bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      20:54:38
"Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu”. Mwenyezi Mungu ndani ya Aya hii anasema kwamba: Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu yaani mali yake kwa matarajio ya kurudishiwa maradufu, na sababu ya hili ni kwamba badala ya kutoa atumie neno kukopesha, ambapo mlipaji si mwingine ila ni yeye Mwenyezi Mungu mwingi
News ID: 257

UTANGULIZI.

Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, sala na amani zimuendee mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w), Yeye pamoja na Aali zake watakatifu (a.s), na laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya maadui zao wote.

Ama baada ya hayo, ni kwamba jamii za binadamu ni mfano wa mwili mmoja, lengo la maisha ni kumnyenyekea Mwenyezi Mungu ambapo hufungamana na ule ule ukamilifu wa kweli, yapo baadhi ya masuala ambayo kwamba ni yenye taathira za awali za kufikia kwenye ukamilifu huo, ama tangulizi hizi za awali ni zenye taathira kubwa mno katika lile lengo la kufikia kwenye ukamilifu, vile vile jamii fukara, ambayo ni moja ya vifungu vya matatizo ya kiuchumi inaweza ikasababisha jitihada za kumfikia Mwenyezi Mungu na kufikia ukamilifu husika, Uislamu umewahamasisha Waumini kuhusu kutoa Mali zao kwa njia ya wajibu wa Khums(Moja ya tano) na zaka: kutoka katika kile kiasi kilichozidi ya mali yake).

Kwa kuzingatia matilaba hapo juu katika utangulizi huu tumeangalia kwa mujibu wa faida za sadaka, zaka na khumsi za kidunia na akhera kwa mujibu wa Quran na maneno ya maasumina (a.s).

MADHUMUNI YA SADAKA KWA MUJIBU WA QUR’ANI

1. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (s.w.t):

«فَفِدْيةٌ مِنْ صِيامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ...».

"Basi atoe fidia kwa kufunga au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama”.[1]

2. Amesema tena (s.w.t):

«قَوْلٌ مَعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيرٌ مِنْ صَدَقَةٍ يتْبَعُهَا أَذًى وَاللَّهُ غَنِي حَلِيمٌ».

"Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole”.[2]

3. Amesema tena katika kauli nyingine:

«لَا خَيرَ فِي كَثِيرٍ مِنْ نَجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَينَ النَّاسِ».

"Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu”.[3]

4. Amesema tena katika kauli hii:

«خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِمْ بِهَا وَصَلِّ عَلَيهِمْ».

"Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema”.[4]

5. Amesema tena:

«يا أَيهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَينَ يدَي نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً».

"Enyi mlio amini! Mnapo sema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu”.[5]

6. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (s.w.t):

«إِنْ تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِي وَإِنْ تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيرٌ لَكُمْ».

"Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu”.[6]

7. Amesema tena (s.w.t):

«يمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ».

"Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi”.[7]

8. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

«إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ فَرِيضَةً مِنَ اللَّهِ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ».

"Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima”.[8]

9. Amesema tena katika kauli hii:

«يا أَيهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَى».

"Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimango na maudhi”.[9]

Pamoja na yote haya ndani ya Qur’an tukufu katika Aya ya 10 ya surat Hadid imekuja kwamba:

«مَنْ ذَا الَّذِي يقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ».

"Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu”.

Mwenyezi Mungu ndani ya Aya hii anasema kwamba: Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu yaani mali yake kwa matarajio ya kurudishiwa maradufu, na sababu ya hili ni kwamba badala ya kutoa atumie neno kukopesha, ambapo mlipaji si mwingine ila ni yeye Mwenyezi Mungu mwingi wa neema.

Hivyo mtoaji kwa mujibu wa Aya za Mwenyezi Mungu ni mfano wa yule anaye kopesha. "Ambapo ni mkopo mwema” ambao huutoa kwa ridhaa na ikhlaas (nia thabiti) katika njia iliyokuwa nzuri. Ambapo pia Mwenyezi Mungu atamrudishia maradufu.

----------------

Imeandaliwa na Sheikh Juma Kazingati.[1] Baqara/ 196.

[2] Baqara/ 263.

[3] Surat an- Nisaai/ 114.

[4] Surat at- tawba/ 103..

[5] Surat al mujaadala/ 12.

[6] Surat al Baqara/ 271.

[7] Surat al Baqara/ 276.

[8] Surat at- tawba/ 60.

[9] Surat al Baqara/ 264.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: