bayyinaat

Published time: 31 ,January ,2018      14:43:48
News ID: 218

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Iran wenye sifa ya jamhuri na Uislamu ni kumbukumbu ya Imam Ruhullah Khomeini MA mwasisi na mwanzishi wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kwamba, wananchi wa taifa hili katu hawatambufia macho mfumo huu wenye sifa hizi mbili.
Rais Rouhani amesema hayo asubuhi ya leo akiwa katika haramu ya Imam Khomeini MA kwa mnasaba wa kukaribia kumbukumbu ya mwaka wa 39 wa maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kwamba, madola ya kibeberu yanapaswa kudiriki kwamba, taifa la Iran lina uhuru na mamlaka ya kkitaifa na litaendelea kulinda hilo.
Rais Hassan Rouhani amebainisha kwamba, hakuna mtu mwenye uwezo wa kulizuia taifa la Iran kutoa maoni, kukosoa na hata kulalamikia jambo fulani na kwamba, viongozi wa serikali wanapaswa kusikiliza matakwa ya wananchi.
Rais wa Iran aidha amesema kuwa, Uislamu, wananchi na nchi ya Iran ni misingi mikuu mitatu na kuongeza kuwa, wananchi wa Iran wanauenzi umoja wa kitaifa na kwamba, hakuna dola lolote lile la kibeberu lenye ubavu wa kubadilisha muelekeo wa taifa hili.
Rais Rouhani ameashiria kufanyika chaguzi 12 za Rais, chaguzi 10 za Bunge, chaguzi 5 za Baraza la Wanazuoni Linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, chaguzi 5 za Mabaraza ya Miji na kura kadhaa za maoni nchini Iran na kusisitiza kwamba, wananchi wa Iran kwa mara nyingine tena tarehe 11 mwezi huu ambayo ndio siku ya kumbukumbu ya maadhimisho yya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu wataonyesha ni kwa kiwango gani ni watiifu kwa Mapinduzi, mfumo wa Kiislamu na Kiongozi Muadhamu wa Mapainduzi ya Kiislamu.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: