bayyinaat

Published time: 28 ,March ,2017      13:59:14
Pia tukitaka familia zetu ziwe bora ni lazima kuzingatia mambo haya baada ya kuzingatia mambo kadhaa niliyotaja hapo awali, nayo ni lazima nyumba ya wanandoa itawaliwe na upendo, utulivu na huruma, mambo matatu haya ndio chanzo.........
News ID: 67

UTAFANYA NINI ILI UFANIKISHE NDOA YAKO?!

Vitabu na Makala nyingi zimeandikwa kuhusu familia na kueleza umuhimu na maana ya familia, na kuzungumzia kila nyanja inayohusu familia.

Uandishi wa Vitabu na Makala haukuathiri kama inavyohitajika kwani kila siku inayokwenda ndivyo jamii inaporomoka na kupoteza tamaduni zake, na sababu ya kutoathiri Vitabu na Makala hizo ni kuwa kinyume na mafunzo ya Mtukufu Mtume Muhammad (saaw) na kufuata mafunzo yasiyokuwa na msingi wa aina yeyote ile.

Katika Makala hii tutajitahidi kuelezea nini la kufanya ili tufaanishe ndoa zetu, na kufanya ndoa zetu kupigiwa mifano katika jamii.

Katika kujenga familia kuna mambo kadhaa lazima kuzingatiwa:

1. kufahamu ukoo na nasaba ya pande mbili (upande wa Kiume na Wa kike).

2. Kuangalia hali ya kiuchumi kwa pande mbili.

3. Elimu kwa pande mbili.

4. Miaka na mengineyo mengi ya weza kuwa sababu ya mafanikio ya uundaji familia.

Pia tukitaka familia zetu ziwe bora ni lazima kuzingatia mambo haya baada ya kuzingatia mambo kadhaa niliyotaja hapo awali, nayo ni lazima nyumba ya wanandoa itawaliwe na upendo, utulivu na huruma, mambo matatu haya ndio chanzo na msingi wa kufanikisha maisha ya ndoa na bila mambo hayo ndoa haina maana, kwani haiwezekani kufikiria mtu ambaye anayetaka kuweka uhusiano na mtu mwingine ilhali ya kuwa yeye hana aina yoyote ile ya hisia kwake ila baadhi ya sehemu tu ambazo si mahala pake tutakua tumetoka nje ya mada.

Kuzingatia mambo hayo Mwenyezi Mungu amesema:

وَمِنْ آَيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآَيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

"Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, na amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.” Surat Ar-Rum 21

Swali la muhimu ni kwamba; Maneno ya Mwenyezi Mungu ya ashiria kuwa ndoa ipo sambamba na upendo unaposema ndoa unamaanisha upendo, kwa mantiki hii kwanini inasisitizwa mno upendo katika ndoa ilhali ya kuwa ndoa ndio upendo?!!

Ni kweli ndoa ndio upendo ila upendo huu ni kama shamba, lahitaji miundo mbinu ili kupata matunda mema, na miongoni mwa miundo hiyo ni kufahamu kwanza Ardhi ina uwezo gani wakuzalisha mazao na ni mazao gani yanayofaa katika Ardhi hiyo na mengi zaidi hukaguliwa kabla ya kilimo.

Upendo katika ndoa ndio nguzo muhimu na kuzinatia hilo utakuwa umeandaa mafanikio ya ndoa na familia yako, ndoa ni shamba lililomwagiliwa maji na kutoa matunda mema, na matunda ya ndoa ni utulivu na uaminifu baina ya pande mbili ili kuandaa mazingira mazuri kwa kizazi kinachokuja.

Ili kuepuka kurefusha makala hii hakuna budi kueleza njia rahisi ya ufanikishaji ndoa na kuendeleza mapenzi na upendo uliokuwa ndani ya familia, kufanikisha hilo lazima ufuate njia tatu hizi;

1. Zidisha kusema kauli hii (nakupenda) katika nyumba yako, na kumwambia (nakupenda) kila mmoja katika familia yako hata Mtoto mchanga.

Kuthibitisha hayo imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) akisema:

قول الرجل للمرأة إني أحبك لا يذهب من قلبها أبداً.

"Kauli ya Mwanaume (Mme) kumwambia Mwanamke (Mke), hakika mimi nakupenda, kamwe (neno hili) haliondoki moyoni mwake”

Naye imamu Imam Jaafar Sadiq (as) anasema:

إن الله ليرحم الرجل لشدة حبه لولده

"Hakika Mwenyezi Mungu amsamehe Mja kwa mapenzi mengi kwa Mtoto wake.”

2. Zidisha kubusu watu wa familia yako, Watoto na...

Imepokelewa kuwa siku moja alikuja mtu kwa Mtume (s.a.a.w) na akamwambia Mtume (s.a.w.w): Kamwe sijawahi kubusu Mtoto, na alipoondoka Mtu yule Mtume (s.a.w.w) aliwaambia watu akisema: Mtu huyu niliyekuwa naye ni wa motoni”

Ndugu msomaji mambo haya ni madogo kutoonekana na faida yoyote ile ila athari na taathira yake ni kubwa, kuzingatia mambo hayo bila shaka utakuwa ni mwenye kufanikisha ndoa na familia yako.

Na Sheikh Khamis Sadik

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: