bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:48:38
News ID: 338

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Wanawake wengi wanafanya jitihada za kubadili mienendo ya waume zao, na utawaona wanatumia mbinu nyingi na wanatafuta njia nyingi za kufikia kile wanataka kwa ajili ya kubadilisha baadhi ya mienendo wanayoichukia kwa waume zao. Je! Kubadilika tabia ya mume ni jambo linalowezekana, na ikiwa inawezekana ni jinsi gani litathibiti suala hilo?.

Watu wengi wanasema kuwa mabadiliko ya tabia ya mtu ni jambo gumu na si rahisi, na kulipigia mifano mingi, kama vile maneno ya msemaji: "Atakaye kulia juu ya kitu basi huzeekea juu yake”. Ukweli ni kwamba mabadiliko ya nafsi na maadili yanawezekana ikiwa vitaambatana na utashi wa kibinadamu, pia hilo lawezekana ikiwa Mtu atakuwa wa karibu, kama vile nafasi ya mke kwa mumewe ambapo ni mahali pa uaminifu katika uhusiano kati ya wanandoa wawili.

NJIA AMBAZO HUMSAIDIA MKE KUBADILI MWENENDO WA MUME WAKE

Ni kwamba mke asitafute njia hasi katika kumpinga mume itakapokuwa ya moja kwa moja, kwani upinzani wa moja kwa moja huwaudhi watu wengi hata kama itakuwa ni pamoja na maneno mazuri, na yampasa mke kutafuta njia ya upinzani iliyokuwa thabiti za ishara na mifano na mengineyo, na mfano wa hilo ni mke kuchukia tabia ya mume ambayo atahisi kupambika mume kwa sifa hiyo itapelekea kutomvutia, na kulalamikia mume kutomjali au kumsifia, katika hali hii ni hila ya Mke kumsimulia mumewe kisa na kuashiria shakhsiya ya Mtu anayemjali mkewe ambayo ni furaha ya mke iliyokuwa nzuri kwake, na huku akimhudumia na kumkirimu ndani ya nyumba zaidi ya hapo awali, hapo mume atahisi kusikiliza kisa hicho na kuitambua kasoro yake katika upande huu kwa mkewe, na hiyo inaweza kupelekea kubadilika tabia yake na kuanza upya kumjali mke.

Pia ni kwamba mke ajaribu kulinganisha njia ya mfano mbaya halisi na mfano mwingine mzuri, mpaka imbainikie mumewe mfano mzuri wa mwenendo mwema kwa familia yake, yumkini mwanamke kulalamikia suala la usafi kwa mumewe na kupuuzia utaratibu wa mambo yake binafsi, hivyo mwanamke kwa ajili ya kulibadilisha hili la kubadilisha tabia ya mumewe ni kuongozana naye kwenye hazina yake binafsi ili kujionea kwa macho yake na lengo ni kukusudia nyuma ya hilo mume kuguswa na faida za unadhifu na uratibu wa mambo yake na mavazi yake, hakika shani ya kufanya hivyo ni kumhamasisha mume ili kubadili mwenendo wa kupuuzia mambo yake ya usafi..

Pia ni jukumu la mke kutumia maneno ya upendo na laini wakati anapotaka kubadilisha tabia ya mumewe, na kumfanya mumewe ahisi thamani na heshima nyumbani kwake, na mume anavutiwa na maneno mazuri na maneno yanayompa thamani na kumpa heshima ya juu, na bila shaka hayo ni mazingira yenye rutuba ambayo mume atapokea kila kitu ambacho ataambiwa na kunasihiwa kwa ajili ya kujipangilia mwenyewe na kubadili mfumo wa maisha yake kuwa bora.

----------------------


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: