bayyinaat

Published time: 03 ,March ,2017      19:03:47
Kwa itikadi ya kila Mwislamu ni kwamba Sala ni nguzo ya dini, na Sala ni ngazi ya mja kumfikia Mola wake. Mtu anapokuwa ameacha Sala huwa........
News ID: 27

Umuhimu wa Sala katika kauli za Mtume(s.a.w.w).

 

 1. Sala humzuia mwanadamu kutenda maovu.
 2. Sala ni miiraji ya Muumini.
 3. Sala ni chanzo cha kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
 4. Sala ni amali bora inayomkurubisha mwanadamu kwa Mola wake.
 5. Sala ni nguzo ya dini.
 6. Sala ni nuru ya Muumini.
 7. Sala ni ngao ya vitimbi vya Sheitani.
 8. Sala ni ufunguo ya pepo.
 9. Sala ni gharama ya pepo.
 10. Sala ni bora kuliko Hijja.
 11. Sala ni amali bora mno mbele ya Mwenyezi Mungu.
 12. Sala ni nuru ya macho yangu (Mtume (s.a.w.w)).
 13. Kupitia sala huridhia Mwenyezi Mungu amali za Muumini.
 14. Sala ni sera za Manabii.
 15. Sala ni ripoti nzuri waipendayo Malaika.
 16. Sala ni taa ya moyo wa Muumini.
 17. Kupitia sala hujibiwa dua  za Muumini.
 18. Sala ni mnong’ono pamoja na Mwenyezi Mungu.
 19. Sala hushusha rehema za Mwenyezi Mungu.
 20. Sala ni nuru ya uso wa Muumini.
 21. Sala ni Baraka kwa taifa.
 22. Sala huzidisha riziki ya mja wa Mwenyezi Mungu.
 23. Sala ni silaha ya Muumini kwa adui.
 24. Sala ni kafara ya madhambi.
 25. Sala ni mahari ya Huurul-Ain.
 26. Sala ni kibali cha kuvuka daraja la sirat.
 27. Sala ni nuru na kivuli siku ya kiama.
 28. Sala ni taji ya kichwani ya muumini siku ya kiyama.
 29. Sala ni taa la kaburini.
 30. Sala ni uokovu wa mwili kutokana na moto wa jahanamu.
 31. Sala ni maandalizi ya Muumini akhera.
 32. Sala ni tegemeo bora kaburini.
 33. Sala ni ponyo baina ya mtu na Malaika wa mauti.
 34. Sala humuepusha Muumini na moto wa jahanamu.
 35. Sala ni jawabu la Munkar na Nakiir kaburini.
 36. Sala ni ripoti ya kukubaliwa amali za Muumini.
 37. Sala ni utulivu wa mwili wa Muumini.
 38. Sala ni swali la kwanza siku ya kiyama.
 39. Sala ni kafara ya amali isiyo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu.
 40. Sala ni amali bora zaidi baada ya mja kumfahamu Mola wake Mlezi.[1]

SALA

Kwa itikadi ya kila Mwislamu ni kwamba  Sala ni nguzo ya dini, na Sala ni ngazi ya mja kumfikia Mola wake. Mtu anapokuwa ameacha Sala huwa anakuwa amekata mawasiliano baina yake yeye na Mola wake, kwa ajili hiyo zimepokelewa hadithi nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Baiti  ya kwamba: tofauti baina ya Uislamu na ukafiri ni; kuacha Sala au kujivua Uislamu.

KUMBUKUMBU

Siku ambayo Mfalme wa Iran alipotoroka nchini Iran, Imamu aliuhutubia ulimwengu alipokuwa mjini Paris huku akizungukwa na waandishi wa habari na stesheni mbalimbali za televisheni.

Siku hiyo, ilikuwa ni siku nzuri katika historia ya Iran, pia ujumbe ule wa Imamu Khomeini ulikuwa ni ujumbe muhimu mno kwa walimwengu.

Wakati huo Imamu alikuwa amekaa kwenye kiti akitoa hotuba kwa umma, punde akamuuliza mwanae aliyekuwa pembezoni mwake: Je! Muda wa Sala haujafika?, akamjibu kuwa: Ndio muda wa Sala umewadia.

Imamu ambaye alikuwa akihutubia dunia alikatiza maongezi yake na kuelekea kusali. Waandishi wote wa habari walitahayari sana na kujiuliza kwa nini ghafla amekatiza hotuba yake muhimu?. Wakaambiwa kuwa: ((Imamu huwa ana maongezi na Mola wake kila unapofikia muda wa Sala, na muda huo unakuwa si kwa ajili ya watu)).[1] Biharul-Anwar, Anwarun-Nu’umaan, Nahaayil-Akhbaar, Ghurur

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: