bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2022      07:16:35
ULIZA UJIBIWE 002
Mke akiwa ni mmoja katika Hurul Ain je na hurul Ain wengine ambao yasemekana watazawadiwa je cheo chake huko peponi kitakua vipi , huurul Ain atakua wakwanza au wa pili au au ... au hamna cha wakwanza wala wa pili wala , wala .... Inshallah, wa billahi Taufiiq
News ID: 437
00002-
Swali: 
Mke akiwa  ni mmoja  katika  Hurul Ain  je na hurul Ain  wengine  ambao  yasemekana  watazawadiwa je cheo chake  huko  peponi  kitakua  vipi  , huurul  Ain  atakua wakwanza  au  wa pili au au ... au  hamna  cha wakwanza wala   wa pili  wala , wala .... Inshallah,  wa billahi  Taufiiq

Jawabu:
Mke wa dunia kwa matendo mazuri na ucha Mungu, atakuwa :

1) Ima sawa na hurul ain kama vile hii hadithi inavyosema:

 عن نبينا الأكرم صلى الله عليه وآله حين قال:‏ أَيُّمَا امْرَأَةٍ كَتَمَتْ سِرَّ زَوْجِهَا فَلَمْ تُطْلِعْ عَلَيْهِ أَحَداً فَهِيَ فِي دَرَجَاتِ الْحُورِ الْعِينِ‏ فَإِنْ كَانَ فِي غَيْرِ طَاعَةِ اللَّهِ فَلَا يَحِلُّ لَهَا أَنْ تَكْتُمَ‏ (إرشاد القلوب للديلمي ج‏1 ص174)
Mtume wetu (s.a.w.a.) alisema: Mwanamke yeyote atakayeficha siri ya mumewe bila ya kumjulisha yeyote, basi yeye  atakuwa daraja sawa na hurul ain. Lakini ikiwa (siri hii) ni katika mambo ya kutomtii Mwenyezi Mungu basi si halali kwake kuificha. (Irshadul Qulub cha Daylami, Juzuu 1, uk. 174)

2) Lakini Akizidisha amali atakuwa bora kuwaliko hurul ain. 
أم سلمة تسأل النبي (ص) عندما ذكر الحور العين فتقول: بِأَبِي أَنْتَ وَ أُمِّي يَا رَسُولَ اللَّهِ أَمَا لَنَا فَضْلٌ عَلَيْهِنَّ ؟ قَالَ: بَلَى، بِصَلَاتِكُنَّ وَ صِيَامِكُنَّ وَ عِبَادَتِكُنَّ لِلَّهِ بِمَنْزِلَةِ الظَّاهِرَةِ عَلَى الْبَاطِنَةِ (الاختصاص ص348)
Ummu Salamah alimwuliza Mtume (sawa) alipotaja hurul ain, kwa kusema: "Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako, ewe Mjumbe wa Allah, je! Sisi si bora kuliko wao?"
Akasema: Ndio, kwa maombi yako, kufunga kwako, na kumwabudu Mungu kwa njia ile ile inayoonekana juu ya ndani (Al-Ikhtisas uk. 348).
3) Na pia ni mbora kuwaliko kutokan na mitihani wanayopitia wanawake duniani:  

سبق لأمنا حواء أن طلبت من ربها طلباً فقالت: أسألك يا رب أن تعطيني كما أعطيت آدم.
فقال الرب عز و جل: إني قد وهبتك الحياء و الرحمة والأنس، و كتبت لك من ثواب الاغتسال و الولادة ما لو رأيته من الثواب الدائم، والنعيم المقيم، والملك الكبير، لقرت به عينك.
يا حواء، أيما امرأة ماتت في ولادتها حشرتها مع الشهداء، يا حواء، أيما امرأة أخذها الطلق إلا كتبت لها أجر شهيد، فإن تحملت‏ و ولدت، غفرت لها ذنوبها و لو كانت مثل زبد البحر و رمل البر و ورق الشجر، وإن ماتت فهي شهيدة، و حضرتها الملائكة عند قبض روحها، و بشروها بالجنة، و تزف إلى بعلها في الآخرة، وتفضل على سائر الحور العين‏ بسبعين درجة. فقالت حواء: حسبي ما أعطيت (البرهان في تفسير القرآن ج‏3 ص356) 
Mama yetu Hawa hapo awali alikuwa amemwomba Mola wake ombi, kwa kusema: Nakuomba, Ee Mola wangu, unipe kama ulivyompa Adam.
Mwenyezi Mungu akasema: Nimekujaalia haya, na rehma na wewe kuwa kitulizo, na nikakuandikia thawabu ya kuoga na kuzaa, kiasi ambacho ikiwa utaiona hiyo thawabu ya kudumu, neema ya milele, na ufalme mkubwa, macho yako yangepata kwa hayo tulizo.
Ewe Hawa, mwanamke yeyote anayekufa wakati wa kuzaa, nitamkusanya pamoja na mashahidi. Ee Hawa, mwanamke yeyote anayepatwa na uchungua mazazi  nitamwandikia thawabu ya shahidi. Ikiwa atatahamili na kuzaa nitamsamehe madhambi yake, hata kama ni kama povu la bahari, mchanga wa nchi kavu na majani ya miti, na akifa, yeye ni shahidi.Na malaika watahudhuria wakati wa kutoka roho yake, na kumpa bishara  ya Peponi, na atasindikizwa kwa mumewe huko Akhera, na kufadhilishwa juu ya hurul ain wote kwa daraja sabini.Hawa akasema: Inatosha yale niliyopewa (Al-Burhan fi Tafsiril Qur’an, juzuu ya 3, uk. 356).

4) Ni mwenye kupendeza Zaidi kuliko hurul ain:

هذا في الفضل، وأما في الجمال، فقد ورد عن الإمام الصادق عليه السلام: الْخَيْرَاتُ الْحِسَانُ مِنْ نِسَاءِ أَهْلِ الدُّنْيَا وَ هُنَّ أَجْمَلُ مِنَ الْحُورِ الْعِين‏ (من لا يحضره الفقيه ج‏3 ص469)
Imepokelewa kutoka kwa Imam Swadiq, (a.s.): alkheiratil hisan ( mema) ni miongoni mwa wake wa watu wa dunia, na ni wazuri (wenye jamala) zaidi kuliko hurul ain (Man la yahdhuruhul Faqih, juzuu ya 3, uk. 469)
5) Hurul ain ni wa aina kadha, kuna wale Allah amewaumba kuwa wake wa waumini, na kuna wengine amewaumba kuwa wajakazi na watumishi wa wanaume na wanawake. Na pia kuna aina wengine pia.

وقد ورد في الحديث الشريف عن النبي (ص) : وَ مَا مِنِ امْرَأَةٍ تَكْسُو زَوْجَهَا إِلَّا كَسَاهَا اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ سَبْعِينَ خِلْعَةً مِنَ الْجَنَّةِ كُلُّ خِلْعَةٍ مِنْهَا مِثْلُ شَقَائِقِ النُّعْمَانِ وَ الرَّيْحَانِ، وَ تُعْطَى يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَرْبَعِينَ جَارِيَةً تَخْدُمُهَا مِنَ‏ الْحُورِ الْعِين‏ (مستدرك الوسائل ج14 ص245)
Imepokewa Hadithi tukufu kutoka kwa Mtume (s.a.w.a.): Mwanamke yeyote altakayemvisha mumewe, Mwenyezi Mungu atamvisha Siku ya Qiyama mavazi sabini katika mavazi ya peponi, kila vazi katika mavazi hayo ni mfano wa ua la Anemone na rehani, na Siku ya Qiyama atapewa wajakazi arobaini katika hurul ain wawe wakimtumikia. (Mustadrakul wasail juzuu 14, uk. 245).
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: