wa kila mmoja (Mwanaume na Mwanamke) kulingana na uwezo wao na uwezo wa mwili na akili, na kwa msingi wa majukumu yao na ufanisi katika jamii ya Wanadamu, kama vile haki za Mwanaume na Mwanamke huwa tofauti kisheria na kuwa mfuasi kama inavyotakiwa kikawaida wanaume na wanawake ni kwa misingi ya majukumu ya kila mmoja.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: