bayyinaat

Published time: 02 ,March ,2018      01:33:04
News ID: 249
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na kundi la maulamaa wa Syria na kusisitizia wajibu wa kushikamana vilivyo na mambo yanayowaunganisha pamoja Waislamu wote. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa: Ni matumaini yetu sote tutaiona siku ambayo mtasali Swala ya jamaa mjini Beitul Muqaddas na siku hiyo haiko mbali tena, bali itafika karibuni hivi, ni sawa tu kama watu kama sisi tutakuwa bado tupo au hatupo tena.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo hayo na Waziri wa Wakfu wa Syria Dk. Mohammad Abdul-Sattar al-Sayyed na ujumbe wa maulamaa alioongozana nao hapa Tehran kwamba, adui hawezi kufanya jeuri yoyote iwapo viongozi wa nchi na mataifa ya eneo hili watachukua maamuzi thabiti kuhusu suala la muqawama.
Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa Syria leo hii iko katika mstari wa mbele wa muqawama na akasema kama ninavyomnukuu "Ni jukumu letu kuunga mkono kusimama kidete nchi ya Syria." Mwisho wa kunukuu. 
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, mheshimiwa rais wa Syria Bashar al Assad amedhihirika katika sura moja ya mwana mapambano na mwana muqawama mkubwa na kwamba yupo imara na hakuna shaka yoyote kuhusu Rais a l Assad; na jambo hilo ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile. 
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, nchi hizi za Kiislamu tunazoziona zinaishi katika hali duni lakini si dhalili bali viongozi wake ndio madhalili. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, iwapo nchi hizo zingekuwa na viongozi wanaohisi kuwa na heshima na izza kutokana na Uislamu na utambulisho wao, basi nchi hizo zingekuwa bora kabisa na adui asingethubutu kuchukua hatua yoyote dhidi ya nchi hizo. 
Akiendelea na mazungumzo na Waziri wa Wakfu wa Syria na ujumbe alioongozana nao hapa Tehran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Iran imeingia katika mwaka wa 40 wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema, tangu siku ya kwanza kabisa ya ushindi wa mapinduzi hayo matukufu, madola yote makubwa duniani yalishikamana na kuchukua hatua dhidi ya Iran. Marekani pia, vile vile Umoja wa Kisovieti, Nato na nchi karibu zote za Kiarabu na eneo hili zilikuwa pamoja na mabeberu katika hilo, hata hivyo taifa la Iran hadi leo lipo imara bali limepata maendeleo makubwa.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: