Ni yapi madhara ya UVUTAJI WA sigara?: SEHEMU YA KWANZA

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU


"وَلَا تُلْقُوا بِأَيدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ".

"wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo”.

Je! Uvutaji wa sigara ni hatari kwa mwanadamu, nini maana ya uvutaji wa sigara? Husababishwa na nini tabia hii? Ni yapi madhara yake? Tutamsaidia je! Mvutaji wa sigara ili kuepuka tabia hiyo?

Mpenzi msomaji: Tambua kwamba moshi wa sigara ni sumu kali yenye kuathiri vibaya mwili wa mwanadamu, na uvutaji wa sigara ni hatari mno sawa uwe kwa ajili ya kupata ladha kinywani au kunusa hewa yake. Na ulevi wa majani hayo huwa kwa njia mbalimbali, kwa kutumia njia ya sigara yenyewe au (shisha) marijuana, au kutafuna tumbaku na mirungi n.k.

Moshi huwa ni wenye sumu nyingi, lakini sisi tutataja misombo ya moshi muhimu zaidi, ikiwa ni pamoja na: nikotini, ambayo ni kifungu chenye sumu kali inayosababisha hali ya mwili inayoitwa "mihadari", na mihadarati ni mwili kuwa na haja ya nikotini kwa kukuza kiwango cha nikotini katika damu, na pia hutumika katika sekta ya kuua baadhi ya aina ya wadudu ambao ni walinzi wa mwili.

Lami pia ni sehemu ya aina inayozalika kutoka katika moshi, vilevile ni sumu inavyosababisha kansa, na usumbufu wa kazi ya cilia inayofunika kuta za njia ya kupumua, na kusababisha kuvimba na kuzuia hewa na kuongeza kukohoa. Kama vile asidi ni aina ya kaboni ambayo hufahamika kuwa ni katika sekta ya moshi pia, na ni gesi ya sumu inayopelekea kubana kwa pumzi, na vilevile inazuia uhamisho wa oksijeni kuelekea kwenye damu, na hii hudhoofisha uwezo wa ukuwaji wa binadamu, na pia kudhoofisha uchangamfu unaofanya kazi za kila siku.

Ama hatari za sigara kwa mvutaji mwenyewe, ni nyingi na zinazomdhuru kiafya. Moshi husababisha magonjwa ya kupumua katika mwili, kama vile husababisha utasa, na kuwa sababu ya mashambulizi ya magonjwa ya moyo na kupooza pia. Na uwezekano wa ongezeko la hatari ya kansa kwa mvutaji, hasa kansa ya mapafu, kansa ya mdomo, kama mvutaji anaposumbuliwa na harufu kali ya kinywa ndivyo kansa hiyo hukirihisha sehemu za midomo yake. Na pia atakabiliwa na madhara ya kuzeeka mapema, aidha moshi wa sigara humsababishia mvutaji kifo cha haraka.
Tusisahau kutaja madhara hasi kuhusu sigara, ambayo ina maana ya hatari ya sigara ambayo hutokea kwa wale jirani wa mvutaji, kwa kunusa hewa ya sigara bila kuvuta sigara yenyewe. Hiyo inakuwa ni maandalizi ya watoto wake na wale walio karibu naye katika hatari ya kupatwa na kansa ya mapafu.
Lakini pia inaweza kusaidia mvutaji kuacha sigara kwa kuzungumza naye na kujaribu kumshawishi kwa kumueleza hatari ya moshi katika mwili wake na familia yake, na kwamba yeye hutumia fedha nyingi juu ya manunuzi ya sigara, ambapo laiti kama angelimbikiza hazina hiyo angeliweza kufanya jambo jipya katika maisha yake.
Aidha yawezekana kumtuma kwenye vituo vya kutoa mipango ya elimu na uendelezaji wa shughuli kuhusu madhara yanayo sababishwa na sigara.
Itaendelea ....

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.