bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      12:07:40
News ID: 329

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Anasema Mwenyezi Mungu katika surat al- Niass;

"وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ".

"Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu”.[1]

Muwe wenye tahadhari kwa Mwenyezi Mungu na kile mukiapiacho kuwa mutatenda kadha wa kadha, na wala musikhalifu maamrisho yake, na ambatano katika Aya hii ni; jamaa wa karibu ambalo limekuja baada ya jina tukufu la Mwenyezi Mungu mtukufu, na imepokelewa kwa Imam Baqir (a.s) maana hii ambayo kwamba imenukuliwa maana yake katika majmau’ al- bayaan, na imenukuliwa katika Al- kaafiy kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) katika maana hii ya Aya tukufu: ambapo ni kwa maana ya: Jamaa wa karibu, kwani Mwenyezi Mungu ameamrisha kuunga undugu pamoja nao na akautukuza undugu huo, tambua kuwa Mwenyezi Mungu ameifanya amali hii kuwa ni katika mambo ayapendayo”.[2]

SALA NA ZAKA – UCHAMUNGU NA KUUNGA UNDUGU:

Kutoka kwa Imam Ridhaa (a.s): "Hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha mambo matatu yakiambatana na mengine matatu, ameamrisha Sala na Zaka, hivyo yeyote anayesali na asitoe Zaka haitokubalika Sala yake, na ameamrisha kumshukuru yeye na wazazi wake wawili, hivyo yeyote asiyewashukuru wazazi wake basi hajamshukuru Mwenyezi Mungu, na meamrisha kumcha Mungu na kuunga undugu, na yeyoye asiyeunga undugu na jamaa zake hajamcha Mungu kikamilifu”.

KUMPA JAMAA WA KARIBU – NI URAHISI WA HISABU

Anasema Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika surat Al- Nahl:

" إِنَّ اللَّهَ يأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَى ".

"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa”.[3]

Na anasema katika Surat al- Ra’d:

" وَالَّذِينَ يصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يوصَلَ وَيخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيخَافُونَ سُوءَ الْحِسَابِ ".

"Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya”.[4] Hadi alipo toa ahadi kwao katika mwisho wa aya tukufu kwa njema hatima na pepo ya milele.

Hufahamika katika jumla hii: (na wanaikhofu hisabu mbaya) kwamba kuunga undugu ni sababu ya urahisi wa hesabu kama ilivyonukuliwa kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Imam Sadiq (a.s) aliposema (a.s.): "Kuunga undugu hurahisisha hesabu ya siku ya kiama ambayo ni fimbo ya awali katika umri wa maisha ya mwanadamu na katika pambano baya”.

KUUNGA UNDUGU KATIKA RIWAYA:

Ziko riwaya tele kuhusu suala la wajibu wa kuunga undugu na miongoni mwake ni hadithi ya Imam Baqir (a.s) aliposema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

" أُوصِي الشَّاهِدَ مِنْ أُمَّتِي وَ الْغَائِبَ مِنْهُمْ وَ مَنْ فِي أَصْلَابِ الرِّجَالِ وَ أَرْحَامِ النِّسَاءِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَنْ يَصِلَ الرَّحِمَ وَ إِنْ كَانَتْ مِنْهُ عَلَى مَسِيرَةِ سَنَةٍ فَإِنَّ ذَلِكَ مِنَ الدِّين‏".

"Ninamuusia aliye shahidi katika umma wangu na aliyeghaibu miongoni mwao na wale waliokuwa katika migogo ya wananume na matumbo ya wanawake hadi siku ya ikuma kuunga undugu hata ikiwa ni kwa umbali wa njia ya miaka elfu moja, kwani hiyo ndio dini”.[5]

HATOVUKA SIRAAT

Kutoka kwa Baqir (a.s) amesema Abuu Dhar kuwa nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema:

" حَافَتَا الصِّرَاطِ- يَوْمَ الْقِيَامَةِ الرَّحِمُ وَ الْأَمَانَةُ فَإِذَا مَرَّ الْوَصُولُ لِلرَّحِمِ الْمُؤَدِّي لِلْأَمَانَةِ نَفَذَ إِلَى الْجَنَّةِ وَ إِذَا مَرَّ الْخَائِنُ لِلْأَمَانَةِ الْقَطُوعُ لِلرَّحِمِ لَمْ يَنْفَعْهُ مَعَهُمَا عَمَلٌ وَ تَكَفَّأَ بِهِ‏ الصِّرَاطُ فِي النَّار".

"Vitatangulia (Nuru ya Undugu na amana) atakapopita muunga undugu na mtekeleza amana vitamfikisha peponi, na atakapopita msaliti wa amana mvunjaji undugu hazitamfaa amali na inampana siraat hadi kuangukia motoni”.[6]

ATHARI ZA KIDUNIA KWA MUUNGA UNDUGU:

Zipo riwaya nyingi ambazo huzungumzia kuhusu athari za kuunga undugu na uzidishiwaji wa umri na kuchelewa kifo chake na kuzuiliwa balaa na ongezeko la riziki na kuepuka ufukara na wingi wa kizazi/ ukoo.

Imenukuliwa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) hadithi tatu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuhusu kuunga undugu ni hilo lilijiri katika kikao cha pamoja na khalifa wa baniy Abbas al- Dawaniqiy:

1. Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.aw.w.):

" إِنَّ الرَّجُل‏ يَكُونُ أَجَلُهُ ثَلَاثَ سِنِينَ فَيَكُونُ وَصُولًا لِلرَّحِمِ فَيَزِيدُ اللَّهُ فِي عُمُرِهِ ثَلَاثِينَ سَنَةً فَيَجْعَلُهَا ثَلَاثاً وَ ثَلَاثِينَ سَنَةً وَ يَكُونُ أَجَلُهُ ثَلَاثاً وَ ثَلَاثِينَ سَنَةً فَيَكُونُ قَاطِعاً لِلرَّحِمِ فَيَنْقُصُهُ اللَّهُ ثَلَاثِينَ سَنَةً وَ يَجْعَلُ أَجَلَهُ إِلَى ثَلَاثِ سِنِينَ".

"Hakika Mtu aungaye undugu na jamaa zake wa karibu na imekwisha baki katika umri wake miaka mitatu, hakika Mwenyezi Mungu huibadilisha kuwa miaka thalathini, na auvunjaye na ikawa imebaki katika umri wake miaka thalathini Mwenyezi Mungu hubadilisha kuwa miaka mitatu, kisha akasema tena (s.a.w.w); Mwenyezi Mungu humfutia amtakaye na humthibitishia amtakaye”.[7]

2. Kuunga undugu huimarisha majumba na kuzidisha umri hata ikiwa watu wake ni katika jamii ya waja wema.[8]صِلَةُ الرَّحِمِ وَ حُسْنُ الْجِوَارِ يَعْمُرَانِ الدِّيَارَ وَ يَزِيدَانِ فِي الْأَعْمَارِ

3. Kuunga undugu hurahisisha hesabu ya siku ya kiama na huepusha kifo kibaya.[9] صِلَةُ الرَّحِمِ تُهَوِّنُ الْحِسَابَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

Na kwa hakika amesema Imam Sadiq (a.s) kumwambia Maysar:

"Hakika zimekwisha wadia siku za kufa kwako zaidi ya mara moja, na zote hizo anazichelewesha Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kuunga kwako undugu na jamaa wa katibu na wema wako kwa familia yako”.[10]

Itaendelea………[1] Al- Nisaa/ 1.

[2] Al- kaafiy juz 2, uk 150, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 1.

[3] Al- Nahl/ 90.

[4] Al- Ra’d/ 21.

[5] Al- Kaafiy: juz 2, uk 151, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 5.

[6] Al- Kaafiy: juz 2, uk 151, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 11.

[7] Al- Kaafiy: juz 2, uk 152, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 17.

[8] Al- Kaafiy: juz 2, uk 152, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 14.

[9] Al- Kaafiy: juz 2, uk 157, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 23.

[10] Al- Kaafiy: juz 2, uk 156, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 27.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: