bayyinaat

Published time: 14 ,March ,2018      11:43:09
News ID: 273
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wameulaumu mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook kuwa, umehusika na uchochezi wa mauaji ya umati dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar.
Kwa mujibu wa Marzuki Darsuman, Mwenyekiti wa Kamati Huru ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Kutafuta Ukweli Kuhusu Myanmar, ni kuwa, mitandao ya kijamii imekuwa na nafasi kubwa katika kuchochea mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu.
Amesema maandishi na taswira za kuchochea mauaji ya Waislamu wa Myanmar zimekuwa zikisambazwa kupitia Facebook pasina mtandao huo wa kijamii kuchukua hatua kuzuia au kufuta propaganda hizo za kichochezi.
Mkaguzi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia faili la Myanmar Yanghee Lee amesema Facebook ina nafasi muhimu katika maisha ya umma na binafsi nchni Myanmar na serikali ya nchi hiyo hutumia mtandao huo wa kijamii kueneza taarifa kwa umma. Amesema badala ya Facebook kuleta pamoja jamii nchini Myanmar imetumika kama chombo chakuchochea maangamizi ya umati ya Waislamu.
Kuanzia Agosti  25 mwaka huu hadi sasa vikosi vya usalama vya Myanmar vimechoma moto vijiji visivyopungua 350 katika eneo la Waislamu huko Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.
Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu. Hadi sasa  jinai hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki saba wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.
Zeid Ra'ad Al Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: