bayyinaat

Published time: 17 ,November ,2018      18:06:33
Tarehe 9 Mfunguo Sita Rabiul Awwali inasadifiana na siku muhimu katika historia ya Uislamu, nayo ni ya kuanza Uimamu na uongozi wa hujja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu....
News ID: 364

Mpenzi msomaji katika makala hii tutamzungumzo Imam Mahdi AF pamoja na kuanza uongozi wake baada ya kuuawa shahidi baba yake yaani Imam Hassan Askary AS.

Tarehe 9 Mfunguo Sita Rabiul Awwali inasadifiana na siku muhimu katika historia ya Uislamu, nayo ni ya kuanza Uimamu na uongozi wa hujja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Imam Mahdi (as). Siku ya kudhihiri Mahdi (as) inayosubiriwa kwa hamu kubwa na walimwengu, itakuwa mwisho wa dhulma na mashaka yote ya wanadamu. Siku hiyo dhulma na uonevu vitafunga virago na haki na uadilifu vitatawala dunia nzima.

Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) alizaliwa katika siku ya nusu ya mwezi wa Shaaban mwaka 255 Hijria katika mji wa Samurra nchini Iraq. Ni mtoto wa Imam Hassan Askary (as) na Bibi Narjisambaye baadhi ya riwaya zinasema ni binti Yoshua, mtoto wa Kaisari wa Roma kutoka kizazi cha Sham'un aliyekuwa miongoni mwa Hawaruyyun na masahaba wa karibu sana wa Nabii Issa Masih (as).

Kipindi cha uongozi wa Imam Hassan Askari (as) kilikuwa miongoni mwa vipindi vigumu sana kwa Ahlul-Beit wa Mtume (saw). Khalifa Muutamid wa kizazi cha Bani Abbas kwa kutegemea habari zilizokuwa zimemfikia, alijua vyema kwamba, hujja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu SW atakayepambana na madhalimu na kuasisi utawala wa uadilifu na Tawhidi kamili kote duniani atazaliwa katika nyumba ya Imam Askary (as). Kwa msingi huo alifanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba, anazuia hilo lisitimie. Hata hivyo Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) alizaliwa kwa uwezo wa Allah na baadaye akaenda ghaiba na kutoweka mbele ya macho ya walimwengu hadi atakaporuhusiwa kudhihiri tena katika kipindi cha akher zamaan na karibu na mwisho wa dunia.

Imani ya kudhihiri Imam Mahdi AF

Imani ya mustakbali mwema na kudhihiri mwokozi wa dunia nzima iko katika dini nyingi na ni itikadi inayozishirikisha karibu dini zote za mbinguni. Dini hizo zinaamini kuwa, mwokozi huyo atadhihiri na kusafisha dunia na dhulma na kueneza uadilifu na haki. Dini za mbinguni zinaamini kwamba, utafika wakati ambapo ufisadi, dhulma na uonevu vitaenea na kutawala duniani nzima. Wakati huo ndipo atakapodhihiri mwokozi aliyeahidiwa na kufanya mageuzi makubwa ya dunia na hatimaye kukomesha dhulma, ufisadi na ukandamizaji. Waislamu wanaaminimwokozi huyoaliyeahidiwa kuja kuijaza dunia uadilifu baada ya kujaa dhulma na uonevu, ni mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Mahdi (as). Waislamu wanamwita Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), na Wakristo wanasema mwokozi wa akheri zamaan atakuwa Issa Masia(AS), wakati Wazartoshi wanasema jina lake ni Sushiant.

Itaendelea……..


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: