bayyinaat

Published time: 02 ,March ,2018      01:35:54
News ID: 251
Wapalestina 35 wameuawa shahidi na wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel tangu Rais Donald Trump wa Marekani aitangaze Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel Disemba mwaka jana.
Ripoti kutoka Palestina zinasema kuwa, baada ya rais wa Marekani kuitangaza Beitul-Muqaddas Disemba 6 mwaka jana kuwa mji mkkuu wa utawala dhalimu wa Israel miji ya Wapalestina imekuwa ikishuhudia mapigano baina ya wanajeshi wa utawala huo ghasibu na Wapalestina.
Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina kimesema katika ripoti yake kwamba, jumla ya Wapalestina 35 wameuawa shahidi tangu kutangazwa uamuzi huo wa Rais wa Marekani.
Aidha inaelezwa kuwa, kati ya waliouawa shahidi wamo watoto 11 wa Kipalestina wenye umri wa chini ya miaka 18.
Ijumaa iliyopita, Heather Nauert, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alitangaza azma ya nchi hiyo kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv, mji mkuu wa utawala haramu wa Israel kwenda mji wa Quds, tarehe 14 Mei mwaka huu.
Itakumbukwa kuwa, Mei 14 itasadifiana na Siku ya Nakba, inayokumbushia tukio la kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala ghasibu wa Israel mnamo mwaka 1948, yaani miaka 70 iliyopita.
Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitangaza Quds Tukufu (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa Israel iliibua makelele na malalamiko mengi katika kona zote za dunia.
Wakati huo huo, Wakristo wa mji wa Quds wamefurahishwa na hatua ya kufunguliwa upya kanisa kuu la 'Al-Qiyamah' baada ya kufungwa kwa siku kadhaa na utawala haramu wa Israel na kuitaja hatua hiyo kuwa ni katika safari ya kuelekea ushindi kamili dhidi ya Wazayuni hao wanaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: