bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2022      07:09:20
ULIZA UJIBIWE 001
00001- Baada ya barzakh ,je wanawake watakao kuwa mahurlain waume zao wakikosa pepo na Allah apishie mbali ,Je itakuwaje?
News ID: 436
00001-
Assalam aleikum  jamani  ni swali  la Baada ya barzakh  ,je wanawake  watakao  kuwa mahurlain  waume  zao wakikosa pepo  na Allah  apishie mbali ,Je itakuwaje?

Jawabu: 
Hilo swali lako tutalipanua Zaidi ili kupata faida zaida, na kuondoa shaka katika pande zote za jambo hili. Nalo ni kuwa:
1) Nini hali ya mwanamke aliyeolewa na zaidi ya mume mmoja katika ulimwengu huu kwa nyakati tofauti, 
2) au ambaye alikuwa bora kiimani na matendo kuliko mumewe, 
3) au ambaye hakuwahi kuolewa katika ulimwengu huu, au aliachana na mumewe kwa talaka au kwa ujane.
Na jibu la kila moja ya hali hizo ni kuwa, 
1) Ikiwa ataolewa na zaidi ya mume mmoja, atachaguo mmoja wao, aliyeishi naye vizuri Zaidi duniani:
سألت أم سلمة النبي (ص) فقالت: بِأَبِي أَنْتَ وَ أُمِّي، الْمَرْأَةُ يَكُونُ لَهَا زَوْجَانِ فَيَمُوتُونَ وَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ، لِأَيِّهِمَا تَكُونُ ؟ فَقَالَ ص: يَا أُمَّ سَلَمَةَ تَخَيَّرْ أَحْسَنَهُمَا خُلُقاً وَ خَيْرَهُمَا لِأَهْلِهِ، يَا أُمَّ سَلَمَةَ إِنَّ حُسْنَ الْخُلُقِ ذَهَبَ بِخَيْرِ الدُّنْيَا وَ الْآخِرَةِ. (الأمالي للصدوق ص 498)
 
Umm Salamah alimuuliza Mtume (s.a.w.a.) na kusema: Je! Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako, (ikiwa) Mwanamke ana waume wawili (kwa nyakati tofauti), kisha wanakufa na kuingia Peponi, atakuwa mke wa yupi?
Mtume (s.a.w.a.) akasema: Ewe Umm Salamah, atamchagua mbora kati yao wawili kwa tabia na aliyekuwa mbora kati yao kwa familia yake, Ee Umm Salamah, hakika tabia njema imebeba kheri ya dunia na akhera. (Al-Amali cha Al-Saduq, uk. 498)

2) Na ama mke aliyekuwa bora kuliko mumewe, Ikiwa atamchagua mumewe aliyekuwa naye duniani, basi atakuwa mkewe peponi, na ikiwa hatamchagua, anaweza kuwa mke wa mume mwingine katika waumini wa ulimwengu.
فقد روى العياشي بالإسناد إلى أبي عبد الله عليه السلام، قَالَ: قُلْتُ لَهُ: جُعِلْتُ فِدَاكَ أَخْبِرْنِي عَنِ الْمُؤْمِنِ تَكُونُ لَهُ امْرَأَةٌ مُؤْمِنَةٌ يَدْخُلَانِ الْجَنَّةَ يَتَزَوَّجُ أَحَدُهُمَا بِالْآخَرِ؟ فَقَالَ: يَا أَبَا مُحَمَّدٍ إِنَّ اللَّهَ حَكَمٌ عَدْلٌ، إِنْ كَانَ هُوَ أَفْضَلُ مِنْهَا خَيَّرَ هُوَ فَإِنْ اخْتَارَهَا كَانَتْ مِنْ أَزْوَاجِهِ، وَ إِنْ كَانَتْ هِيَ خَيْراً مِنْه خَيَّرَهَا فَإِنِ اخْتَارَتْهُ كَانَ زَوْجاً لَهَا..(بحار الأنوار ج8 ص105)

Al-Ayyashi anasimulia kwa silsila ya mapokezi (sahihi) kutoka kwa Abu Abdullah (Imam Swadiq), (a.s.), anasema: Nikamwambia: Niwe fidia kwa ajili yako? Nijulishe kuhusu muumini, ambaye ana mke muumini , watakapoingia Peponi, je wao wataowana? 
(Imam) akasema: Ewe Abu Muhammad, hakika Allah ndiye hakimu muadilifu, ikiwa ndiye mbora kuliko mkewe, basi atapewa yeye nafasi ya kuchagua. Akimchagua basi atakuwa miongoni mwa wake zake (wa peponi).Na ikiwa mke ndiye mbora kumliko yeye, (mke) atapewa nafasi ya kuchagua, basi akimchagua, atakuwa mumewe (wa peponi)...(Biharul anwar juzuu 8, ukurasa 105)
3) Ama yule ambaye hakuolewa katika ulimwengu huu, au aliachana na mumewe kwa talaka au kwa ujane (mume kufariki kabla yake)
Atakuwa mke wa mmoja wa waumini Peponi, kwani inaripotiwa kuwa waumini wana wake wengi wa kibinadamu na wengi wa Hurul ain.
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: