bayyinaat

Published time: 28 ,February ,2017      21:07:09
Katika tamaduni za Roma kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a.s) ni kwamba, mwanamke na msichana walitumikishwa kama watumishi bila kujali.........
News ID: 21

DHULMA KWA MWANAMKE KABLA YA UISLAMU

Dhulma kwa mwanamke katika ulimwengu wa kabla ya Uislamu imegawanyika katika vipindi vya aina mbili:

1.                 kipindi cha uhayawani ambayo mwanamke hakutambulika kama mwanadamu na hatimaye kuamiliana naye kwa ukali wa hali ya juu. Na miongoni mwa mikingamo mikubwa iliyomsibu mwanamke, ilikuwa ni mwanaume kumuuza au kumkodisha kwa mwanaume mwingine.

2.                 Kipindi cha tamaduni za kale za Kigiriki, Misri, Roma pamoja na tamaduni za Iran kwa mwanamke hazikumteulia haki yoyote ile ya kimsingi wala ya kijamii, naye alitambulika kuwa ni mfuasi wa mwanamke (Yaani; Kila aliamualo mwanaume juu yake basi yeye hufuata na kutii matakwa ya mwanaume).

MWANAMKE KATIKA BARA LA ULAYA:

MWANAMKE KATIKA MILA NA TAMADUNI ZA KALE ZA UGIRIKI NA ROMA:

Katika tamaduni za Ugiriki mwanamke alihesabika kuwa ni bidhaa ya kibiashara kama bidhaa nyingine, ambaye alikuwa akiuzwa na kununuliwa masokoni, bila kujali shakhsiya yake wala haki zake za kijamii, pia baada ya kufariki mumewe (kwa mujibu wa itikadi zao potovu) ni kwamba alipoteza haki ya kuendelea kuishi. Vilevile mwanaume alikuwa ni mwenye uwezo wa kumkodisha mwanamke kwa mwanaume yeyote ule amtakaye au kumzawadia rafiki yake.

Katika tamaduni za Roma kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a.s) ni kwamba, mwanamke na msichana walitumikishwa kama watumishi bila kujali shakhsiya katika jamii, pia walifananishwa na wanyama. Na walikuwa wakiuzwa na kununuliwa mfano wa bidhaa za kibiashara, alinyimwa haki zake za kijamii. Kama vile alivyokuwa hana haki ya kumrithi mzazi wake au kumiliki kitu chochote kile.

Pia mwanaume alikuwa na haki ya kumkagua mwanamke (kwa mujibu wa itikadi zao potovu) na vilevile  alikuwa na uwezo wa kumhukumu kifo kwa sababu ya kosa lake.

URUSI:

Katika tamaduni za kale za Urusi ilikuwa kwamba Baba alipokuwa akimuoza binti yake, anampeleka ukweni kwake, kisha Bi harusi alipokuwa akifikishwa kwa ukweni, basi Baba anatoa hukumu ya kupigwa bakora na Mumewe, ili ifahamike katika akili za wanawake ya kwamba; Iwapo mwanamke atakuwa ukweni atambue kuwa yeye kupigwa na mumewe ni ada na desturi ambayo ni lazima aifahamu pindi atakapokuwa ukweni.

Vile vile katika tamaduni za kale za Yugoslavia pamoja na Serbia ilikuwa kwamba (Mwanamke alihesabika kuwa ni fungu katika mafungu ya ngawira za kivita) pia wanawake kuporwa na kuibiwa ni jambo ambalo liliendelea kuenea hadi karne iliyopita.

MWANAMKE KATIKA MTAZAMO WA DINI ZA KIYAHUDI NA KIKRISTO:

Kwa mujibu wa dini ya Kiyahudi, ni mfano wa zile itikadi potovu za Waarabu kabla ya Uislamu, kwamba; Anapozaliwa mtoto wa kike basi humhesabu kuwa ni nuksi kwa baba, pia Mama huyo alijifungua mtoto wa kike naye pia alihesabika kuwa ni nuksi kwa muda wa siku kumi tano hadi sabini. Hivyo mwanamke (Kwa mujibu wa dini hizo) alikuwa ni fungu katika mafungu ya urithi wa Baba wa familia.

Vilevile katika jamii za Kikristo mfano; Italia na Hispania, baada ya midahalo mingi iliyojiri baina yao ikapelekea kuitikadi  ya kwamba katika wanawake wote ulimwenguni Mariam (a.s) ni mwanamke pekee aliyekamilika na mwenye roho ya milele, na kwamba wanawake baki wamekosa sifa ya uanadamu katika jamii, na kuongezea hilo ni kwamba hana roho ya milele, hivyo huhesabika kuwa ni jahanamu ililokuwepo baina ya mwanadamu na mnyama.

Kwa msingi huu ni kwamba, wako baadhi huamini ya kwamba ni bora baada ya kifo cha mwanaume, mkewe naye asibaki hai, yaani azikwe pamoja naye akiwa hai, kwani iwapo ataendea kuishi basi hana haki ya kuolewa tena na mwanaume mwingine.

MISEMO YA WAMAGHARIBI KUHUSIANA NA MWANAMKE:

Katika wa watu wa magharibi imeenea misemo ambayo ni ya kustaajabisha mno kuhusiana na mwanamke. Ambayo miongoni mwake ni hii ifuatayo:

v    Mwanamke, ni kiumbe mfano wa kizingiti na mpungufu wa akili.

v    Mwanamke, ni kiumbe wa duni mithili ya hayawani ambaye humaliza matamanio ya mwanaume. 

Waingereza:

v    Mwanaume anapomchukua mwanamke ni mfano wa mtu anayelea nyani.

v    Wanawake ni mikia ya Shetani.

Wajerumani:

v    Mwanaume ni mwenye maumbile ya Malaika, moyo wake ni wa nyoka na hisia zake ni mfano wa punda.

v    Matendo yote ya Shetani huyakabidhi kwa wanawake kuyatekeleza.

Wagiriki:

v    Mambo matatu ni mkosi: Mwanamke, moto pamoja na tufani (Kimbunga).

Na misemo mingine mingi zaidi ya hiyo inayoshusha hadhi pamoja na shakhsiya ya mwanamke na vilevile kumnyima haki zake za kisheria.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: