bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:50:01
News ID: 339

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Amesema Mwenyezi Mungu katika surat Rum:

«وَمِنْ آياتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيهَا وَجَعَلَ بَينَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآياتٍ لِقَوْمٍ يتَفَكَّرُونَ».

"Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri”.

Hakika silika ya mwanadamu aliyoumbiwa na Mwenyezi Mungu ni kutoishi peke yake, kwani daima anahitajia yule atakayeshirikiana nae katika nyakati za maisha yake na shughuli zake, kwa minajili hiyo Mwenyezi Mungu ameweka sheria ya ndoa ili kuhakikisha haja hii inapatikana kwa Mwanadamu, kwani Baba yetu Adam alipoumbwa na Mwenyezi Mungu alipea utulivu ndani ya pepo na akahitajia atakaye shirikiana naye maisha yake, ndipo Mwenyezi Mungu akamuumbia Hawa kwa ajili ya kumliwaza katika upweke wake.

Ndoa yenye furaha ni moja ya sababu za furaha na utulivu katika maisha kwa mwanadamu, na hivyo uwezo wa kutekeleza majukumu na kazi ambazo Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu alizomwajibishia kuzitekeleza, hivyo ni namna gani tunaweza kutengeneza uhusiano wa ndoa kuwa ni wenye furaha? Hili ndilo tutakalojaribu kuelezea katika makala haya.

NAMNA YA KUJENGA MAISHA YA NDOA YENYE FURAHA

Ili kuunda uhusiano wa ndoa wenye furaha, ni lazima tokea mwanzo wakati wa wanandoa kuchaguana, uchaguzi huo uwe kwa misingi ya upendo (mapenzi), kukubaliana na kuridhiana, na kusiwe na aina yoyote ile ya kulazimishwa au kukirihishwa.

Ni muhimu kuamini kwamba lengo la ndoa ni kufikia utulivu, upendo na huruma, kwani wanandoa wote wawili wanatafuta upendo na huruma katika ndoa zao, na ndoa haipaswi kutegemea maslahi au ili kukidhi mahitaji ya kimwili tu, bali iwe ni kanuni timilifu.

Utendaji kazi wa wanandoa wote ni kusimamia nyadhifa zao na kushikilia majukumu yao yanayowakabili, kwani Dini ya Kiislamu inampa mwanamume jukumu la muhimu la kuitumikia familia, ikiwa ni pamoja na mke, na kumfanya awe wajibu mbele yao mbele ya Mungu Siku ya Ufufuo. Kama ambavyo alivyompa mwanamke wadhifa wa kuwalea watoto malezi mazuri.

Kufanyia kazi chanzo cha uadilifu kati yao, ambapo ni muhimu kujiepusha kuendeleza uhasama na maneno mabaya (yaani unyanyasaji wa maneno), wala mmoja asimtwike mwingine jambo asiloweza kumudu, wala asisumbue maisha ya ndoa kwa kumlinganisha mume wa ndoa na wanaume wengine, kwani kila jambo la namna hiyo lina kero na aibu.

Kutokuza mambo na kutafuta udhuru kwa upande mwingine, na kutosimamia makosa ya kila mmoja wao, bali hata kinyume lazima kushinda matatizo na kujaribu kuyatatua kwa njia ya ustaarabu na mbali na unyanyasaji.

Ni wajibu wa mke kuhifadhi mali za mumewe, nyumba yake na watoto wake asipokuwepo, kama ambavyo anapaswa kuendelea kujitahidi mwenyewe kujichunga na kulinda wake uzuri, na kuwa na uvumilivu na hali ya umbali wa mumewe, mbali na malalamiko mengi, na amtii mumewe katika mambo yote isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amekataza. Daima awe ni mwenye bashasha na furaha pindi (Mume) anapomtazama, kwani mambo haya yote hufanya kumpenda na kushikamana naye, na kifuatacho kufikia furaha ya ndoa.

Hivyo mume unapaswa kuepuka kuamsha mada ambayo inaweza kusababisha hisia mbaya na dhiki kwa mke wako, na kutokataa mapendekezo yake yote bila majadiliano, jambo hili linapoteza maana yake ya thamani yake kwako, kama ambavyo unapaswa kuwa mwenye busara wakati unapoomba kitu fulani na kuacha kujikweza kwa kiburi na kumtenza nguvu mwenza wako (yaani mfumo dume), simamia kushauriana naye katika masuala yanayokuhusu wewe, hata kama rahisi, basi kufanya hivyo utapunguza umbali uliokuwa kati yenu, na samehe makosa yake na usijaribu kukuza mambo, na kadri unapokuwa unazingatia hali zake mbalimbali za kisaikolojia hakika hujisikia furaha, na mambo haya yote humfanya mke wako akupende na kuambatana na wewe daima.

----------------------


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: