bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      10:42:16
Liwaat; ni kitendo cha kijinsia baina ya jinsia mbili za kiume kiasi kwamba inakuwa ni mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzie katika tupu yake ya nyuma, ambapo kwa mujibu wa Dini tukufu ya Kiislam pamoja na Dini nyinginezo za Kimungu ........
News ID: 317

DHAMBI YA KULAWITI

Tafadhali soma makala hii kamili, kwa sababu ikiwa kama katika maisha yako umekwisha tenda dhambi yoyote ile basi jitahidi kuepuka kitendi hiki kichafu. Na ikiwa mtu atatenda kitendo hiki (Mungu apishie mbali) basi mlango wa toba daima uko wake kwa Mtu huyo, hivyo ni lazima atubie dhambi hii kubwa na chafu.

Liwaat; ni kitendo cha kijinsia baina ya jinsia mbili za kiume kiasi kwamba inakuwa ni mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzie katika tupu yake ya nyuma, ambapo kwa mujibu wa Dini tukufu ya Kiislam pamoja na Dini nyinginezo za Kimungu zimeharamisha vikali kitendo hicho. Vile vile huhesabika kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa. Na yeyote atakayetenda kitendo hicho basi atakuwa ametenda kitendo cha kuchukiza mno na kiovu, pia atalaaniwa na Mwenyezi Mungu, Mtume wake pamoja na Malaika wake, na ikiwa atakayetenda uchafu huo ni Mtu aliyekwisha balehe au ni mtu mwenye akili timamu na kisha akafariki Dunia bila kutubia dhambi hiyo, basi ataadhibiwa vikali siku ya Kiama.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) amesema: "Pindi atakapofariki Dunia Mtenda kitendo hicho basi hatokaa siku tatu ndani ya kaburi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtupa katika kundi la watu Nabii Luut waliongamizwa, vile vile atafufuliwa siku ya Kiama miongoni mwa watu madhalimu walioghadhibikiwa na Mola wao”. Rejea: Miizanul hikmah, juzuu 11, uk 5369. Ikiwa wote wawili au mmoja katika ya waliotenda kitendo hicho atakitende mbele ya Hakimu wa kisheria au atakiri mbele yake, au ushuhuda wa shahidi utathibitika, basi ni lazima Hakimu huyo atoe adhabu dhidi ya mtu huyo. Adhabu miongoni mwa adhabu hizi zifuatazo:

1. Auliwe kwa upanga na mfano wa panga.

2. Achomwe moto.

3. Afungwe mikono na miguu na kisha aangushwe kutoka kwenye kilele cha mlima hadi chini.

4. Apigwe mawe hadi kifo.

5. Kumwangushia ukuta kwa juu.

(Ndio. Kila aina ya adhabu ambayo Hakimu atakayoona ndio inayofaa basi aitekeleze na hii ni pindi pale itakapothibitika ya kwamba kitendo hicho kimetokea kweli. Lakini ikiwa kwamba tendo la kuingiliana la watu hao halikuthibitika, basi wapigwe bakora mia moja. Lakini ikiwa kabla ya shahidi kutoa ushuhuda Mtendani wa uchafu huo akatubia dhambi hiyo, basi hatoadhibiwa. Vile vile ikiwa mtenda na mtendewa hawatokuwa wamefikia umri wa Balehe nao pia hawatoadhibiwa, isipokuwa iwapo itathibitika mbele ya Hakimu wa kisheria ni jukumu lake kuwaadabisha. Kwa sababu wale wasio balehe hata katika kitabu cha amali zao haitaandikwa dhambi hiyo.

Na yeyote atakayetenda tendo hilo (Mungu apishie mbali) na Kijana, ikiwa itabainika ya kwamba wakati wa kitendo cha Liwaat hata kiasi kidogo cha tupu ya Mtendaji kitaingia kwenye tupu ya mtendewa, basi Dada na Binti pamoja na Mama wa Mtendewa watakuwa ni haramu kwa Mtenda uchafu huo kuwaoa kwa mujibu wa Hukumu wa Dini ya Kiislam, Lakini Dada na Mama wa Mtenda liwaat hawatokuwa haramu kuolewa na Mtendewa.

Lakini iwapo watakuwa wamelawitiana (Yaani kila mmoja amemlawiti mwenzie) basi kila mmoja miongoni mwao atakuwa ni haramu kuoa Msichana kutoka katika familia ya mwingine. Isipokuwa pale kitendo hicho hakikufanyika kwa sura ya kitendo bali kwa sura ya mikwaruzokwaruzo au ikapatikana shaka ya kutokea kitendo hicho kichafu, basi kutokana na hukumu ya kisheria ya Kiislam familia iliyotajwa hapo juu itakuwa ni halali kwa kila mmoja bila pingamizi). Rejea: Tahrirul Wasilah, juzuu 4, uk 198-199.

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: