bayyinaat

Published time: 02 ,March ,2018      01:34:34
News ID: 250
Kongamano la kimataifa la Kiislamu la kupambana ugaidi limefanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambapo wanazuoni walioshiriki katika kongamano hilo wametaka nchi zote duniani zichukue hatua kali dhidi ya waungaji mkono wa ugaidi.

Hayo yamebainika katika Kongamano la 28 la Kimataifa la Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu lilifanyika Jumatatu na Jumanne mjini Cairo ambapo wanazuoni, wanafikra na wataalamu kutoka nchi 50 walishiriki ambapo mada kuu ilikuwa ni: "Kadhia ya Ugaidi na Njia za Kukabiliana Nayo."
Taarifa ya mwisho ya kongamano hilo imesisitiza juu ya haja ya serikali na tawala kuchukua hatua kali za kukabiliana na ugaidi na pia kuweza kuvuka vizingiti katika jitihada za kufikia lengo hilo.
Aidha washiriki wa kongamano la kimataifa la Kiislamu la kupambana ugaidi wamesema kwamba, jamii zina jukumu ya kutangaza msimamo imara wa kupinga kikamilifu ugaidi na magaidi. 
Kadhalika taarifa hiyo imetaka kuchukuliwa hatua za kusitisha misaada ya kifedha na misaada mingine yote ambayo huyafikia makundi ya kigaidi. Washiriki katika mkutano huo pia wametilia mkazo umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha umma kuhusu njia za kukabiliana na ugaidi.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: