bayyinaat

Published time: 14 ,September ,2021      23:30:21
TARJUMA YA KITABU CHA YALIYO SAHIHI KATIKA SERA YA MTUME MTUKUFU (S.A.W.A.) - 001
MWANZO WA MAZUNGUMZO: Maisha ya jamii sio matokeo tofauti yasiyokuwa na uhusiano wowote, lakini ni endelezo, linalochukua yote yaliyopita katika juhudi zake za kila siku na mapambano endelevu na kuyaweka katika zama za sasa hivi, ili kupata kutoka kwake nguvu inayoitegemewa pamoja na harakati, na nyenzo za maendeleo yake, kisha maendeleo yake yaendelee katika hatua thabiti na tulivu kuelekea mustakbal anaoutamani na anaoutaka.
News ID: 431

DIBAJI [1]

MWANZO WA MAZUNGUMZO:

Maisha ya jamii sio matokeo tofauti yasiyokuwa na uhusiano wowote, lakini ni endelezo, linalochukua yote yaliyopita katika juhudi zake za kila siku na mapambano endelevu na kuyaweka katika zama za sasa hivi, ili kupata kutoka kwake nguvu inayoitegemewa pamoja na harakati, na nyenzo za maendeleo yake, kisha maendeleo yake yaendelee katika hatua thabiti na tulivu kuelekea mustakbal anaoutamani na anaoutaka.

Kwa hivyo ni kawaida sisi kupata athari wazi maishani mwetu ya kila siku, matokeo mengi ya kihistoria, hata yale ambayo yaliyotokea kwenye kina cha historia, na kufifia kiasi cha kukaribia kutoonekana, bali athari zake zinaonekana katika maisha ya mataifa na matendo yao, bali katika ufahamu wao na hisia zao, bila kusahao athari zake pia katika hali za kidini, fasihi, elimu, kisiasa, kiuchumi, na mahusiano ya kijamii, na kadhalika.

Hata ingawa athari za matokeo haya ya kihistoria hutofautiana kwa kina na mapana katika umma mmoja hadi mwingine, na kutoka kwa taifa moja hadi nyingine.

JUKUMU LA HISTORIA:

Ama historia jukumu lake ni kuonyesha kwa usahihi na uaminifu maisha ya hapo zamani ya umma, na hali ambazo walipitia, na misukosuko ya kifikra, matatizo ya kiuchumi na kijamii na mengineyo.

Na vilevile inatutilia mkazo umuhimu wa historia, na kudhihirisha kiwango cha athari zake maishani, na kutuonyesha sababu ya umma kufanya hima katika uandishi wa histotria yake, na katika kufanya utafiti, uchambuzi, na udadisi na katika kutafuta sababu za matokeo hayo.Basi kila umma unataka kujua kwa kupitia hayo baadhi ya mambo yaliyo fichika ya maisha yao wanayoishi.

Na ili wafaidike nayo kama msingi thabiti mgumu wa maisha yake ya baadaye, na kugundua kutokana nayo pia baadhi ya sababu za kupanda na kushuka kwake, ili hii iwasaidie kujijengea nguvu na usalama, na kujiandaa kwa maisha yake ya baadaye kwa misingi imara, yanye nguvu na kakamavu..

JE TUNAYO HISTORIA:

Sisi ni umma unaotaka kuishi maisha kwa nguvu zake zote, na kwa ufanisi, lakini huku tunamiliki historia tajiri iliyowahi kujulikana, lakini hatuna vitabu vya historia na turathi ambavyo tunaweza kutegemea kupata picha kamili, na sahihi ya matokeo ya yote yaliyotangulia, kwa kuwa mengi ya yale yaliyoandikwa yanatawaliwa na mitizamo finyu, na taassubi za kimadhehebu, na yanaelelekea mwelekeo wa kujipendekeza kwa watawala.

Kwa kusema "mitizamo finyu" ninamaanisha mchakato wa kutazama tukio kando na chimbuko na sababu zake, na kisha kando na natija na athari zake.

KWA IBARA ILIYO WAZI ZAIDI.

Kwa hakika tulicho nacho - haswa - ni historia ya watawala na masultani, na hata hii historia ya watawala, imepotoshwa na kubadilishwa, na wala haiwezi kuonyesha kwa uaminifu picha halisi ya maisha yao, mienendo na misimamo yao, kwa sababu mwanahistoria alikuwa akirekodi tu yale yanayolingana na matakwa ya mtawala, na yanayokwenda sambamba na matamanio yake, na yanatumikia maslahi yake, bila kujali ni kinyume gani na ukweli au kinyume na kile mwanahistoria mwenyewe anakiamini na kukikubali.

Kwa hivyo, hatutashangaa tukiona mwanahistoria anajishughulisha na mambo madogo na ya yaliyo duni, akifafanua na kuelezea kuhusu kikao la kunywa mvinyo, au mabishano ya amiri au mtawala, au anatunga matokeo au kubuni watu wasiokuwepo katika historia, na kisha kupuuza matokeo muhimu katika historia, au kuwapuuza watu muhimu wenye hadhi na athari kubwa katika historia na katika umma. au anayapotosha mambo yaliyofanywa na mtawala mwenyewe, au wengine, au anayaeleza - kwa sababu moja au nyingine - kwa usiri, na kuyaepusha na uwazi.

KUISOMA HISTORIA:

Kwa hivyo, yeyote anayetaka kusoma historia na kufaidika na vitabu vya kihistoria na vya turathi ni lazima avisome kwa tahadhari na ufahamu, na kwa umakini na kutafakari, ili asiingie katika mtego wa habari potofu na udanganyifu.

Ni lazima afungue macho na moyo wake kwa kila neno analopitia, na ajaribu iwezekanavyo kuhoji, na atoe ndani yake kile kinachopatana na ukweli, kinachoungwa mkono na dalili na ushahidi alioweza kukusanya, na kukataa au kuacha kila kilichochezewa na kuathiriwa na vishawishi na ubaguzi.

Hili sio jambo rahisi na jepesi, haswa kuhusiana na historia ya awali ya Uislam, ambayo ilitawaliwa na hisia za matamanio duni ya nafsi na taassubi za kidhulma, na ikachezewa na mikono ya watu wenye chuki, iliyoipora masimulizi yake mazuri na usafi wake kwa kiwango kikubwa sana.

NINI TUNATAKA:

Sisi kwa upande wetu, katika kitabu hiki, tutajaribu kudondoa picha safi na ya wazi kiasi kiwezekanacho kuhusu historia ya Mtume wetu Mtukufu (s.a.w.a).

Na umuhimu wetu zaidi utakuwa katika kuondosha hizo sehemu gonjwa za masimulizi, yaliyotungwa katika historia, ingawa mengi yake sio zaidi ya udanganyifu na takhayali, zilizoundwa na watu wenye nia mbaya, walaghai, wasimulizi wadanganyifu na wenye kutawaliwa na hawa za nafsi.

SIFA MSINGI ZA KIPEKEE ZA HISTORIA YA UISLAMU ILIYO ANDIKWA:

Tunasema yaliyotangulia, hata ingawa tumesema hapo juu, ya kwamba tunakinai kwamba historia ya Uislamu iliyorekodiwa - licha ya kasoro na mapungufu yake - ni historia tajiri zaidi ya umma iliyo wahi kurekodiwa, katika umma zote, na imetofautiana na historia nyinginezo kwa umakini na ushamiri wake wa matokeo, kwa kiwango ambacho mara nyingi utakuta imekurekodia harakati, ishara, na vidokezo, pamoja na maneno, misimamo na matokeo, kwa umakini wa hali ya juu na ushamiri usio kuwa na kifani.

Ongeza kuwa, historia ya Uislamu inamiliki aya nyingi za Qur'ani, kisha masimulizi mengi (ya riwaya) sahihi, ambayo hautapata katika historia yoyote nyingine.

Hii ni ikiwa hatutasema kuwa jambo hili ni moja ya sifa za kipekee za historia ya Uislamu, tutakapothibitisha uhakika kuwa hakuna historia inayoweza kuthibitisha madai yake ila kwa kiwango kidogo sana, na haswa katika undani wa mambo, na katika maelezo ya kimapana.

Na sifa nyingine ya kipekee inayotofautisha historia ya Uislamu, ni kwamba inamiliki misingi ambayo inaweza kumpa mtafiti njia salama, ambazo kwa kuzifwata anaweza kufikia uhakika anaoutaka, uwe mdogo au mkubwa.

Tutayazungumzia baadhi ya hayo katika baadhi ya milango ya kile tulichokiita "Utangulizi katika uchambuzi wa sera ya Mtume Mtukufu."

MWANZO KIKAWAIDA WA HISTORIA YA UISLAMU:

Ni wazi kwamba kikawaida mwanzo wa historia ya Uislam, na jambo kuu na la muhimu ndani yake ni sera ya Bwana wa Mitume, Muhammad "s.a.w.a."

Kwa hivyo hamna budi kuanza nayo, hata kama ni kwa kuchambua maswala na matokeo yaliyo msingi ndani yake, ili hii iwe kama hatua ya kwanza katika njia ya wataalamu na watafiti, waliohitimu na wenye hima za juu ya kuingia kwenye tafiti pana na za kushamiri.

Lakini huku kunahitaji kutoa utangulizi, ambao utatoa maoni ya jumla ya hali ya utafiti.

Basi tuingie kwenye utangulizi huu, ambao unabeba sura kadhaa...

Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuafikisha na mtoaji wa msaada, anayeombwa auni na Yeye ndiye wa kutegemewa..



[1]- Utangulizi huu ni makala kutoka kwa utangulizi wa kitabu chetu: «Maisha ya Kisiasa ya Imam al-Ridha, (amani iwe juu yake), na tumeileta hapa kwa sababu ya uhusiano wake wa moja kwa moja na mada yetu hii hapa, na ili tusilazimike kumwambia msomaji kukirejelea kitabu hicho.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: