bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:51:38
“Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu” na amesema tena (s.w.t) kuhusu yeye:
News ID: 265


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

MUENDELEZO WA DALILI YA TATU…

Na tutakapotambua uadui wa sheitani huyu hakika tutafahamu ya kwamba amekwisha sisitiza ya kwamba atakuja na kila hila, na ataleta kila kitendea kazi ili kupotosha wanadamu, na ndipo anapokumbusha Mwenyezi Mungu kuhusu yeye katika kauli yake aliposema:

"وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّهِ

"Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu” na amesema tena (s.w.t) kuhusu yeye:

"لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا

"hapana shaka nitawaangamiza dhuria zake isipokuwa wachache tu”.

Yaani dhuria wa Adamu ila wachache, na Mwenyezi Mungu akatutahini na kumchelewesha, na amesema kumwambia:

"قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ

"Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula”. Na amesema tena kumwambia:

"اذْهَبْ فَمَنْ تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً مَوْفُورًا وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِمْ بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ

"Akasema Mwenyezi Mungu: Ondokelea mbali! Atakaye kufuata katika wao, basi Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo ya kutimia. Na wachochee uwawezao”.

Yaani wapelekee kila aina ya hila, na uwamiliki kwa nguvu zote, na watumikishe kwa kila aina ya wasila uwezavyo, na sheitani ni mwenye pupa juu ya kumpotosha mwanadamu na atafanya jitihada yake ya kumghuri.

Na aina hii ni katika viumbe wake wenye nafasi, na wenye kudura juu ya mwanadamu, na amekwishatuhabarisha Mtume (s.a.w.w) ya kwamba anatembea ndani ya mwanadamu katika mapito/ mirija ya damu, yaani hupenya ndani ya mwanadamu na kufika katika viungo vyake na kutembea ndani ya mwili wake, kama itembeavyo damu ndani ya mwili wake, na amesema (s.a.w.w) ya kwamba: "Hakika Sheitani hutembea katika wanadamu kama ambavyo itembeavyo damu”.

Na anamshawishi katika moyo wake na ilihali yeye hamwoni, amesema (s.w.t):

«إِنَّهُ يرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيثُ لَا تَرَوْنَهُمْ».

"Hakika yeye na kabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni”.

Hii ni kwa maana kwamba: Yeye na wale ambao wako katika maumbile yake katika majini na mfano wao ambapo hatuwaoni, na amejaalia Mwenyezi Mungu kinga na herizi zituzuiazo kutokana nao, na kumtii Mwenyezi Mungu mfano ni kinga kutokana na sheitani, na kumdhukuru Mwenyezi Mungu ni kinga kutokana na sheitani, na ibada kwa ukamilifu wake na kisomo cha Qur’ani kwa kutadabari, na vile vile dhikiri ni kinga pia kutokana na sheitani na aidha kumsabihi Mwenyezi Mungu, na mfano wake. Na kinga hizi hukuepusha kutokana na Sheitani wakati wowote uzitamkazo kwa ikhlaas/ nia safi na ukweli, kwa hakika zitakuepusha na kukunufaisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Na natija ni kwamba vitu hivi ambavyo ni kamari, vilevi, masanamu na kupiga ramli amevifanya Mwenyezi Mungu sababu ya kuviharamisha kwake ni kuwa kwake ni katika amali za sheitani, kwa maana kwamba yeye ndiye ambaye amevitumia na kuwaita watu kuviendea, na yeye ndiye ambaye amehamasisha watu kuabudu masanamu pasi ya Mwenyezi Mungu!! Na yeye ndiye ambaye amewaita watu kunywa pombe!! Na yeye ndiye anawaita kubeti kamari hii!! Na yeye ndiye ambaye anawaita wajifunze kuchonga masanamu na kupiga ramli!! Na yote haya ni katika amali za sheitani rajimu.

Na endapo utayatambua hayo basi jiepushe ili usalimike na vishawishi vya sheitani rajimu, anasema Mwenyezi Mungu (s.w.t):

«إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ».

"Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani”.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: