bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:44:04
Hakika amebainisha Mwenyezi Mungu mtukufu ya kwamba Vilevi ni katika amali za sheitani katika kauli yake: “مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ” “katika kazi ya Shetani” na kila jambo ambalo kwamba hutokana na amali za sheitani ni haramu, na hiyo ni kwa sababu kwamba sheitani ni mwenye pupa ya kuwapotosha wanadamu, na kuwatupia katika maangamio.
News ID: 264


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

DALILI YA TATU: HAKIKA VILEVI NI KATIKA AMALI ZA SHEITANI

Hakika amebainisha Mwenyezi Mungu mtukufu ya kwamba Vilevi ni katika amali za sheitani katika kauli yake: "مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ "katika kazi ya Shetani” na kila jambo ambalo kwamba hutokana na amali za sheitani ni haramu, na hiyo ni kwa sababu kwamba sheitani ni mwenye pupa ya kuwapotosha wanadamu, na kuwatupia katika maangamio.

Na utakapotambua ya kwamba vilevi ni katika amali za sheitani hakika tambua ya kwamba sheitani hakukuletea chochote isipokuwa akudanganye na kukutoa katika njia iliyokuwa sawiya, na ili kuzua baina yako na ndugu yako uhasama!

Na sheitani ni adui wa mwanadamu, na amekwisha tutahadharisha Mwenyezi Mungu kwa tahadhari kali, aliposema (s.w.t):

«إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ».

"Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni”.

Na ametuhabarisha ya kwamba Yeye amefanya vitimbi kwa Adam na Hawa na ikawa ni sababu ya kuondolewa kwao katika pepo, na akawaapia ya kwamba atakuwa ni mwenye kuwanasihi na ilihali ni muongo, na amesema (s.w.t):

«وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ».

"Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini”.

Na ametutahadharisha Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na adui huyu katika kauli yake nyingine tukufu:

«يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ».

"Eny wanaadamu! Asije Shetani kukufitinini kama alivyo watoa wazazi wenu Peponi”.

Na sheitani huyu ni adui kwa mwanadamu na ni mwenye pupa ya kumpotosha, na vilevi, masanamu na kupiga ramli ni katika amali zake, yaani yeye ndiye ambaye aliyevileta, na yeye ndiye anayewashawishi waja kuviendea, na ambaye amewapambia kuvipenda na kuwadumbukiza ndanimo.

Na utakapotambua kitu ambacho ni katika amali za sheitani ni wajibu wako kujitenga nacho mbali na kukiacha ili usalimike, kwani atakacho ni kukuangamiza, na hataki kingine ila kukupotosha.

Na vile vile sheitani ni mwenye kuambatana kwa moyo wa mwanadamu, na kumtia wasiwasi katika kifua chake, na ameshusha Mwenyezi Mungu katika hilo sura, nayo ni hitimisgo la sura za Qur’ani, amesema (s.w.t):

«قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَهِ النَّاسِ مِنْ شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ».

"Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, Mfalme wa wanaadamu, Mungu wa wanaadamu, Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, Kutokana na majini na wanaadamu”.

Na hakika shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas ni sheitani, ametuamrisha Mwenyezi Mungu kujilinda kwa Mola wa watu, na Mungu wa watu kutokana na shari ya huyu sheitani, ambaye hufika katika vifua na kutia wasiwasi ndani yake na kujenga shari pia, na kumuita, na kumpambia shari kwa mandhari ya heri, na kupendezesha fikira za watu kuvielekea, na kuwasukuma msukumo wa kuvikimbilia.

Lakini amejaalia Mwenyezi Mungu mtukufu kundi lake na watu wake ngao na kimbilio kutokana na shari ya sheitani, na akateua wema na wabora katika waja wake kuwa ni salama kwao kutoka na shari ya huyu sheitani, na akawasamilisha kutokana naye, amesema tena (s.w.t):

«إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ».

"Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata”.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: