bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:20:36
Katika Aya hii imeashiriwa uhakika huu ya kwamba watu wenye imani utoaji wa sadaka kwa njia ya Mwenyezi Mungu ambazo zinaambatana na masimango na adha, ni batili na isiyo na thamani.
News ID: 261


SHARTI LA SITA: ni kwamba sadaka na utoaji visiambatane na adha wala masimango.

Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:

«يا أَيهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَى كَالَّذِي ينْفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ».

"Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimango maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu”.[1]

Katika Aya hii imeashiriwa uhakika huu ya kwamba watu wenye imani utoaji wa sadaka kwa njia ya Mwenyezi Mungu ambazo zinaambatana na masimango na adha, ni batili na isiyo na thamani.

KHABARI NA RIWAYA ZA KUKEMEA MASIMANGO NA ADHA KATIKA UTOAJI NA SADAKA.

1. Katika kitabu (waqaai’ul ayaa) imenukuliwa kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuwa amesema:

«ألمنان بما یعطی لا یکلمه الله ولا ینظر إلیه ولا یزکیه».

"Mwenye kutoa kitu na kusimanga, Mwenyezi Mungu hatoongea naye, na hatomtazama na hatomtakasa”.

2. Imam Sadiq (a.s) amesema:

«من أَنْفَقَ مَالَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاةِ اللَّهِ قَالَ فَمَنْ أَنْفَقَ مَالَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاةِ اللَّهِ ثُمَّ امْتَنَّ عَلَى مَنْ تَصَدَّقَ عَلَيْهِ كَانَ كَمَنْ قَالَ اللَّهُ‏: أَ يَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَنْ تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِنْ نَخِيلٍ وَ أَعْنابٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهارُ لَهُ فِيها مِنْ كُلِّ الثَّمَراتِ وَ أَصابَهُ الْكِبَرُ وَ لَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفاءُ فَأَصابَها إِعْصارٌ فِيهِ نارٌ فَاحْتَرَقَت‏».

"Mwenye kutoa mali yake kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wake, kisha akamsimanga yule aliyempa sadaka, ni mfano wa yule ambaye amemsema Mwenyezi Mungu katika Aya hii tukufu ya kwamba: "Je! Yupo mmoja wenu anaye penda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu ipitayo mito kati yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia naye hali ana watoto wanyonge, kikapigwa na kimbunga chenye moto, kikaungua?”.[2]

3. Amesema Mtume mtukufu (s.a.w.w):

«مَنْ أَسْدَى إِلَى‏ مُؤْمِنٍ مَعْرُوفاً ثُمَّ آذَاهُ بِالْكَلَامِ أَوْ مَنَّ عَلَيْهِ فَقَدْ أَبْطَلَ اللَّهُ صَدَقَتَه‏».

"Yeyote atakaye mpa Muumini kitu kisha akamsimbulia na kumuudhi, Mwenyezi Mungu mtukufu ataibatilisha sadaka yake”.[3]

4. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema:

« مَنِ اصْطَنَعَ إِلَى أَخِيهِ مَعْرُوفاً فَامْتَنَّ بِهِ أَحْبَطَ اللَّهُ عَمَلَهُ وَ ثَبَّتَ وِزْرَهُ وَ لَمْ يَشْكُرْ لَهُ سَعْيَه‏».

"Yeyote ampaye nduguye Muumini kitu na kisha akamsimbulia Mwenyezi Mungu atabatilisha amali zake na mzigo wa madhambi yake atauthibitisha juu yake na jitihada zake hatozifanya kuwa ni mwenye kuzishukuru”.[4]

5. Mtume mtukufu amesema:

«إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَ تَعَالَى كَرِهَ لِي سِتَّ خِصَالٍ وَ كَرِهْتُهُنَّ لِلْأَوْصِيَاءِ مِنْ وُلْدِي وَ أَتْبَاعِهِمْ مِنْ بَعْدِي الْعَبَثَ فِي الصَّلَاةِ وَ الرَّفَثَ فِي الصَّوْمِ وَ الْمَنَّ بَعْدَ الصَّدَقَةِ وَ إِتْيَانَ الْمَسَاجِدِ جُنُباً وَ التَّطَلُّعَ فِي الدُّورِ وَ الضَّحِكَ بَيْنَ الْقُبُور».

"Hakika Mwenyezi Mungu tabaraka wa taala amenikirihishia mambo sita, na nimeyachukia kwa mawasii wangu katika wanangu na wafuasi wao wa baada yangu: Mchezo katika Sala, na kufanya tendo la ndoa katika hali ya funga, na masimbulizi baada ya sadaka, na kuingia msikitini katika hali ya janaba, na kutazama kwenye manyumba ya watu, na kucheka makaburini”.[5]

6. Amesema Imam Sadiq (a.s):

«لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ الْعَاقُّ لِوَالِدَيْهِ وَ الْمُدْمِنُ الْخَمْرِ وَ الْمَنَّانُ بِالْفَعَالِ لِلْخَيْرِ إِذَا عَمِلَه‏».

"Hatoingia peponi yeyote mwenye kuwadharau wazazi wawili, mlevi wa kuduku katika pombe, na yule ambaye atendaye jambo jema lakini akawasimbulia watu kwa kuwatendea wema”.[6]

7. Amesema Imam Sadiq (a.s):

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تَكُونَ الصَّلَاةُ مَنّاً وَ الْأَمَانَةُ مَغْنَماً وَ الزَّكَاةُ مَغْرَماً الْخَبَر».

"Hakitasimama kiama mpaka Sala iwe ni yenye kusimbuliwa, na amana ikawa ni ngawira, na zaka ikawa ni gharama na madhara pia”.[7]

8. Amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w):

«ثَلَاثَةٌ لا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ‏ الْمَنَّانُ الَّذِي لَا يُعْطِي شَيْئاً إِلَّا بِمِنَّةٍ وَ الْمُسْبِلُ إِزَارَهُ‏ وَ الْمُنَفِّقُ سِلْعَتَهُ بِالْحَلْفِ‏ الْفَاجِر».

"Watu aina tatu Mwenyezi Mungu hatozungumza nao: Msimbuliaji ambaye hatoi kitu kwa watu wengine ila kwa masimango yake, na mvua nguo njiani, na muuzaji ambaye huapa viapo vya urongo kwa biashara yake ili inunulike kwa bei kubwa”.[8]

9. Mtume (s.a.w.w) amesema:

«یا علی: کره الله عز وجل لأمتي العبث في الصلاة والمن في الصدقة».

"Ewe Ali: Haridhiki na mambo haya kwa umma wangu: Kucheza katika Sala, na kusimanga katika Sadaka”.[9][1] Surat al Baqara/ 246.

[2] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 96, uk 143, Riwaya 8.

[3] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 93, uk 142.

[4] Rejea ile ile, uk 141.

[5] Rejea ile ile, uk 140.

[6] Rejea ile ile, uk 141.

[7] Rejea ile ile, uk 28.

[8] Rejea ile ile.

[9] Rejea: Jaami’ ahaadith ash-shiah, juz 8, uk 422.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: