bayyinaat

Published time: 16 ,December ,2017      20:11:25
Naam, mke ni lazima ajichunge na ajue mipaka yake, kama ambavyo inatakiwa ajue ni yapi anatakiwa kusema kwa mumewe na yapi hatakiwi kuyasema kwake, hebu chukulia mfano wa mwanamke ambaye siri zake yeye huzungumza na..........
News ID: 155

Kama ambavyo mwanaume au mume anatakiwa ajipambe na mambo kadhaa ambayo tumeyazungumzia katika makala iliyopita, vilevile mke anatakiwa ashikamane na baadhi ya mambo, kwa sababu lengo la kujenga msingi imara wa mahusiano yao si la mume peke yake, bali ni lengo la wao wote kama ambavyo lao ni la wote. Na katika kuelezea mambo hayo Imamu Sadiq (as) baada ya kutaja mambo ambayo mume anatakiwa kujipamba nayo, akaunganisha na mambo ambayo mke anakiwa pia kujipamba nayo. Anasema:

".....ولا غنى بالزوجة فيما بينها وبين زوجها الموافق لها عن ثلاث خصال وهن:
صيانة نفسها عن كل دنس حتى يطمئن قلبه إلى الثقة بها في حال المحبوب والمكروه
و حياطته ليكون ذلك عاطفاً عليها عند زلة تكون منها
وإظهار العشق له بالخلابة والهيئة الحسنة لها في عينه...."

".....Kisha mke siku zote anahitajika kumfanyia mume wake ambaye ameendana naye mambo matatu, nayo ni: Kujichunga nafsi yake kutokana na mabaya, ili mume wake awe na imani naye katika hali zote (Hasira na amani), Kuwa mke bora kwake ili tu mume awe na huruma naye itakapo tokea amemkosea, na kudhihirisha mapenzi yake kwa ulimi wake n akwa mwonekano mzuri mbele ya macho ya mume wake.......”.[1]

Ufafanuzi:

· Kwa kuwa lengo la kila mmoja wa wana ndoa ni kujenga misingi mizuri ndio maana mambo kama haya yanatakiwa kupatikana katika hayo mahusiano yao. Hebu tuangalie jambo moja moja katika mambo ambayo Imamu amayataja hapo juu.

1. Kujichunga

Naam, mke ni lazima ajichunge na ajue mipaka yake, kama ambavyo inatakiwa ajue ni yapi anatakiwa kusema kwa mumewe na yapi hatakiwi kuyasema kwake, hebu chukulia mfano wa mwanamke ambaye siri zake yeye huzungumza na mwanaume mwingine ambaye si mume wake, unadhani mume wake atakuwa na imani naye katika kila jambo?, bila shaka ni hapana!, n a ikitokea mume amekosa imani kwa mke wake basi hakuna cha kutarajia zaidi ya matatizo katika mahusiano yale. Sasa ili mke awe ni mwenye kuaminiwa na mume wake inatakiwa ajichunge sana.

2. Kuwa mke bora

Hapa Imamu alikuwa anaagalia upande wa kwamba namna gani mke anaweza kuwa mke bora kwa mumewe. Hivi unadhani mke ambaye hamtii mkewe, wala hashughuliki na mambo ya kuhudumia familia yake, kila siku yeye yupo mashughuli na mambo yake binafsi, anaweza kuwa mke bora kwa mumewe?. Kama jibu ni hapana basi mke wa namna hii asitarajie matunda anayopata mke bora hata siku moja, matunda hayo ni ambayo imamu amayataja katika hadithi kwamba, endapo huyu mke bora siku akiteleza basi mume wake humwelewa na huamiliana naye kwa upole na ukarimu n a kumwelewa. Ila kama hatakuwa mke bora basi jambo dogo tu huwa ni sababu ya ugomvi na malumbano makubwa baina yao, kwa sababu mume huchukulia jambo lile ni kama zao la mengine mengi ambayo yamepita.

3. Kudhihirisha mapenzi

Moja kati ya mambo ambayo watu wamekuwa wakiyafasiri ni kama udhalili ni swala la mke kudhihirisha mapenzi yake kwa mume wake au hata kinyume pia. Wakati ambao jambo hili ni katika mambo ambayo yanachangia kiasi kikubwa sana katika kuimarisha mahusiano yenu kama wana ndoa. Mke usifiche mapenzi yako kwa mume wako, mwambie tena kwa ulimi wako kwamba unampenda, hujui ni namna gani maneno yako hayo yatamuathiri katika moyo wake.

Kisha Imamu anamalizia kw akutaja njia nyingine ya kuonyesha kwamba mke anampenda mume wake na anadhihirisha hilo, nayo ni njia ya kupendeza mbele yake kwa yale ambayo amekuhudumia. Mume anajipinda anakununulia nguzo nzuri mfano, basi ivae mbele yake na si siku ambayo unataka kutoka na wenzako ndio uvae, kwani kufanya hivyo kunamvunja moyo mume.

Dhihirisha kwa mume kwamba unampenda.

Shukran kwa kuungana nami katika mada hii nikiwa na imani kwamba itapelekea watu kunufaika na haya ambayo tumeyaongea humu.

Sh Abdul Razaq Bilal.



[1] Tuhaful Uquul cha Ibn Shuubah Al Harraniy -ra- uk 323


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: