bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:54:33
News ID: 343

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Wanawake wengi hutahayari na kuuliza ni njia ipi nzuri kwa ajili ya mazuri ya mpenzi mwenye hasira na harasa, baadhi yao hujaribu kutafuta suluhu kwa wenza wao na kuyafanya mambo kuwa mabaya zaidi, na baadhi yao huzuiliwa kwa kiburi chao na ukubwa wao kuliendea hilo, hatimaye huandamwa na ukame na kupoteza uhusiano kufuatana na athari ya mambo hayo, na huenda ikawa sababu ni ghadhabu za hapa na pale kwa mwenza, na huenda ikawa si sababu hata moja, lakini natija ikawa moja kwamba ghadhabu huu itazidisha chuki na mtengano kati ya pande mbili, jambo ambalo huelekea mwisho wa kuachana kwao, na ghadhabu kwa daraja yoyote iwavyo na sababu zake na ukali wake pamoja na haki zake, hakika upo ushauri na nasaha zenye kumnufaisha kila msichana kwa kutafuta njia bora ya suluhu kwa mwenza wake king’ang’anizi na mwenye ghadhabu za hapa na pale.

1. Kuwa wa kwanza kutabasamu, wala usimfanye kuwa wa kwanza kutabasamu.

2. Msikilizeni, mjadiliane kwa upole na ustaarabu, bila kuinua sauti zaidi ya kiwango cha sauti yako.

3. Angalia nukta chanya yenye neno (Ndiyo) ya maongezi yake, na jaribu kuzuia kwa kadri iwezekanavyo kwa kila jibu ambalo ulitarajialo ndani yake neno ambalo halina majibu yake.

4. Endelea kuwa mg’avu kwake na mwenye kuonyesha upendo na mapenzi machoni mwake pindi uwapo naye, kila mwanaume kwa ibara hii ni mtoto mkubwa, kwani ukaidi hausaidii kuwa pamoja naye, lakini kwa urafiki na upoke utamfanya atulie na kurudi kwenye furaha yake na ridhaa yake.

5. Mkumbushe kwa njia isiyo mubashara kwa wakati wenu mzuri mkiwa pamoja, na kamwe usipite njia yenye vituo hasi katika mahusiano yenu.

6. Fanya upya mwelekeo wa maneno mazuri kwake kwa kuonyesha hisia chanya za kweli.

7. Kumbuka mambo ambayo uliyomchekesha zamani na yakariri tena mbele yake.

8. 9Msiwe makini na kila kitu anachosema akiwa mwenye hasira, na utambuae kwamba ikiwa utaendelea kunyamaza na kuwa na uvumilivu, atajutia mwenyewe na kuomba msamaha kwako kwa maneno yote yaliyokukwaza na asiyokusudia kuyasema kwako akiwa ni mwenye hasira.

9. Mwambie kuwa unamheshimu na unaheshimu hasira yake, na unaheshimu uamuzi wake wakati anapotulia, na kumbuka kuwa hasira ni hali ambayo mtu anakuwa hayupo ndani ya uhakika wake, kumbuka ndani akili yako kwamba mpenzi wako ameridhika na mtulivu na mwenye furaha. Na subiri kurudi kwake kwenye hali yake ya kweli kwa uvumilivu, ufahamu, hekima na subira.

Zawadi, bila kujali ilivyo ni jambo lenye kumstaajabisha kila mwanadamu, hivyo kuwa wa kwanza kumzawadia kitu chochote hata akikikataa kihasira, au muekee kando, kumbuka kuwa kuna aliyekuwa mbele yako ni mtoto mkubwa, anavuma na baada ya muda atatulia, na utakapompa muda ataokota zawadi yake ile na kuifungua kama watoto.

Hasira yoyote ile, bila kujali makali yake ni kiasi gani, hayakatishwi na kingine isipokuwa ni uvumilivu, hekima, huruma na tabasamu.

----------------------


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: