bayyinaat

Published time: 08 ,April ,2018      19:35:40
Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Ali Mohammadi, Mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran katika ba kuongeza kuwa kutakuwa mashindano manne tofauti ya Qur’ani katika duru ya mwaka huu.
News ID: 291

Nchi 23 zimetangaza azma ya kushiriki katika Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baadaye mwezi huu.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Ali Mohammadi, Mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran katika ba kuongeza kuwa kutakuwa mashindano manne tofauti ya Qur’ani katika duru ya mwaka huu.

Amesema mbali na mashindano ya kawaida kutakuwa na mashindano maalumu ya wanawake, wanafunzi wa shule na pia mashindano maalumu ya wenye ulemavu wa macho. Aidha amesema kuwa, kwa ujumla mashindano ya mwaka huu yatakuwa na washiriki zaidi ya 300.

Hujjatul Islam Ali Mohammadi pia amesema kuna mpango wa kuandaa kongamano la kimataifa la utafiti wa Qur'ani ambapo mada kuu itakuwa namna ya kupambana na uistikbari kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu na Sirah ya Ahul Bayt AS.

Aidha ameashiria kuhusu mpango wa kuhifadhi Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema hadi sasa watu milioni 2 wamejisajili kushiriki katika mpango huo wa kitaifa ambao unasimamiwa na Shirika la Wakfu la Iran.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: