bayyinaat

Published time: 14 ,March ,2018      11:41:43
News ID: 272



Wasiwasi umetanda katika jamii ya Waislamu nchini Uingereza baada ya kundi lenye chuki dhidi ya Uislamu kusambaza barua za kuhimiza kuhujumiwa Waislamu na misikiti nchini humo.
Taarifa zinasema wakaazi wa mji wa London na maeneo ya West Midlands na Yorkshire wamesema wamepokea barua hizo, zinazowataka kufanya hujuma dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada mnamo Aprili 3, siku ambayo wameitaja kuwa  'Siku ya Kumwadhibu Mwislamu'.
Sehemu moja ya barua hiyo imetangaza zawadi ya pointi 10 kwa kumshambuliwa kwa matusi Muislamu, pointi 50 kwa yule atayemwagia tindikali Mwislamu, pointi elfu moja kwa atakayeshambulia msikiti, na pointi 2,500 kwa yule atakayekishambulia kwa silaha za nyuklia kibla cha Waislamu, Al Kaaba, katika mji mtakatifu wa Makka.
Miqdaad Versi, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Uingereza amelaani vikali kusambazwa barua hizo zinazoashiria kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, lakini pia amebainisha kuwa kitendo hicho kimewaweka Waislamu wa nchini Uingereza katika hali ngumu. Aidha ametoa wito kwa polisi kuwakamata wanaoeneza barua hiyo ya chuki na kuwafikisha kizimbani.
Kuna Waislamu karibu milioni tatu nchini Uingereza na hivyo kuufanya Uislamu kuwa dini ya pili kwa ukubwa katika nchi hiyo ya bara Ulaya.
Tell MAMA, taasisi inayochunguza vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu imelaani hatua hiyo na kusema hali ya taharuki imeenea katika jamii ya Waislamu nchini Uingereza.
"Barua hii imeibua hofu kubwa katika jamii,” amesema Iman Atta, mkurugenzi wa Tell MAMA.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Waislamu barani Ulaya hususan Uingereza, katika miaka ya hivi karibuni wameanzisha kampeni za kuwafahamisha wasiokuwa Waislamu mafundisho ya Uislamu ili kuondoa fikra potofu miongoni mwao kuhusiana na dini hii.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: