bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:40:10
"Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?”.
News ID: 263


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

DALILI YA KWANZA: UKARIBU WA KAMARI KWA POMBE NA KUABUDU MASANAMU NA KUPIGA RAMLI:

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

«إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ».

"Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?”.

Katika Aya hii tukufu Mwenyezi Mungu ameweka sambamba ulevi kwa kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, na vitu hivi hakuna shaka katika uharamu wake, na hiyo ilikuwa ni dalili juu ya uharamu wa pombe.

Na pombe ni kitu ambacho kipo wazi, na kile akinywacho Mtu na kulewa na kupoteza akili yake ima kiujumla au nusu, na anazungumza na kufanya mambo pasina kufikiria na bila akili, yawezekana kuzini, na anaweza kuua au kuchoma moto na kufanya lolote mfano wa hayo. Na kwa sababu hii imekuja sheria ya kuiharamisha.

Ama kuabudu masanamu ni jambo ambalo limeharamishwa tokea awali, kwa sababu ni njia ya kuviabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Na kitu ambacho kimewekwa sambamba kwa kuabudu masanamu na kingine kwa pombe, na kingine kwa kupiga ramli, hakika hakuna shaka katika uharamu wake na ukali wa madhambi yake.

DALILI YA PILI: KUITWA POMBE KWA JINA LA UCHAFU:

Rijs (uchafu) ni najisi, ama neno (الرجس) ni kila chenye madhara ndani yake na kile chenye dhambi ndani yake, na ameyaita Mwenyezi Mungu masanamu kwa jina la Uchafu katika kauli yake:

«فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ».

"Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu”.

Imeandikwa na Sheikh Juma Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: