Ndugu Mwislamu Hijabu ni stara adhimu kwa
Mwanamke na huhesabika kuwa ni miongoni mwa hukumu za kisheria ambazo ni za
dharura katika dini tukufu ya Kiislam.
Mwenyezi Mungu amesema:
«يا أَيُّهَا النَّبِىُّ قُلْ لِأَزْواجِكَ
وَ بَناتِكَ وَ نِساءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ
ذلِكَ أَدْنى أَنْ يُعْرَفْنَ فَلا يُؤْذَيْنَ وَ كانَ اللَّهُ غَفُوراً
رَحِيماً».
"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti
zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza
kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye
kurehemu”. (Suratul Ahzaab/59).
Pia ni muhimu mno kuashiria nukta kadhaa
zinazohusiana na Umuhimu na falsafa ya vazi hilo ambazo ni hizi zifuatazo:
1. Kuheshimu vazi hili imepelekea kupungua
maovu katika jamii kwa wenye matamanio ya haraka pindi ionekanapo shepu ya
mwili wa mwanamke asiye jisitiri vizuri.
2. Hijabu inalinda heshima ya mwanamke,
ambapo wakati mwingine hijabu husaidia wanaume kumiliki hisia zao, kwa matakwa
yao wenyewe pindi mwanamke anapojisitiri.
Amesema Mtume Muhammad (saw):
النَّظر سهمٌ مسمومٌ من سهام
ابليس فمن تركها خوفاً من اللَّه اعطاه اللَّه ايماناً يجد حلاوته فى قلبه
"Kutazama (mwili wa Mwanamke asiyejisitiri)
ni mtego katika mitego ya Ibilisi, hivyo yeyote atakayeacha kutazama Miili ya
wanawake wasiojisitiri, basi Mwenyezi Mungu atampa imani thabiti ambayo atapata
ladha ya imani hiyo ndani ya moyo wake”.
Ndugu msomaji: Namna ya ushonaji nguo, una
mchango mkubwa katika vazi la kumstiri Mwanamke. Mavazi mepesi, mavazi ya
yakubana, ni makosa.
Hivyo, wadhifa wa Uislamu ni kumlinda
Mwanamke kikamilifu. kwa lengo la kuzuia kusisimua hisia za Wanaume wenye
matamanio ya haraka, na ili nguzo ya mwanadamu pamoja na nidhamu ya dini ibaki
kuwa madhubuti.