Ni yapi madhara ya UVUTAJI WA sigara?:; SEHEMU YA PILI

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


HUKUMU ZA KISHERIA ZA UVUTAJI WA SIGARA NA SHISHA NI ZIPI?

Katika wasifa wa madhara ya sigara yaukumbao mwili wa binadamu imebainishwa kwa sana ma kukaririwa ukumbusho huo juu ya madharaya sigara kwa afya ya binadamu. Kwa minajili hiyo tunataka kubainisha utumiaji wa sigara kwa upande mwingine tukiangazia katika nadharia ya Qur’ani na hukumu za kisheria.
Ijapokuwa awali katika zama uhai wa nabii mtukufu (s.a.w.w) sigara na shisha ni vitu ambavyo havikuwepo, lakini imeshiriwa kwa uwazi ndani ya Aya za Qur’ni ya kwamba, mwanadamu hapaswi kudhuru afya yake na kuiangamiza nafsi yake. Na kwatika muendelezo wa mada hii tutaashiria Aya kadhaa na riwaya katika wasifa huu:

"وَلَا تُلْقُوا بِأَيدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ".

"Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo”.[1]

"وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ»

"Na anawahalalishia vizuri”.[2]

"وَلَا تَقْتُلُوا أَنْفُسَکمْ»

"Wala msijiuwe”.[3] Pia mtume mtukufu (s.a.w.w) amesema:

«لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ».

"Ni haramu kujidhuru mwenyewe na kusababisha kwa wengine maangamio”.[4]

MARAAJI WATOA HUKUMU IPI KWA MATUMIZI YA SIGARA?

Hujjatul islaam wa la- Muslimiin Adiib Yazdi. Mtafiti wa mambo ya kimadhehebu kwa mtazamo wa kiujumla hunena haya kuhusiana na hukumu ya uvutaji wa sigara na shisha, ya kwamba: Baadhi ya Marajii hutoa hukumu ya uharamu kwa uvutaji wa sigara na shisha, na baadhi kwa sababu ya kuwa si yenye kulevya, huihukumu kuwa ni makuruhu (jambo lenye kukirihisha).
Ameongeza kusema kuwa: Ikiwa mtu atavuta sigara na moshi wake kuwafika watu wengine na ukapelekea madhara kwao. Udhaifu na kukohoa kwa sana. Hakika amali au kitendo hiki ni haramu na hakifai.
Katika muendelezo wa fatua za baadhi ya marajii hususan katika suala la uvutaji wa sigara tunasoma kwamba:
Ayaatullah Khamenei:
Hakika hukumu hutofautiana kufuatana na hitilafu za madhara kwa utumiaji wa sigara, na kwa ujumla hairuhusiwi kutumia sigara endapo kiwango wa uvutaji huo kitapelekea madhara katika mwili, na ikiwa mtu atafahamu ya kwamba kuanza kuvuta itapelekea hatua hii hakika haijuzu kuvuta kwa wakati huo.
Ayaatullah Sistaani:
Swali: Kwa mujibu wa ushauri wa daktari ni kwamba uvutaji wa sigara ni sababu kubwa ya maradhi ya moyo na kansa, na wakati mwingine ni sababu ya kupungua umri, sasa ni ipi hukumu ya uvutaji wa sigara kwa watu wafuatao?
1 Mtu ambaye anaeanza kuvuta.
2 Aliyeathirika kwa kuvuta sigara.
3 Tukaapo kando ya mtu avuatae sigara, na ilihali daktari amekwishanena kwamba, yeyote atakayekaa karibu ya mvutaji sihara yatamfika madhara ya moshi wa sigara.
Jawabu: ni haramu uvutaji wa sigara endapo utasababisha madhara, sawa kwa baadae au kiujumla, na ima madhara yanayofahamika au yasiyofahamika, madamu kwa mujibu wa akili hupiga dhoruba afya ya bianadamu basi ni haramu jambo hilo. Ama ikiwa kinga ya madhara itakuwa kali hadi kupunguza madhara hayo, hakika hapana kizuizi.
Ikiwa kuendelea kuvuta sigara itazidisha madhara lazima aache, isipokuwa pale ambapo endapo ataacha kuvuta kwa ghafla itasababisha madhara, mfano wa madhara yapatikanayo ikiwa ataacha kuvuta.
Mtu kama huyu ni mfano wa yule ambaye anayeanza, na jawabu la kifungu cha kwanza humshamili na yeye pia.
Ayaatullah Makarim shirazi:
Swali: Uvutaji sigara kwa wanaoanza, na kuendeleza hilo kwa waliokwisha athrika, sawa kuacha kwake ni rahisi au ngumu, ni ipi hukumu yake?
Jawabu: Uvutaji wa sigara na aina ya mioshi, ni haramuna kwa kuzingatia kwamba kuacha hayo kwa walioathirika ni jambo lawezekana, suala la wasiwasi kawaida halizingatiwi, isipokuwa kwa amri maalum ya daktari bingwa na mwerevu, na hapana tofauti kati ya aliyeathirika na mioshi au anayeanza.
Ayaatullah Haadawi Tehrani:
Utumiaji wa moshi kwa dalili ya madhara yake ni haramu moja kwa moja.
Ayaatullah Saafi Golpaygan:
Kula au kuvuta kitu ambacho ni sababu ya kuleta madhara kwa akili ya mtu au afya yake ni haramu (kitu hicho), lakini ikiwa ni madhara ya muda mfupi au machache ambapo akili haitadhurika wala kusumbuka, si jambo haramu.
Katika hitimisho lazima ifahamike kwamba Dini tukufu ya Uislamu imesisitiza mno suala la kulinda nafsi ya mwandamu, mali yake, heshima yake na haiba yake, na madaktari wote na maulamaa wa kidini wameafikiana juu ya mambo hayo, na kwamba uvutaji wa moshi hupelekea dosari katika afya ya mwanadamu na nafsi yake, hivyo ni lazima kuacha, na hapana madhara mengine makubwa zaidi ya kupoteza nguvu kazi ya mwili, nafasi ya kijamii na mali za watu ambazo ni thamani kuu ya jamii za binadamu.
UVUTAJI WA SIGARA NI HARATI KWA AFYA YAKO.

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.[1] Surat al- baqarah, 195.

[2] Surat al- A’raaf, 157.

[3] Surat an- Nisaai, 29.

[4] Sahih a;- Jaami.