bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      22:10:31
Na tunawaambia ya kwamba: Ilikuwa ni jambo la kupewa kipaumbele kwa wakati wenu huu muupotezao na kusahau kumdhukuru Mwenyezi Mungu, tambueni kuwa munao wajibu wa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na ktafakari, na tambueni ya kwamba munavyo vitu vingi, vinaweza kukushughulisheni katika mambo yenye manufaa, na michezo hiyo isiyo na faida ndani yake si kidini wa kidunia, hakika inakushughulisheni na hatimae kumsahau Mwenyezi Mungu na kumuomba na kumuabudu pia, na hatimae kukuleteeni kughafilika na ugumu wa moyo.
News ID: 268


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

DALILI YA NANE: HAKIKA KAMARI HUZUIA NJIA ZA MJA KUMDHUKURU MOLA WAKE

Na kuzuia kumdhukuru Mwenyezi Mungu mtukufu ni dalili nyingine juu ya kuharamishwa pombe na kamari, na hiyo ni kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t). na michezo hii ya kisheitani ndani yake yamo maovu makubwa nayo ni kuzuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na yote haya hushuhudiwa kwani watu wake ni wale ambao hupingiana hubeti hata ikiwa si kwa kutoa kitu mbadala lazima washughulishwe navyo kwa muda mrefu na kustareheka kwa michezo hiyo, na wakidhania ya kwamba wao hujitajirisha na kujiinua kiuchumi, na hapo hupitwa na muda ambao kwao ni kitu chenye thamani katika mchezo huu, na hilo huwapumbaza kumbumbuka Mwenyezi Mungu na kuzama katika upuuzi na hawaa na hatimaye kumsahau Mola wao: "Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau”.

Na tunawaambia ya kwamba: Ilikuwa ni jambo la kupewa kipaumbele kwa wakati wenu huu muupotezao na kusahau kumdhukuru Mwenyezi Mungu, tambueni kuwa munao wajibu wa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na ktafakari, na tambueni ya kwamba munavyo vitu vingi, vinaweza kukushughulisheni katika mambo yenye manufaa, na michezo hiyo isiyo na faida ndani yake si kidini wa kidunia, hakika inakushughulisheni na hatimae kumsahau Mwenyezi Mungu na kumuomba na kumuabudu pia, na hatimae kukuleteeni kughafilika na ugumu wa moyo.

DALILI YA TISA: HAKIKA KAMARI HUSHUGHULISHA KUACHA SALA

Na kupumbazika kuacha Sala ni kitu kinaonekana kwa wengi, wale wacheazao michezo hii ya kisheitani na kushughulika nayo hupoteza muda wao mwingi, kwani hupoteza Sala, na wanashughulishwa na mengi mbali na ibada, na uwajiapo muda wa ibada pasi hujisahaulisha na kushawishika, na wengi wanaokesha usiku mzima wanalala na kuacha Sala ya Asubuhi au kupitwa na baadhi ya Sala, au kupitwa na jamaa!! Je! Yote haya si dalili zionyeshayo kuwa ni haramu?!

DALILI YA KUMI: AMRI YA KUACHA KAMARI.

Amesema (s.w.t): "Basi je, mmeacha?” na hii ni dalili ya dhahiri/ wazi juu ya kuharamisha kamari, na amekwishatuamrisha Mwenyezi Mungu mtukufu kukoma, na kukoma hapa ni kwa maana ya kuacha na kutubia, na kwa sababu hii iliposhuka Aya hii wamesema Masahaba: Tumekoma… tumekoma. Yaani tumeacha kunywa pombe na kucheza kamari na mengineyo, na kauli yake (s.w.t): "Basi je, mmeacha?” hii si kwa maana ya suali kama ilivyodhahiri ya alama ya swali, bali ni kwa ajili ya kuomba, kwa maana acheni, vile vile kwa maana kwamba hadi lini musiache?! Hadi lini mutaendelea katika mchezo huu?! Je! Haujafikia wakati wa nyinyi kuacha?!

Je! Mmekwisha tambua madhara yake? Je! Hamkomi?

Wakasema: Ndio, tumekoma.

Hakika hizi ni dalili kumi kutoka katika Aya tukufu juu ya kuharamisha kamari. Na Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake ni wajuzi zaidi.

Mwisho

Na Sheikh Juma Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: