bayyinaat

Published time: 21 ,March ,2018      22:33:44
Kwa hakika mwenye kufunga siku moja katika mwezi wa Rajab kwa imani na matarajio basi radhi za Mwenyezi Mungu huwa ni lazima kwake, na kwa funga yake hiyo atakuwa amezima ghadhabu za Mwenyezi Mungu katika siku ile, pia hufunga mlango baina ya milango ya moto.
News ID: 277

Katika mwezi huu kuna matendo ya aina mbili, kwanza kuna matendo ambayo huhesabika ni matendo ya ujumla, kwa maana ya kwamba katika mwezi huu hayana siku maalumu ya kuyatenda, bali kila siku au kila wakati unaweza kuyatenda kwa lengo tu la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.

1. Funga (swaum)

Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saww):

ألا فمن صام من رجب يوماً إيماناً واحتساباً استوجب رضوان الله الأكبر، واطفأ صومه في ذلك اليوم غضب الله، وأغلق عنه باباً من أبواب النار، ولوَ أُعطى ملءَ الأرض ذهباً ما كان بأفضل من صومه، ولا يستكمل أجرَه بشئ من الدنيا دون الحسنات إذا أخلصه لله

"…Kwa hakika mwenye kufunga siku moja katika mwezi wa Rajab kwa imani na matarajio basi radhi za Mwenyezi Mungu huwa ni lazima kwake, na kwa funga yake hiyo atakuwa amezima ghadhabu za Mwenyezi Mungu katika siku ile, pia hufunga mlango baina ya milango ya moto. Hata kama ikitokea akipewa dhahabu ujazo wa ardhi nzima haitafikia fadhila za funga yake hiyo, na kama ataifunga kwa nia safi ya Mwenyezi Mungu basi hakutakuwa na jambo la kukamilisha malipo yake hapa duniani tofauti na mema”

2. Mbadala wa Funga

Kuna wakati inaweza kutokea kwamba funga ikawa nzito kwa namna moja au nyingine, hii haina maana kwamba mtu huyu hana nafasi ya kuchuma katika mwezi mtukufu wa Rajab, la hasha, na ndio maana kuna matendo mbadala kwa mja wa aina hii.

Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saww) mahimizo sana kunako kufunga katika mwezi huu, lakini alipoulizwa juu ya mwenye kushindwa kufungwa kutokana na udhaifu au sababu nyinginezo ni yapi anatakiwa kufanya? Alisema: atatoa sadaka hata kama ni kwa kitu kidogo. Kisha akasema:

والذي نفسي بيده أنه من تصدَّق بهذه الصدقة كل يوم، ينال ما وصفتُ وأكثر لأنه لوَاجتمع جميع الخلائق كلهم من أهل السماوات والأرض على أن يقدّروا ثوابه قدر ثوابه ما بلغوا عُشر ما يصيب في الجنان من الفضائل والدرجات" قيل: يا رسول الله فمن لم يقدر على الصدقة يصنع ماذا لينال ما وصفت؟.. قال: يُسبِّح الله في كل يوم من أيام رجب إلى تمام الشهر هذا التسبيح مائة مرة

"سبحان الإله الجليل سبحان من لا ينبغي التسبيح إلا له سبحان الأعز الأكرم

"…Naapa kwa ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake (Mwenyezi Mungu), kwa atakayetoa sadaka hata ndogo katika masiku ya mwezi wa Rajab, atayapata yote niliyoyaelezea (Thawabu za Funga) pamoja na zaidi ya hayo, kwa maana ya kwamba hata kama viumbe wote wa mbingu na ardhi watakutana kwa lengo la kukadiria malipo yake basi hawatofikia hata machache ya yale ambayo atayapata mja huyu katika fadhila na daraja za pepo. Kisha Mtume akaulizwa: Ewe Mtume wa Allah, ikiwa mtu atashindwa hata kutoa sadaka kwa kiwango kidogo afanye nini?. Mtume akajibu : amtukuze Mwenyezi Mungu kila siku mara mia moja kwa maneno yafuatayo

"..Ametakasika Mwenyezi Mungu mtukufu, ametakasika ambaye haipaswi kumtukuza mwingine pasi na yeye, ametakasika Mwenyezi Mungu mtukufu na mkarimu…..”.

Haya ni baadhi tu ya matendo ambayo waja wanaweza kushikamana nayo katika mwezi huu wa Rajab, lakini pamoja na hayo kuna matendo mengine kama vile:

· Swala za suna

· Dua za kila siku hasa dua ifuatayo:

"يا من أرجوه لكل خير، وآمن سخطه عند كل شر، يا من يعطي الكثير بالقليل، يا من يعطي من سأله، يا من يعطي من لم يسأله ومن لم يعرفه تحنناً منه ورحمة، أعطني بمسألتي إياك جميع خير الدنيا وجميع خير الاخرة، واصرف عني بمسألتي إياك جميع شر الدنيا وشر الآخرة، فإنه غير منقوص ما أعطيت، وزدني من فضلك يا كريم

"….Ewe ambaye namtarajia katika kila kitu, na nahofia chuki yake katika kila shari, ewe ambaye hulipa mengi kwa machache, ewe ambaye humpa mwenye kuomba, ewe ambaye humpa asiye muomba na hata asiye mtambua yeye, hii yote ni katika hali ya mapenzi na rehema zako, basi kwa maombi yangu haya naomba unipatie heri zote za dunia na akhera, na niepushia kw amaombi yangu haya shari zote za dunia na za akhera, kwani wewe hupungukiwa kwa kutoa kwako, na naomba uniongezee kwa fadhila zako ewe uliye mkarimu”.

Kisha kwa mujibu wa mapokezi ni kwamba baada ya kufika hapo Imamu Swadiq aliinua mkono wake wa kushoto na kushika ndevu zake huku akitikisa kidole cha shahada cha kulia kwenda kulia na kushoto na kusoma maneno haya:

يا ذا الجلال والإكرام يا ذا النعماء والجود، ياذاالمن والطَّوْل، حرم شيبتي على النار

"..Ewe mwingi wa utukufu na ukarimu, ewe mwingi wa neema na utoaji, ewe mwingi wa kusamehe na kutoa, weka mbali na moto ndevu zangu (mapambo yangu ya mwili).

Katika baadhi ya riwaya imepokelewa kwamba Imamu alikuwa hashushi kiganja chake ila kitakuwa kimejaa machozi.

· Kuzidisha sana kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu pamoja na kumtukuza.

Na kila ambalo ni jema na linafaa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu basi katika mwezi huu ni mahala pake, kama tulivyotanguliza kwamba mema katika mwezi huu yanaongezwa maradufu na Mwenyezi Mungu, hivyo ni fursa munasibu sana kwa waja wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu.

Imeandikwa na Sh Abdul Razaq Bilal (Abuu Asghar).


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: