bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:52:51
“Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki”. Kwa maana kwamba Sheitani ni mwenye haraka na kiu kubwa ya kumuingiza mwanadamu katika chuki na uadui, na uadui ni kuvunja undugu baina ya ndugu wawili, na marafiki kuvunja urafiki wao kwa kuchukiana na kutengana, na yote hayo ni kwa sababu ya pombe na kamari, kama asemavyo (s.w.t):........
News ID: 266


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

DALILI YA NNE: AMRI YA KUEPUKA KAMARI

Ameamrisha Mwenyezi Mungu kujiepusha na manne haya, ambayo ni pombe, kamari, masanamu na kupiga ramli, na kujiepusha kwa madhumuni yake ni kukoma, yaani: Jitengeni mbali navyo, ambayo ni kubwa zaidi kuliko kusema, viacheni, na kuacha haina maana ya muktadha wa kujiweka mbali, lakini kujiepusha ni yenye kina zaidi, yaani wekeni kando, na nendeni kando nyingine mbali navyo. Na jiepusheni mbali ni vinne hivi.

Na kujitenga mbali na Kamari ni jambo lisilo na shaka ndani yake, na kuikirubia ni sababu ya kudumbukia ndani yake au ni wasila katika wasila wa kuingia katika Kamari, kwa hiyo ametuamrisha Mwenyezi Mungu kujiepusha kwa maana ya kujitenga mbali, na wala usiwakurubie wacheza Kamari wala kusahibiana nao wala kurafikiana nao wala kuamiliana nao wala usiwapende na kukaa pamoja nao wala usipendane nao; bali kujiweka mbali nao ni kuepuka ili kulinda yako heshima, na ili kusalimisha dini yako na itikadi yako, kwani inaogopeka kwamba endapo utashikamana na vitu hivi, au utakapokaa pamoja na wacheza Kamari kwa mfano, au wenye kupingia Kamari na wenye kunywa pombe na mfano wake inatazamiwa kuporomosha heshima yako, na inaogopeka ya kwamba kuwakaribia ni sababu ya kuingia chembe ya kitu katika nafsi yako hata japo kidogo, au ukapenda kitu katika hayo na mfano wa hayo, na hii ikawa ni sababu ya kuwa Mwenyezi Mungu ametuamuru kujitenda mbali navyo, kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t): "فَاجْتَنِبُوهُ "Basi jiepusheni navyo” kwa maana kwamba mjitenge mbali na mambo hayo.

DALILI YA TANO: KUPATA UFAULU KWA KUACHA KAMARI

Na hiyo ni kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t) isemayo kwamba: "لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ” "ili mpate kufanikiwa” na mafanikio ni kufuzu na ushindi na saada ya dunia, na aidha saada ya akhera na kufikia malengo na makusudio, na huu ndio ufaulu/mafanikio, na mwenye kufanikiwa ni yule ambaye kwamba atapata makusudio yake siku ya Kiama.

Lakini ni wakati gani yatapatikana kwako mafanikio?!

Na utakapojitenga na mambo haya ikiwepo Kamari ndanimo, na utakapojiepusha mbali navyo na kuvichukia, hakika wewe ni katika wale waliofuzu, kwa maana kwamba yatarajiwa kwako kuwa ni katika watu watakao faulu, na hiyo ni sababu katika mafungamano ya Mwenyezi Mungu juu ya kujitenga kwako mbali na vitu hivi na miongoni mwake ikiwemo Kamari. Na kitu ambacho kipatikanacho bi mafanikio kwa kujitenga kwake, na kupata maangamio kwa kuvikurubia, na kutokea umwagaji damu kwa kuvifanya, na kupatikana upotovu kwa kupingia Kamari, hapana shaka ya kwamba Kamari imeharamishwa.

DALILI YA SITA: HAKIKA VILEVI HUIBUA UADUI BAINA YA WATU

Anasema (s.w.t):

{إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ}

"Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki”.

Kwa maana kwamba Sheitani ni mwenye haraka na kiu kubwa ya kumuingiza mwanadamu katika chuki na uadui, na uadui ni kuvunja undugu baina ya ndugu wawili, na marafiki kuvunja urafiki wao kwa kuchukiana na kutengana, na yote hayo ni kwa sababu ya pombe na kamari, kama asemavyo (s.w.t):

{ إِنَّمَا يرِيدُ الشَّيطَانُ أَنْ يوقِعَ بَينَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيسِرِ }.

"Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari”.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: