bayyinaat

Published time: 02 ,March ,2017      12:27:22
.......................Kutokana na tafiti mbalimbali juu ya mwanadamu kama mwanadamu, na pia baada ya kubainisha maana halisi ya neno tamaduni, tunafikia katika maana........
News ID: 23

Utangulizi

kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

Kila sifa iliyokuwa njema inamstahiki Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote, ambaye hana mfano katika wasiokuwa yeye. Kisha sala na amani na salamu nazipeleka kwa kiongozi wa umma huu ambaye ni mtukufu Mtume (saww) pamoja na kizazi chake kitakatifu,

Hakika miongoni mwa sifa ambazo dini ya Kiislamu imepambika nazo, ni kwamba kila mafundisho ambayo amekuja nayo mtukufu Mtume Muhammad (saww), basi yatakuwa ni yenye kuwa na uongofu na mafundisho ya kuchukuliwa na walengwa wa ujumbe na mafundisho yale. Na hali hii si kwamba tunaikuta tu katika kitabu kitakatifu alichokuja nacho ambacho ni Quran, bali pia hata katika mwenendo mzima wa bwana Mtume kuanzia maneno, vitendo na hata mambo ambayo ameyaona  na kuyapitisha kwa ridhaa yake.

Na tunaweza kuchukua mfano mdogo lakini ukawa na maana kubwa sana katika kuthibitisha jambo  hili, nao ni pale tunaporejea katika baadhi ya aya takatifu za Quran, tunakuta kwamba Mwenyezi Mungu (swt) anatunukulia na kutuelezea baadhi ya habari za watu waliopita kuanzia namna ya maisha waliyokuwa wakiishi, sababu za wao kuishi maisha yale, na je walifanikiwa au walifeli katika maisha yale, na mpaka mwisho kabisa tunakuja kuelezewa mwisho wao ulikuwa vipi, je, ulikuwa ni mwisho mzuri, au ulikuwa ni mwisho mbaya? Na ni mambo gani ambayo yalipelekea wao kufikia mwisho ule? Haya yote tunayakuta ndani ya Quran tukufu yakiwa yameelezewa kwa kirefu.

Lakini jambo la muhimu kwetu ni kuweza kuchukua baadhi ya mambo katika visa na habari kama hizi ambazo zimekuja ndani ya kitabu hiki kitakatifu, na kuweza kutambua kwamba, sababu ya kuweza kuwa na mwisho mzuri au mbaya ni namna ambavyo mwanadamu anajipangia jinsi ya kuishi au kwa maana nyengine ni kwamba ni aina gani ya mwanadamu anaichagua katika kuishi? Hii aina inaweza kuwa sababu ya kuendelea na kuwa na mwisho mzuri, au pia inaweza kuwa sababu ya kufeli na kuwa na mwisho mbaya.

Kama ambavyo sisi ambao leo hii tunataka kujua sababu za kuendelea au kuanguka kwa tamaduni fulani, ni lazima kutambua kwanza kwamba, tamaduni ni ile namna ambayo wale waliopita waliweza kukabiliana na maisha waliyokuwa nayo, kama ambavyo tutakuja na kuelezea kwa kirefu zaidi.

Kwa maana hiyo basi, swala la kuweza kutambua sababu zilizopelekea kuanguka au kuendelea kwa tamaduni fulani ni swala muhimu mno, kwani ndani yake tunaweza kutambua kwamba watu wale waliishi namna gani mpaka ikawa sababu ya kuendelea kwa tamaduni yao, na mpaka kufikia kuwa na mwisho mzuri, kama ambavyo pia tunatambua kwamba watu wale walikuwa na mfumo upi ambao ulipelekea kuanguka kwa jamii na tamaduni zao kwa ujumla na hatimaye kuwa na mwisho mbaya, ili na sisi kupitia wao tuweze kuchagua misingi sahihi ya kuweza kuendeleza tamaduni zetu, na hatimaye kuwa na mwisho mzuri.

Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) katika makala hii, tutajaribu kutumia njia ambayo ndio sahihi katika kusoma jambo lolote ambalo linahitajia kupimishwa na jambo lingine, nayo ni njia ya kusoma na kuangalia tamaduni zilizopita ili kuzifanya kama kioo na kipimo katika maisha yetu na tamaduni zetu pia.

Na tutaanza kwa kueleza kwanza maana ya tamaduni, kisha kuja na rai mbalimbali juu ya sababu ya kuanguka au kuendelea na tamaduni hiyo, na kisha tutakuja na rai au mtazamo wa Quran tukufu katika kuelezea sababu za kuanguka au kuendelea na tamaduni hizo.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: