bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      22:07:24
Na hapa tutaje baadhi ya mifano ambayo imetokea kwa sababu ya kamari, na miongoni mwa mifano hiyo ni pale watu wachezapo kamari kisha kubeti kwa atakayeshinda kupokea pesa, na mmoja wao ashindapo huchukua pesa hiyo, na endapo pesa hiyo itakuwa ni nyingi hakika watu waliwao hupelekea kubaki maskini, na kukabiliwa na shida, na kuwa mafukara na wenye kuhitaji mikopo, na vile vile hupelekea kutafuta pesa kwa njia tofauti ili kulipiza kiasi alicholiwa.
News ID: 267


بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Idadi ya ushahidi:

DALILI YA SABA: HAKIKA KAMARI HUANZISHA CHUKI BAINA YA WATU

Bughudha ni; mtu kumchukia Mtu mwingine, na kumkasirikia, na kuchukia matendo yake na kazi zake, na itakapo patikana bughudha basi itapatikana athari ya kutengana na kufarakana vitu ambavyo husababisha mfarakano baina ya Waislamu.

Na hapa tutaje baadhi ya mifano ambayo imetokea kwa sababu ya kamari, na miongoni mwa mifano hiyo ni pale watu wachezapo kamari kisha kubeti kwa atakayeshinda kupokea pesa, na mmoja wao ashindapo huchukua pesa hiyo, na endapo pesa hiyo itakuwa ni nyingi hakika watu waliwao hupelekea kubaki maskini, na kukabiliwa na shida, na kuwa mafukara na wenye kuhitaji mikopo, na vile vile hupelekea kutafuta pesa kwa njia tofauti ili kulipiza kiasi alicholiwa.

Na vile vile wengine huchoka kuzikusanya, kisha akacheza mchezo wa kisheitani, na mwingine akazila bila kuzisumbukia na kuzisotea, hakika hali hiyo itaibua chuki dhidi ya mlaji, na ikiwa atamchukia lazima kutokee baina yao uadui, na wakati mwingine chuki hiyo hupelekea vita na mzozo baina yao, na uibukapo mzozo ndipo unasababisha tofauti za kauli baina ya Waislamu (endapo watajihusisha na michezo ya kisheitani), na kutengana, na yote hayo hupelekea maadui wao kuwa wenye nguvu dhidi yao na kufilisi mali zao, na kuchukua miji yao, yote hayo ni kwa sababu ya pombe na kamari.

Na Mwenyezi Mungu ameamrisha Waislamu kuwa ni ndugu wapendanao, na waondoe yote yachocheayo chuki na uadui pamoja na uhasama, na amewaamrisha kuungana, na akawaita kwa jina la Waislamu, na akawaneemesha neema ya undugu wa dini, amesema (s.w.t):

«وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَى شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا».

"Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo”.

Na Mwenyezi Mungu akajaalia kwa umoja huo neno lao baada ya mfarakano, na kwa undugu wao baada ya kutengana, na kupendana kwao baada ya kuwa ni maadui, na kuungana nyoyo zao muungano ambao hauwezi yeyote ila anayejua ya ghaibu kuwa ni moja, amesema (s.w.t):

«وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنْفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ».

"Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeliweza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha”.

Na akatuongoza kuwa ni wajibu juu yetu kuwa ni wenye kuungana, na anakirihishwa kuwa kwetu ni wenye kuchukiana na kutengana, na ni wajibu juu ya waumini kuwa ni kitu kimoja, na kusaidiana, na ameamrisha Mwenyezi Mungu hilo ndani ya kauli yake tukufu isemayo:

« وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ».

"Na saidianeni katika wema na uchamungu, wala msisaidiane katika dhambi na uadui”.

Na ametuamrisha (s.w.t) pindi utokeapo mzozo baina ya makundi mawili tufanye jitihada za kusuluhisha baina yao hadi waungane, amesema (s.w.t):

«وَإِنْ طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِنْ بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَى فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّى تَفِيءَ إِلَى أَمْرِ اللَّهِ فَإِنْ فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ».

"Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki. Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu”.

Na ametuamrisha Mwenyezi Mungu kusuluhisha baina yao, na amewaita kuwa ni ndugu zetu, na lau kama watapigana, na akaamuru kupeana mikono, kwa sababu wao ni ndugu, lakini kitu hichi ambacho ni kamari hakika hubomoa undugu huo, na kuibua uadui, chuki, uhasama, kutengana na mengine vitu ambavyo Mwenyezi Mungu ametukataza na Mtume wake (s.a.w.w) kutukemea.

Na tutakapotambua kitu hiki, na tukatambua madhara yake juu yetu hapana shaka ni wajibu wetu kujiepusha na kujitenga mbali navyo.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: