bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:27:30
“Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayotenda”.
News ID: 262


SHARTI LA SABA: Utoaji na sadaka lazima viwe kama mapacha ikiambatana na ikhlaas nia safi, na hivyo visichanganyike pamoja na Riyaa (kwa maana ya: kujionyesha).

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

«وَمَثَلُ الَّذِينَ ينْفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَينِ فَإِنْ لَمْ يصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ».

"Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayotenda”.[1]

Na vile vile imekuja ndani ya Qur’an:

«وَالَّذِينَ ينْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيوْمِ الْآخِرِ وَمَنْ يكُنِ الشَّيطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا».

"Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shetani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno”.[2]

SHARTI LA NANE: Ni kwamba kamwe mtoaji asidhanie kuwa yeye ndiye mmiliki wa kweli, bali yeye ni njia baina ya Mola wake kwa waja wa Mola wake, na vile vile avidharau hata kama vikiwa vikubwa.

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu ndani ya kitabu chake:

«وَأَنْفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُمْ مُسْتَخْلَفِينَ فِيهِ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَأَنْفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ».

"na toeni katika alivyo kufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake. Basi walio amini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa”.[3]

Ndani ya Aya hii tukufu imesisitizia moja ya athari muhimu ya imani kwamba ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambapo kujitolea ni katika mambo ambayo amepewa mwanadamu, isipokuwa tu kwamba usisitizwaji umeambatana na nukta hii kwamba asisahau ya kuwa: "Kiukweli mmiliki wa asili ni Mwenyezi Mungu mtukufu” na mali pamoja na akiba hizi ziko kwake kwa muda mfupi kwa anuani ya amana, kama vile ambavyo wamepewa waliokuwa kabla yake.

Hakika ya kweli humpa mwanadamu roho ya ukarimu na kujitolea, na kufungua mkono wake na moyo wake katika kutoa.

Na vile vile katika Aya nyingine anasema kwamba:

« قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيرٌ لِمَنِ اتَّقَى».

"Sema: Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kumchamungu”.[4]

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema:

«ولا تستکثروا شیئا من الخیر وإن کثُر فبأعینکم».

"Msihesabu kitu kwa ukubwa zaidi ya heri na hata kama ikiwa machoni mwenu ni kingi”.[5]

Na lazima tufahamu ya kwamba kile ambacho Mwenyezi Mungu atamlipa mwanadamu badala ya sadaka ni kikubwa mno.

SHARTI LA TISA: Utoaji na sadaka ziwe katika mali ambazo azipendazo mtu, na kuzithamini.

Kwa sababu ndani ya Qur’an tukufu imekuja kwamba:

«لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ».

"KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda”.

SHARTI LA KUMI: Toa katika mali ambayo inapendwa na kuhitajika kwa Mtu.

Katika Qur’an tukufu imekuja:

«وَيؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ».

"bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa”.

Na vile vile katika sehemu nyingine imekuja:

«وَيطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَى حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيتِيمًا وَأَسِيرًا».

"Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa”.

SADAKA BORA

1. Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

«خَيْرُ مَالِ الْمَرْءِ وَ ذَخَائِرِهِ الصَّدَقَة».

"Mali bora na akiba bora ya Mwanadamu ni sadaka”.[6]

2. Amesema tena (s.a.w.w):

«تَصَدَّقُوا عَلَى أَخِيكُمْ بِعِلْمٍ يُرْشِدُهُ وَ رَأْيٍ يُسَدِّدُه‏».

"Toeni sadaka kwa ndugu zeu katika imani kwa kuwafundisha elimu yenye manufaa itakayomuongoza na nadharia itakayomfanya imara”.[7]

3. Nabii mtukufu (s.a.w.w) amesema:

«وَ مِنَ الصَّدَقَةِ أَنْ يَتَعَلَّمَ الرَّجُلُ الْعِلْمَ وَ يُعَلِّمَهُ النَّاس‏». «زَكَاةُ الْعِلْمِ تَعْلِيمُهُ مَنْ لَا يَعْلَمُه‏».

"Na katika sadaka Mtu kujifunza elimu sahihi, na kuifundisha watu”. "Zaka ya elimu ni kuifundisha kwa asiyeijua”.[8]

4. Imam Sadiq (a.s) amesema:

«يُسْتَحَبُ‏ لِلْمَرِيضِ‏ أَنْ يُعْطِيَ السَّائِلَ بِيَدِهِ وَ يَأْمُرَ السَّائِلَ أَنْ يَدْعُوَ لَه‏».

"Ni mustahabu kwa mgonjwa kutoa sadaka kwa mkono wake mwenyewe, na kumtaka muombaji amuombee dua”.[9]

5. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) amesema:

«أَمْسِكْ لِسَانَكَ فَإِنَّهَا صَدَقَةٌ تَصَدَّقُ بِهَا عَلَى نَفْسِك‏».

"Miliki ulimi wako kwa hiyo ni sadaka uitoayo kwa ajili yako mwenyewe”.[10]

6. Imam Sadiq (a.s) amesema:

«إِسْمَاعُ‏ الْأَصَمِ‏ مِنْ غَيْرِ تَضَجُّرٍ صَدَقَةٌ هَنِيئَة».

"Kumuelewesha kiziwi kwa sharti la kutokereka ni sadaka yenye thamani kubwa”.[11]

7. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema:

« أَفْضَلَ الصَّدَقَةِ صَدَقَةُ اللِّسَانِ‏ تُحْقَنُ بِهِ الدِّمَاءَ وَ تُدْفَعُ بِهِ الْكَرِيهَةُ وَ تَجُرُّ الْمَنْفَعَةَ إِلَى أَخِيكَ الْمُسْلِم‏».

"hakika sadaka bora ni sadaka ya ulimi ambao kwa kauli zake huzuia kumwagika damu, na kumaliza matatizo na masaibu, na kuleta faida na manufaa kwa ndugu zako Waislamu”.[12]

Mwisho[1] Surat al baqara/ 265.

[2] Surat an- Nisaa/ 38.

[3] Surat al- hadid/ 7.

[4] Surat an- Nisaa/ 77.

[5] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 71, uk 181, Riwaya 37.

[6] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 93, uk 122.

[7] Rejea ile ile, uk 135.

[8] Rejea ile ile, uk 136.

[9] Rejea: Mahajjat al- Baydhaau, juz 2, uk 19.

[10] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 68, uk 298.

[11] Rejea ile ile, juz 71, uk 388.

[12] Rejea: Jami’ ahaadith ash- shiah, juz 1, uk 269.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: