JE! UVAAJI HIJABU UNAFAIDA AU NI MADAI YA UISLAMU?

JE! UVAAJI HIJABU UNAFAIDA AU NI MADAI YA UISLAMU?

Ashukuriwe mola mmiliki wa mbingu na ardhi, mlezi wa viumbe vyote, na rehema na amani iwe juu ya kipenzi chake Muhammad {s..a.w.w }na masahaba wake wema waliofuata mwenendo wake mwema hadi siku ya mwisho.

Baada ya utangulizi mfupi, Uislamu umetoa mafunzo mema katika kila nyanja na harakati zote za mwanadamu ili aishi maisha mema yasiyokuwa na dosari.

Uislamu ulishatoa mafunzo mengi kunako Mwanamke au Wanawake na jamii na jinsi ya kujihifadhi na kujihifadhi kuna maana gani? Je! Mwanamke jinsi atakavyo taka kujihifadhi ndivyo atakavyo jihifadhi? Au ni kutokana na mafunzo ya Kiislamu au mafunzo ya dini aliyokuwa nayo?!!...

Mitume waliyopita ulinganiaji wao haukuwa na tofauti bali kila mmoja alikuwa mwendelezaji sera za waliomtangulia kabla, utakapo kuwa ni mfuatiliaji sera za mitume waliopita utakuta kuwa swala la hijabu si la Uislamu bali ni uendelezaji yale yaliobakishwa na dini zilizopita.

Hijabu ni sitara na hifadhi njema iliyomueka mwanamke kuwa bora katika jamii, tofauti na kipindi cha Mtume Muhammad {s.a.w.w} kipindi ambacho mwanamke alikuwa kama takataka bila kuwa na hadhi yoyote ile kama alivyo kuwa nayo hapo kabla.

Hijabu ilikuwepo kabla ya kutumwa Muhammad {s.a.w.w} ilikuwa kwa maana ya kujihifadhi na kusafika moyo na kuzuia macho kunako vitu ambavyo vya weza sababisha kumpelekea mtu hisia zake kufanya dhambi, sababu hiyo Uislamu ulikuja kuboresha swala hili kwa maana hijabu ni kuhifadhi mwanamke viungo vya mwili wake wote ila uso, mikono {viganja vya mikono} na miguu, {kuanzia katika fundo za miguu hadi visigino na vidoleni} hivyo ndivyo vyaruhusiwa kuwa wazi, miguu ni bora nayo kufunikwa, falsafa na lengo la Uislamu kulazimisha au kuwalazimisha waliyotangulia kujihifadhi hasa wanawake kila kiungo chake ambacho chaweza sababisha kuamsha hisia upande wa pili {mwanaume}.

Kwa mantiki hii swala la hijabu si la Uislamu pekee bali Dini zilizopita pia lilikuwepo na si madai ya Kiislamu ama faida ya hijabu si mahala pake kuwa nami.

FAIDA YA HIJABU KATIKA SIHA NA AFYA YA MWANAMKE

Mwili wa mwanadamu unahitaji vitu tofauti ili uwe salama kutokana na maradhi ya hapa na pale, mwenye kutaka kuwa salama na maradhi yampasa kutumia vitu au vyakula ambavyo vyauweka mwili kuwa salama kama matunda mbogamboga na vinginevyo, mazoezi nayo ni miongoni mwa vitu vinavyoweka mwili kuwa salama.

Maisha na Uhai wa mwanadamu yamemili na kutegemea oksijeni na haidrojeni bila vitu hivyo Uhai wa mwanadamu ungelikwa hatarini.

Bila shaka umbile la mwanadamu ni nzuri na bora kwani mwenyezi mungu alipo muumba mwanadamu alimuweka kuwa bora na kila kiungo kuweka mahala pake bila kukosea sehemu isiyo stahili kiungo hicho.

Mwenyezi mungu anasema:

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ

"bila shaka hakika tulimuumba mwanadamu katika umbo bora kabisa kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini”.

Maneno yake mola yapo wazi kabisa, umbile la mwanadamu jinsi lilivyo kuwa nzuri halina kifani wala methali ila tu usipo kuwa makini umbile hili waweza kulikosa au umbile hilo kuwa chini na kulikosa milele.

Umbile la mwanamke ni umbile lisilokuwa na dosari kwa sababu hiyo Uislamu ukatoa mafunzo mazuri kuhusu kiumbe ambacho ni pambo na pambo hilo lina njia tofauti ya kuhifadhiwa.

Uislamu ulipomuamrisha mwanamke kuvaa hijabu ulikuwa na malengo, miongoni mwayo ni kwamba mwili wa mwanamke kama ilivyo kuwa wazi ni tofauti na mwanaume mwili wake wapokea magonjwa haraka hasa katika viungo vyake ambavyo Uislamu umeamrisha kuvihifadhi, matundu ya mwili wa mwanamke ni makubwa zaidi kuliko ya mwanaume na matundu hayo kipindi mwanamke hajahifadhi mwili wake kama ipasavyo upumuaji wa mwili unakuwa ni zaidi na oksijeni yaingia katika mwili bila mpangilio wowote ule na matundu hayo ya funguka zaidi na mionzi ya Jua yaigia moja kwa moja bila kizuizi sababu hiyo ya weza sababisha maradhi tofauti kama upungukaji damu na maji na ngozi kuwa kavu na kuhisi mchovu kila mara na mengineyo muda hutoshelezi.

Faida ya hijabu ni kuhifadhi mwili kunako maradhi tofauti, mwanadamu kuwa salama ndiyo uhai wake kama ilivyo wazi na maradhi ya mara kwa mara husababisha umri na maisha yake kuwepo hatarini pia hijabu ya hifadhi hadhi ya mwanamke tafauti ya hapo kabla mwanamke alikuwa ni njia ya biashara tu.

Khasara aipatayo mwanamke sababu ya kutozingatia swala hili ni kama jinsi tulivyo nakili kutoka kwa Dr Nadia Husaini katika kitabu cheke cha {UMLIMWENGU WA WANAWAKE} akisema: {…hijabu ina athari na mchango mkubwa katika siha na afya ya mwanamke kuwa ni himaya ya mwili huzuia maradhi, huhifadhi nywele, nywele kiafya hazitakiwi kupigwa na mionzi ya jua moja kwa moja kwani oksijeni haina mchango katika ukuaji wa nywele bali husababisha nywele kuwa ngumu na kukatika na hili ni tatizo katika jamii limezagaa sababu ya kutofahamu na utatuaji wa tatizo hili ni swala dogo tu nalo ni hijabu…}

Faida ya hijabu ya rejea kwake mvaaji lengo kulinda na kuhifadhi Uhai wake, kama ambavyo khasara anayoweza kuipata endapo hatazingatia jambo hili na kama vile kuwa mwenye matumizi mengi ya pesa akiwa na lengo la kutibu maradhi au magonjwa yaliyomsibu sababu yake ikiwa ni kutozingatia hijabu, pia kuna hasara ya kinafsi ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na hasara ya mali, nayo ni kwamba hukabidhi roho yake bila kufikia malengo aliyokuwa nayo sababu ya msiba uliyompata kiini chake ni kutozingatia swala hili.

Je!! Mtu yu tayari kufanya kitu kinacho mdhuru au kujipa hali ya kuwa kinga yake anaijua na anaweza kuifanya?

Imeandikwa na Sheikh Khamis Sadiki