ELIMU, MUHIMILI WA KILA KITU

ELIMU, MUHIMILI WA KILA KITU

Mmoja kati ya maimamu kumi na wawili naye si mwingine ni Imamu Ridhaa (a.s) amepokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akisema:

العلم امام العمل.

ELIMU NI KIONGOZI WA MATENDO.

Hapana shaka kwamba, kabla ya kufanya amali na kazi yoyote ile, kuitambua amali hio nakua na ufahamu nayo ni jambo la dharura,

Na kutokuwepo ufahamu nayo ni jambo la dharura, na kutokuwepo ufahamu na weledi wa hilo ni sawa na kuandamana katika usiku wa kiza totoro.

kazi na hatua zinazo chukuliwa na watu ziko makundi mawili:

1- kazi zinazofanywa kwa mujibu wa elimu na ufahamu ambazo hufanyika baada ya kuweko uchunguzi na tathmini ya lazima na yakila upande kuhusiana na kazi husika.

2- Kazi zinazo fanywa kibubusa, kwa kutanguliza misingi ya hisia, tena bila ya kuweko tathmini na chaguo kuhusiana na kazi husika.

Ni wazi kwamba, kazi ambayo inafanyika kwa ufahamu wa elimu sahihi na uchunguzi wa lazima hufikia katika lengo tarajiwa na hivyo kuwa na natija ya lazima na maridhawa.

Kazi ambazo na chimbuko lake ni uelewa na ufahamu ni kazi ambazo zina msingi imara nakuwa na sudi na faida ndani yake;

Na bila shaka zina vigezo vya lazima vinavyo hitajika.

kwa hakika kazi ambazo zinafanyika pasina kuweko na uchunguzi wa kielimu na utafiti wa lazima huwa hazina natija ya maana na sahihi na haziwezi kufanya mtu akaribie katika lengo lake.

Kwa muktadha huo basi, kazi sahihi na zenye thamani ni zile ambazo nyanja zake zote na mazingira yake yamechunguzwa katika fani ya kielimu katika nyanja zote.