bayyinaat

Published time: 28 ,December ,2017      20:51:50
Hakuna shaka kuwa moja ya njia za kuujua Uislamu ni kuijua na kuifahamu sira iliyojaa fahari ya Mtume Muhammad SAW na Watu wa Nyumba yake au Ahlul-Baiti wake watoharifu.
News ID: 168

Mwaka 201 Hijria katika siku kama ya leo, yaani tarehe 10 Mfunguo Saba Rabiu Thani ulimwengu wa Kiislamu ulikumbwa na huzuni, ghamuu na majonzi makubwa kutokana na kuaga dunia Bibi Fatima Maasuma (Alayihas Salaam). Bibi Fatima Maasuma nib inti mwema na mtakasifu wa Imam Mussa al-Kadhima (AS). Alikuwa ni mwanamke mtukufu ambaye katika siku za mwisho za umri wake uliojaa baraka aliaga dunia katika sehemu ya ardhi ya Iran yaani mji wa Qum ambao pia umepambwa kwa ziara lake takatifu.

Sala na salamu za Mwenyezi Mungu zimfikie Mtume Muhammad na Watu wa Nyumba Yake. Sala na Salamu Zimfikie Bibi Fatima Maasuma SA mwanamke azizi ambaye ndugu yake, Imam Ali bin Mussa al-Ridha AS alisema hivi kuhusu adhama yake:

من زار اختی المعصومه بقم کمن زارنی

Atakayemzuru dada yangu huko Qum, ni kama amenizuru mimi.

Hakuna shaka kuwa moja ya njia za kuujua Uislamu ni kuijua na kuifahamu sira iliyojaa fahari ya Mtume Muhammad SAW na Watu wa Nyumba yake au Ahlul-Baiti wake watoharifu. Ingawa katika siku za hivi karibuni maadui wa Uislamu wamezidisha njama na hila zao za kuchafua jina la dini hii tukufu ya Mwenyezi Mungu sambamba na kumvunjia heshima Mtume Mtufuku SAW, lakini ukweli ni kuwa, Uislamu ni dini yenye mafundisho ya kudumu milele na pia sira ya Mtume SAW na Ahhulu-Baiti wake waliotakasika, wote wataendelea kuangazia dunia kwa nuru yao isiyozimika. Kwa hakika tunamshukuru Mwenyezi Mungu SWT kutokana na kututunuku neema ya Uislamu, Mtume Muhammad SAW na Ahlul Baiti wake.

NASABA YAKE

Bibi Maasuma (Salaamullahi Alayha) alikuwa bintiye Imam Mussa al-Kadhim AS na dada yake Imam Ali bin Mussa al-Ridha AS na alizaliwa mwaka 173 Hijria Qamaria. Alikuwa na umri wa miaka 10 tu wakati baba yake, Imam Kadhim AS alipouawa shahidi. Kwa msingi huo, zama zake za utotoni zilijawa na majonzi na huzuni ya kuaga dunia baba yake kipenzi. Pamoja na hayo kutokana na kuishi pamoja na ndugu yake aliyetakasika, Imam Ridha AS, cheche za matumaini zilibakia katika maisha yake. Mtukufu Fatima Maasuma SA alikuwa na kiwango cha juu cha imani na utakasifu. Katika zama zake za utotoni alikuwa na fadhila kubwa za kielimu na kimaanawi. Imenukuluwa kuwa, mwamamke huyu mtukufu hata katika zama zake za utotoni alikuwa akijibu maswali mengi sana ya kielimu na kifiqhi.

KAULI YA WANAHISTORIA KUHUSU FATIMA MAASUMA

Wanahistoria wanasema kuwa, Mtukufu Fatima Maasuma alikuwa mtaalamu wa hadithi na pia katika elimu na maarifa alikuwa na daraja ya juu. Wanasema kuwa, alikuwa amebobea katika nyuga hizo. Alijitahidi sana katika kujifunza sayansi na maarifa ya Kiislamu. Fatima Maasuma alifikisha amana kwa uaminifu mkubwa kwani kila ambacho alijifunza kutoka kwa baba yake alikifikisha kwa umma pasina kuwepo mapungufu yoyote. Alikuwa akinukuu hadithi kutoka kwa mababu zake na hadithi hizo zilikuwa zikitumiwa na Maulama wakubwa Waislamu.

Weledi wakubwa wa kidini walimtaja Fatima Maasuma kwa lakabu ambayo iliashiria cheo chake cha juu cha kielimu, kimaadili na kimaanawi. Lakabu kama vile 'Sidiqah' ambayo inamaanisha mwanamke msema kweli sana au lakabu ya 'Muhaditha' yaani mwanamke mwenye kufikisha au kusimulia hadithi. Alikuwa akinukuu hadithi kutoka kwa baba yake na babu zake watukufu.

JINA LA FATIMA MAASUMA KATIKA HADITHI

Jina la 'Fatima Binti Musa bin Jaafar' limeonekana katika silisila ya baadhi ya riwaya ambapo Maulamaa wa Kishia na Ahli Sunna wamenukulu na kuzikubali riwaya alizoziwasilisha kutokana na kuwa ziliweza kuthibitika na pia zilikuwa sahihi. Kati ya riwaya hizi ni zile zinazonasibishwa na Bibi Fatima Zahra AS na Mtume SAW. Hadithi hizo ni 'Hadithi ya Ghadir' na 'Hadithi ya Manzilat' kuhusu nafasi ya Imam Ali AS. Katika hadithi hii, Mtume SAW alijinasibisha na Imam Ali AS na kusema kwamba, nasaba hii ni kama ile ya Harun na Mussa (AS).

Hali kadhalika Fatima Maasuma SA katika kubainisha tukio muhimu la Ghadir, alifafanua kuhusu hadhi na cheo cha juu cha Ahlul-Baiti wa Mtume SAW ili watu wasighafilike na kile ambacho waliachiwa na Mtume wa Allah.

Kwa mujibu wa riwaya mbali mbali, Fatima Maasuma alikuwa na lakabu nyingine mashuhuri ya 'Karima Ahlul Bait'. 'Karima' ni neno lenye maana ya mwanamke mkarimu.

Itaendelea…..


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: