bayyinaat

Published time: 01 ,January ,2021      17:53:07
Uchambuzi wa Sinema Django bila minyororo.
Uchambuzi wa Sinema Django bila minyororo.
News ID: 394
Uchambuzi wa Sinema
Django bila minyororo.

Huenda Kwa mtazamo wa kwanza na wa haraka haraka, wengi wa wakaona kuwa Quentin Tarantino anatoa heshima kwa mfumo wa kimagharibi (mfumo ambao unaitakidi umepambana na suala la ubaguzi wa rangi), lakini unapoangalia filamu hii kwa makini unapata kuwa asili ya matukio yenyewe ni kinyume sana na fikra hizi.
Tarantino kwa muda mrefu amekuwa akiitakidi kuwa ubaguzi wa rangi Umekuwa ni jambo la kawaida sana mioyoni mwa watu wengi ulimwenguni.
Na amedhihaki suala hili kwq njia moja au nyingine katika filamu zake alizozitengeza. Ila katika filamu hii ya Django hii ndio imekuwa dhana kuu.
Filamu hiyo inaeleza hadithi ya mtumwa anayeitwa Django (Jimmy Foxx) ambaye usiku mmoja kipindi wanasafirishwa pamoja na watumwa wengine anakombolewa na Daktari wa Meno aitwaye Dokta Schultz.
Baada ya muda mfupi Django anagundua kwamba Schultz ni mshindi wa Tuzo, na Dokta Schultz anatambua kuwa Django ni mtu mwerevu na mwenye ari. Anamwomba amsaidie kunasa baadhi ya watu na malipo yake anaahidi kumsaidia kumkomboa mke wa Jango, ambaye anashikiliwa mateka na bwana mkatili anayeitwa Calvin Kennedy (Leonardo DiCaprio).
Makubaliano haya yanakuwa ni mwanzo wa safari ya kuvutia ya mtu mweupe na mtumwa mweusi aliyeachiliwa, katika jamii iliyojaa ubaguzi wa tabia na kiakili.
Wakiwa safarini Django analipa kisasi kwa wale waliomdhalilisha na kumtumikisha yeye na watu wa wakati wake kwa sababu ya rangi yao ya ngozi.
Tarantino alinukuliwa akisema katika mojawapo ya mahojiano kwamba, jamii ambayo Django anakabiliana nayo ni ii hii ambayo watu ulimwenguni kote wanaishi leo. kwa ibara nyengine ni jamii yetu ya leo na sio ya zama zile.
Tarantino, kama mkurugenzi, hataki kuwahofisha watu zaidi ya kawaida, kwa sababu watu wengi wanaonekana kuamini kwamba wametatua tatizo la ubaguzi wa rangi ilhali uhalisia sivyo kabisa.
Kile ambacho Tarantino anasema juu ya filamu hiyo ni kweli kabisa.

Ubaguzi unaweza ukafanyika leo pia, na ni mara nyingi tu tunasikia kutoka kwa watu wengi, na katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kuhusiana na jamii tofauti na hii ni suala la kutisha.
Kwa kweli, ingawa filamu hiyo ni ya kikatili, uwezo wa kuchekesha wa ndani ya kazi
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: