bayyinaat

Published time: 21 ,September ,2018      16:05:11
Imepokelewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s), na Imam Sadiq (a.s) kuwa wamesema: “Hapana yeyote katika waja wa Mwenyezi Mungu ila amekosea kosa la zinaa kwani zinaa ya jicho ni kuangalia cha haramu na zinaa ya mdomo ni ..........
News ID: 335

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


MSHALE WA SHEITANI WENYE SUMU:

Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s): "Kumtazama mwanamke asiyejistiri ni mchale katika mishale ya Ibilisi yenye sumu kali, na uangaliaji ulioje! Wa kukithirisha uliopelekea kuleta masimanzi marefu”.

ZINAA YA VIUNGO VYA MWILI:

Imepokelewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s), na Imam Sadiq (a.s) kuwa wamesema: "Hapana yeyote katika waja wa Mwenyezi Mungu ila amekosea kosa la zinaa kwani zinaa ya jicho ni kuangalia cha haramu na zinaa ya mdomo ni kumbusu maharamu, na zinaa ya mikono ni kugusa asiyestahiki”.

Na imepokelea pia: "Yeyote atakayejaza macho yake mwanamke wa haramu, Mwenyezi Mungu atayapigilia misumari ya moto siku ya kiama, na yatachomeka hadi atakapoamrisha Mwenyezi Mungu kupelekwa motoni”.

IBILISI MWENZA NDANI YA MOTO:

Yeyote atakaye kusanya wanawake wawili ajinabi Mwenyezi Mungu atamkusanya pamoja na Ibilisi katika minyororo ya moto, na katika riwaya nyingine ni kwamba: Mwenye kumtazama mwanamke kisha akainua macho yake mbinguni au akafunga macho yake, hakika hatofungua macho yake ila Mwenyezi Mungu amemuandikia kuoa wanawake wa peponi na atamfuatishia ladha ya imani yake ambayo hajawahi kupata ladha ya imani hiyo.[1]

Na kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Hakika imeshitadi ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa mwanamke mwenye mume aliyejawa na tamaa ya wanaume katika macho yake, atakapofanya hayo Mwenyezi Mungu ataporomosha amali zake zote.

Hakika ziko riwaya tele ambazo zimekataza kuangalia maumbile ya nyuma ya mwanamke, hata akiwa ni mwenye kujistiri, kwani hili ni jambo makuruhu kisheria.

UHARAMU WA KUWA FARAGHA PAMOJA AJINABI:

Kwa hakika imeharamishwa kujiweka faragha pamoja na mwanamke ajinabi kwa uwezekano wa kutokea jambo la haramu, hata wakiwa wakijishughulisha na ibada.

Kutoka kwa mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asilale mahali atakayosikia pumzi ya mwanamke ambaye kwake ni halali”.[2]

Na kutoka kwa Abuu Abdillah (a.s) amesema: Hakuchukua bai’a Mtume (s.a.w.w) kutoka kwa wanawake ili tu wasikae pamoja na wanaume faragha.[3]

Na madhumuni ya faragh, ni sehemu ambayo hawezi yeyote kuingia, kama vile chumba kilichofungwa mlango wake, au nyumba isiyoingiliwa na yeyote.

HUDUDI KALI:

Hududi ambazo Uislamu umeziweka kwa ajili ya kitendo hiki kichafu ni mojawapo ya mambo ya wajibu ambayo huzuia kuenea kwa uchafu huu, na yumkini kutokomeza ikiwa yatazingatiwa matano haya:

Ikiwa mtu atazini na moja ya ndugu zake kinasaba, mfano: Dada, binti, shangazi, mama mdogo, binti ya kaka, binti ya Dada, hakika ni wajibu kuuliwa.

Ikiwa mtu atamuona mwanaume anazini na mkewe na akawa katika amani kutokana na madhara anaweza kuwachukulia hatua ya kifo wawili hao.

Ikiwa kafiri atazini na mwanamke wa Kiislamu, hakika atauliwa mara ya nne kama hatokoma.

Ikiwa mwanaume ni mwenye mke wa daima na akamuingilia akiwa amebaleghe na mwenye akili, na akaweza kumuingilia wakati wowote atakao kisha akazini na mwanamke aliyepevuka, ni wajibu apigwe mawe, na wako baadhi wasemao kwamba: Ni wajibu kupigwa bakora mia moja, kisha kupigwa mawe.

Ikiwa mzinifu wa kiume si mwenye mke na akazini na asiyekuwa halali kwake, basi hududi yake ni bakora mia moja, na vile vile mzinifu wa kike aliyekuwa hana mume. Na zimepokelewa hududi nyingi katika vitabu mbalimbali vya Kiislamu kwa lengo la kuzuia uchafu huu.

Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

"الزَّانِيةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيوْمِ الْآخِرِ وَلْيشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ. الزَّانِي لَا ينْكِحُ إِلَّا زَانِيةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيةُ لَا ينْكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ".

"Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini. Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini”.[4]

Itaendelea......[1] Wasaail al- shia, juz 14, uk 246, mlango; tahriim muqaddimaat al- zinaa, hadithi 2.

[2] Wasaail al- shia, juz 14, uk 141, mlango; tahriim al- nadhar ilaa al- nisaai, hadithi 16.

[3] Wasaail al- shia, juz 14, uk 134, mlango wa 99, hadithi 3 na 1.

[4] Al – Nuur/ 2 – 3.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: